CHUAKACHARA
JF-Expert Member
- Jun 3, 2011
- 12,388
- 6,482
Watanzania wenzangu wanatia kinyaa, wale wanaoshangilia upupu bila tafakuli ya kina.Yaani sijui watz wamelishwa unga gani. Ili uyaone mabadiliko ya sera za uchumi bora yaone kwanza mfukoni mwako na kisha kwenye familia yako. Huku kushangilia wanaotumbuliwa bila kujua kuwa wamepewa likizo ya kwenda kutumia na kutumbua walichochota ni uzuzu! Hebu badilikeni kwa kuona mnavyozugwa na wanasiasa.
Miezi 6 unataka mabadiliko, je ukifuga Ng'ombe, unahitajika muda gani kumkamua maziwa, hivyo mipango inafanywa kuwa mpole mkuu
Mfano mfu kweli, nimesema nenda hospitali hakuna huduma, hakuna dawa all is in shamble as usual, unashangilia nini? Ni kwa vile yule alikuwa nacho mimi sina sasa tumefananamfano mfu.
Nashukuru umenisoma. Watu tunakuwa wepesi wa kusahau! Nyerere alisema tufunge mikanda, nina uhakika yeye na wanaomzunguka hawakuwahi kukosa sabuni, dawa ya mswaki , nguo etc. Watanzania tukashangilia lakini walio na akili waliona kukosea kukubwa kwa Nyerere. Leo wanashangilia kila cha mtukufu anachokifanya hata kama kina dosari za wazi!Enzi za Nyerere kipindi waziri mkuu Sokoine
hali ilikuwa kama hivi
watu wanaruka ruka kwa furaha wakisikia walanguzi wamekamatwa
hawajiulizi why unga na sigara viwe adimu hadi kuwepo walanguzi....
na bado wapo watu wanakwambia hakuna kama Sokoine....
taifa zima tunajikunyata jioni kusikiliza Nyerere leo kaongea nini
umasikini ulipamba moto
enzi hizo msichana akivaa suruali mtaa mzima mnatoka kumtazama
Akaja Mwinyi akafungua milango..watu wakajua TV
wakajua fashion
wakajua kununua vyakula na kuweka ndani kwenye friji
still watu hao hao wanakwambia Sokoine alikuwa bonge la kiongozi
Mwinyi hawamtaji.....
Hii ya Magufuli kutumbua majipu itavuma kwa mda mrefu
hata asipokuwepo Magufuli watasema 'angekuwepo Magufuli' angewatumbua
hata kama utumbuaji wenyewe una walakini nyingi....lakini ndo hivyo...
ndo watanzania hao
Afadhali kwenu kuna mabadiliko hasi! HongeraHuku kijijini kwangu bei ya inga kg 10 inetoka 11,000 hadi 12,500
Huku kijijini kwangu bei ya inga kg 10 inetoka 11,000 hadi 12,500
Watanzania wengi wana roho mbaya na wanafiki, wanaangalia maisha ya wengine sio ya kwao, ndio maana mpaka sasa sehemu nyingi hawajaendelea kwa sababu hata ukienda likizo na suruali mpia unalogwa, ukijenga wanaloga,ukiwapa kazi hawafanyi bali wanataka pesa, hatutaki majizi na washikwe lakini waweke mifumo na sheria rafiki ili watu waweze kufanya biashara wanajua kuwa wao wenyewe ndio wameharibu kwa manufaa yao kwa nini kuwatesa watz ambao wanakesha usiku na mchana kutafuta pesa, weka sheri ya kodi iwe wazi ondoa makadirio ya kodi bali fuata inivoice au risiti ya manunuzi na ondoa kodi lukuki ambazo hazifai, hao masikini wanaoshangilia siku zinahesabika wataanza kuliaNimekuwa nikifuatilia mienendo ya watanzania kumshangilia Mh kila analolifanya. Strange maisha ndiyo yanazidi kuwa ya shida. Jana nimepita hospitali, rushwa ndio imepamba moto. Barabarani usiseme. Mnashangilia nini? Ni ile ya TUKOSE WOTE, NI WIVU wa sisi masikini; nimekuja kugundua na wala siyo kuwa masikini wanashangilia (masikini wanaoshangilia) kuwa tunaeleke kuzuri. Tatizo la sisi masikini tukiona tajiri kaporomoka, tunapata usingizi mzuri kama vile tumepata nafuu ya maisha. Wanashangilia Kabwe kaangushwa, of what direct benefit to you from today!
Wewe ulitaka miezi mingapi ndiyo tuhoji?Miezi 6 unataka mabadiliko, je ukifuga Ng'ombe, unahitajika muda gani kumkamua maziwa, hivyo mipango inafanywa kuwa mpole mkuu
Dah.. chief na wewe umetumbuliwa nini?Kilio kilio kilio kila kona twende wap jamani? Au tukimbilie Kenya yeuwiiiiiiiiie auwiiiiiiiiie yeuwiiiiiiiie jaman nife au nibaki?