Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,742
- 40,874
Neno la Leo: Kuna watu hawataki kuamini kabisa kati ya watu wawili ambao Watanzania walipewa wawachague kuwa viongozi wao kwa miaka mitano Magufuli alikuwa bora zaidi kuliko yule mwingine. Lakini ndugu zetu hawa hawataki kabisa kukubali ambao wao wenyewe waliutengeneza na kutaka wengine tuamini kuwa uchaguzi ule wa Oktoba 25 mwaka jana haukuwa wa kuchagua vyama; ulikuwa wa kuchagua mtu! Magufuli alisema "Serikali ya Magufuli" na wao wakasema "Lowassa = Mabadiliko" huku wakizungusha mikono. Hakukuwa na ajenda ya vyama; CCM walisimama nyuma ya Magufuli na CHADEMA nyuma ya Lowassa.
Huu ni ukweli. Matokeo ya Uchaguzi yaliyonesha kuwa hili ni kweli; Lowassa kama yeye alipata kura nyingi zaidi kuliko kura za chama chake kwa wabunge na madiwani (yaani kuna watu walimpigia kura yeye lakini hawakumpigia kura Mbunge wala diwani wake) na Magufuli naye alipata kura nyingi zaidi kama yeye huku watu wakimpigia kura diwani au mbunge wa chama cha upinzani. Unaweza kuita ni "political paradox" ya aina yake hii.
Jibu ni kuwa uchaguzi ule ulikuwa siyo nani Urais unamfaa zaidi bali nani anafaa zaidi kuwa Rais.
Ulikuwa uchaguzi rahisi sana kwa Watanzania wengine. Nashukuru kuwa upande ule wa wale walioamini ni nani anafaa zaidi. Na hadi sasa bado sijaona sababu ya kujutia msimamo wangu ule. Nitautetea.
MMM