Mbona hivi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbona hivi?

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by MgonjwaUkimwi, Nov 22, 2007.

 1. M

  MgonjwaUkimwi JF-Expert Member

  #1
  Nov 22, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 1,288
  Likes Received: 521
  Trophy Points: 280
  Mbona hivi? Jamaa aliyekatika kidole kwenye ajali anapiga kelele masaa kadhaa, aliyekatika shingo yuko kimyaaaa!!

  Mbona hivi? Mtu akikaa uchi bila kukusudia na huku akiwakodolea macho wanaomwangalia kwa mshangao, wanaomwangalia wanasemezana kwamba ni malaya, wakati akikaa uchi kwa makusudi huku akisoma gazeti, wapita njia watamsaidia wakizani kakosea!!

  Mbona hivi? Majuu wahuni uvalia suluari zao magotini wakati watu wenye heshima zao bongo uvalia tumboni/kwapani!! wahuni wa bongo watavalia wapi, na wenye heshima zao majuu watavalia wapi??

  Mbona hivi? Mwalimu anayelipwa anaandikia ubaoni, mwanafunzi hasiye na kazi anaandikia daftarini

  Mbona hivi? Kunguni au mbu hawajaenda japo shule na inawachukuwa robo sekunde kugundua mshipa wa damu, dokta mwenye madgree ya kugundua mishipa atachukuwa masaa kadhaaa huku akiomba wasaidizi wake waje!!

  Mbona hivi? Pilau ni wali husiohitaji mboga na mchuzi, kachumbari na mchuzi wake vimefikaje mezani?

  Mbona hivi? Mtu kajikwaa na kuanguka barabarani, yuko bize kuangalia nani amemuona wakati anaanguka, badala ya kuangalia wapi yawezekana kaumia!

  Mbona hivi? Hakuna kikaratasi cha onyo kutoka wizara ya ustawi wa jamii kwa wavaaji sketi na gauni kinachosema "vazi hili kamwe halitakustiri na halitaendana na maadili ya jamii pale mvaaji unapokaa chini na kutawanya miguu mbele ya kadamnasi"
   
 2. N

  Nesindiso Sir JF-Expert Member

  #2
  Nov 22, 2007
  Joined: Oct 31, 2007
  Messages: 374
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kali babaake!!
   
 3. YournameisMINE

  YournameisMINE JF-Expert Member

  #3
  Nov 22, 2007
  Joined: Aug 29, 2007
  Messages: 2,451
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 145
  Naona weekend ya Thanxgiving ipo mwendo mdundo/maneno semaga, maposo ponsoloto. Haya kaka, hayo ni mambo ya known knowns/known unknows/unknown knowns.........kaazi kweli kweli.!!!!
  Umenikumbusha mambo ya uswahilini, choo cha nje mlango gunia. Balaa ni ile siku yenye kiupepo cha taratibu kiasi kwamba gunia linakuwa linapeperushwa kishkaji bila mjisaidiaji kujua!!! inakuwa "mbona hivi" pale watu wanapoona mali za watu kwa bei ya dezo na hakuna atayethubutu kumstua muhusika juu yalojiri ili apate kubuni miondo mbinu mipya, ya kujisaidia kwenye choo cha mlango gunia!!!.
   
 4. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #4
  Nov 22, 2007
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mkuu MgonjwaUkimwi

  MgonjwaUkimwi unashitakiwa na jamii kwa ksababisha mbavu za wasomaji kuvunjika vunjika kwa maadishi yako ndani ya JF kitendo ulichokifanya siku na mahali pasipojulikana. Kuna wagonjwa kibao wako MOI na kuna hatari wakafanyiwa upasuaji wa vichwa badala ya mbavu. Hukumu nitatoa mara mgonjwa wa mwisho atakapopata nafuuuuu.

  Hongera Mkuu kwa ubunifu mzuri.
   
 5. M

  MgonjwaUkimwi JF-Expert Member

  #5
  Nov 23, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 1,288
  Likes Received: 521
  Trophy Points: 280
  Mbona hivi? 1+1 = 2, lakini 0+0 = 0. Pambafu! Taifa stars wakipoteza mechi ya ugenini na nyumbani, yaani 0+0, tutasema hawajapoteza mechi? Si watakuwa wamepoteza mechi mbili, yani 0+0 = 2?
   
 6. M

  MgonjwaUkimwi JF-Expert Member

  #6
  Nov 25, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 1,288
  Likes Received: 521
  Trophy Points: 280
  Mbona hivi?Ulaya mbwa akijisaidia bosi wake anaokota kinyesi, Africa bosi akijisaidia mbwa wake anaokota kinyesi
   
Loading...