Mbona Kabendera hakuchangiwa? (maswali tata michango CHADEMA)

Mbona Kabendera hakuchangiwa? (maswali tata michango CHADEMA)

Wakati hukumu ya mwanahabari Eric Kabendera imetoka na kuamuriwa Alipe zaidi ya fedha za kiTanzania milioni mia mbili sikuona wanaharakati, wanahabari wala wafadhili wakichangisha fedha.

Kwa hukumu hiii iliyotoka dhidi ya viongozi waandamizi wa chama kikuu cha upinzani nchini nimeona ni ajabu kampeni za michango karibu dunia nzima ili kupata fedha za Kitanzania milioni mia tatu na hamsini, cha kustaajabisha sasa hata pamoja na Mashinji kuhama chama na kuchangiwa na chama chao kipya kiasi cha shilingi milioni thelathini, hivyo kufanya deni lililbakia kuwa milioni mia tatu na ishirini lakini wachangishaji bado wamesisitiza kuwa hela wanayotakiwa kulipa ni 350,000,000.

Nashindwa kuelewa Kabendera alikuwa na deni la zaidi ya milioni 200. Wale wote waliokuwa wanatembeza hashtag hawakujiongeza kufanya kampeni ya michango, na chama kikuu upinzani nchini kimeshindwa kulipa fedha hizo licha ya ruzuku, mishihara yao ya ubunge na wahisani.
Kwa nini mtu akiomba msaada wa kumlipia mwanae ada ili akasome mnakuwa wagumu lakini mtu huyo huyo akiomba fedha ili kijana wake afunge ndoa mnachanga?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe hujatoa wazo la kumchangia wakati ule inakuwaje leo ndo unabwekabweka hapa eti kwa nini kabendera hakuchangiwa! Who are you by the way?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom