Mbona foleni zimezidi?

Karibu mwezi sasa hali ya barabara haifai. Hapa nasikia Bagamoyo Road hakufai, Morogoro Road hakufai, Kilwa Road hakufai. Tatizo nini na tumeambiwa watu wamehamia Dodoma? Kuna watu hawafanyi kazi zao ipasavyo.
Tatizo Traffic ndio wanaoleta foleni Jiji hili.
 
Hata mimi nahisi hivyo
Kama wakiita magari fairly lazima mtatembea, unapoita magari upande mmoja kwa dakika 20 maana yake una-tripple congestion, kwenye junction zile barabara tatu kwa dakika ishirini zitaongeza congestion mpaka kwenye barabara ndogo.
 
Magari yanaongezeka, na hakuna uwiano na miundombinu iliyopo...

CBD bado ni ile ile tangu mkoloni, Kariakoo ni kulekule tangu mkoloni...

Kitu pekee tunachojiaminisha kitapunguza foleni ni kuweka overpass na kupanua barabara, lakini shughuli kuu bado zimeachwa kuwa posta au kkoo...

Kitu pekee kinaweza kikapunguza foleni ni kurudi katika master plan, kuwe na vitovu vya mji vingi...

Miji iliyoendelea huwezi ukakuta vitu vipo centrolized kama kwetu...yaani ukitaka nyanya uende Kariakoo na ukitaka simu pia uende Kariakoo...this should change...
Karibu mwezi sasa hali ya barabara haifai. Hapa nasikia Bagamoyo Road hakufai, Morogoro Road hakufai, Kilwa Road hakufai. Tatizo nini na tumeambiwa watu wamehamia Dodoma? Kuna watu hawafanyi kazi zao ipasavyo.
 
Tatizo kariakoo na posta ndio kila kitu, watu wengi wakiamka asubuhi wanaanzia mitaa hiyo, wengine hadi jioni so lazima foleni zotakuwepo tu.

Ujenzi wa mabarabara pia, huku Morogoro road ni kichefuchefu, mda wote ni foleni, sio asubuhi mchana wala jioni. Lakini kwa structure inayojengwa tunaamini suluhu itapatikana.
 
Ila mkuu ofisi nyingi zimepungua posts. Foleni sasa hivi iko nje ya mji. Mfano Bagamoyo road zote ukivuka selander bridge kule mbele kuingia mjini hakuna foleni. Kilwa road ukivuka gerezani katikati ya mji unapeta dakika 10 ushafika Kinondoni,Makumbusho. Morogoro road ukivuka Manzese au Magomeni mbele hakuna foleni? Why? Main junctions ndio tatizo
 
Mkuu kitambi siyo sifa ni ugonjwa unaokumaliza taratibu bila ya wewe kujua, hebu jitahidi kufanya chchote iwavyo ili ukiondoe hicho kitambi mkuu kabla hakijakugharimu. Ila siyo lazima kuufuata ushauri wangu.
Ntakuwa nakuja likizo huko najua kitapungua tu mkuu...
 
Fact.

Mwanza soon inakua grid locked kama Dar kwa sababu ofisi zote za umma ziko mjini na hawana mpango wa kuniondoa na kuzitawanya.

Pamoja na kukua kwa tehama bado ofisi zinarundikana sehemu moja utafikiri tuko miaka ya 60 ambapo ofisi zilikua zinahitajika kukaa jirani ili iwe rahisi kwa kuhamishiana nyaraka.

Angalia hata Dodoma, ujinga ni ule ule kuweka ofisi za serikali eneo moja, hatujifunzi, viongozi wetu kila siku wanatembelea ulaya hawajifunzi hata kidogo.

Hizi nchi zetu masikini ni masikini hadi akili za kupanga miji.
 
Miundombinu michache kuliko idadi ya watumiaji magari...

Ujenzi wa makazi usiofuata master plan
 
Huu utaratibu siku hizi haueleweki

Kilwa road kuanzia Mission utaratibu unajulikana so mimi natoka zangu Chamazi uku uwanja wa Azam saa 12 kamili pale mission nafika kama 12:45 navizia ikifika Moja kamili wanafungua njia kila baada ya dk 15 mpk Moja na nusu so tunavutwa sana mpk nafurahia ila cha moto kipo jumatatu na barabara ya kilwa kuanzia kongoe uko ndo balaa juzi saa nane nimekaa mpk kumi na moja kwa foleni gari zimenasa katikati ya barabara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…