Mbona Bunge Haliwakilishi Wananchi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbona Bunge Haliwakilishi Wananchi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gurudumu, Apr 8, 2011.

 1. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #1
  Apr 8, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu,

  Nilikuwa kimya muda mrefu lakini tangu Mswada huu wa kutunga sheria ya kutunga katiba mpya utoke nimekerwa na vitendo vya serikali na Bunge kiasi kwamba nimelazimika kujitokeza tena.

  Binafsi sioni sababu Bunge linaendelea na vikao vya Public hearing kuhusu mswada huu, hasa baada ya kongamano la UDASA lililofanyika Nkuruma hall wiki iliyopita. Wananchi wa vyama vyote na wasio na vyama waliongea kutoa maoni na uchambuzi wao. Asilimia 90 ya wachangiaji waliagiza serikali ikaandike upya huo mswada kwa sababu una mapungufu mengi mno kuweza kurekebishwa.

  Kongamano lile lilirushwa live na ITV na Radio One, na pia magazeti yaliandika kwa kina. Matumaini yangu ni kwamba serikali, ccm, na wananchi walifuatilia maoni yale na walipata kufahamu fika maudhui ya huo Mswada na mapungufu yake.

  Nilitarajia kwamba serikali na ccm wangekuwa na nia njema na kusitisha mchakato wa kutoa maoni mara moja na kuuandika upya. Huo Mswada mpya ambao umezingatia maoni yote yaliyotolewa pale Nkuruma ndio ambao sasa ungetumika kukusanya maoni ya wananchi kupitia Public Hearing. Badala yake sasa kinachoendelea ni Public Heating! Pia wanaendelea kutupotezea muda na kutumia vibaya pesa zetu eti wanakusanya maoni, as if watapata maoni tofauti sana na yale yaliyokwishatolewa pale Nkuruma.

  Potelea mbali kama walikengeuka na kudhani kwamba ya Nkuruma ilikuwa ni "uvunjivu wa amani" wa wasomi wanaochochea "chuki" dhidi ya serikali. Lakini yaliyotokea jana Dodoma na Dsm ni salamu nyingine kwa serikali na ccm. Unless kama nia yao ni kufanya marudio ya Januari tano 2011.

  Wanaoongea kuhusu mapungufu ya huu mswada ni wananchi. Wamejitokeza Nkuruma, Dodoma, DSM, Zanzibar, na pia kupitia kwenye radio, runinga, magazeti, blogu, simu, mijadala kwenye daladala, majumbani, maofisini, vijiweni, kilabu za pombe na michezo, n.k. Wote wanaupinga muundo na maudhi ya Mswada huu.

  Wabunge wanadai kwamba hao wanaopinga muundo na maudhui ya Mswada huu wanachochewa na Chadema. Kama ni kweli kwamba wanachochewa na Chadema, na kwamba zaidi ya asilimia 90 ya waliotoa maoni yao wanaupinga, basi ina maana kwamba wananchi wanaoupinga ni wengi kuliko wanaouunga mkono, na hivyo wananchi wengi ni wanachama wa Chadema kuliko ccm.

  Na kama Bunge ni chombo cha kuwakilisha wananchi, basi kuendelea kutafuta maoni kuhusu huo mswada kwa maudhui na muundo wake wa sasa hivi ni kutowakilisha wananchi, ni kiburi, jeuri, na dhuluma.

  Mtagundua kwamba nimeshindwa kutofautisha Bunge, serikali na ccm. Nimejitahidi kutafuta namna ya kutofautisha nikashindwa.

  Naomba mjadala kuhusu hili, tafadhalini sana.
   
 2. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #2
  Apr 8, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  :love:

  One thing brother you need to know about hawa wabunge wetu...they are real far away from the real touch..usingizi mnono wa pono utokanao na madaraka...they have nothing to loose

  Simply the best, they are far away from where we are
   
 3. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #3
  Apr 8, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na wewe kabisa, kwa sababu inastaajabisha mno kwamba wanamwakilisha nani
   
 4. muhosni

  muhosni JF-Expert Member

  #4
  Apr 8, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,114
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  CCM is probably hitting the last nail of their own coffin, nitafurahi kama wakiendelea hivi na hatimaye wakaupitisha huo mswada kwa jeuri
   
 5. M

  Mtu wa Mungu JF-Expert Member

  #5
  Apr 8, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 445
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  MwanaJF Gurudumu hongera kwa thread hii; ni kweli kwa sehemu, hasa wa kuangalia zaidi ni wale 19 batili wa sisiemu walioingilia mlango wa nyuma; wakiwemo vigogog wawili wa bunge hilo, pinda na makinda; hawa wameingia kwa kuchakachua hivyo ni hatari zaidi kwa uchakachuaji bungeni-rejea uongo (wa pinda na jinsi makinda alivyotumia nguvu ya kiti kumlinda mpaka leo) aliolipua mb. Lema wa cdm;
   
 6. mbogo31

  mbogo31 JF-Expert Member

  #6
  Apr 8, 2011
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 687
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Mkuu hapa tupo pamoja, Wabunge wengi isipokuwa wa Chadema hawawakilishi Wananchi, wapo kwa manufaa yao wenyewe. hawana uchungu na sisi hata kidogo lakini yaja siku nasi hatutawahurumia hata kidogo.
   
 7. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #7
  Apr 8, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  hapo kwenye red mkuu sijakupata vizuri
   
 8. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #8
  Apr 8, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Siku imeshawadia mkuu, huu mswada ni kama kipindupindu utawapuputisha wote
   
 9. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #9
  Apr 8, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hivi bunge hili ni makini kweli? ilikuwaje leo hii likahairisha shughuli zake hadi j3 mara tu baada ya kipindi cha maswali! ndiyo kusema alikuwa na shughuli ya kufanya?
   
 10. muhosni

  muhosni JF-Expert Member

  #10
  Apr 8, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,114
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Umeiona hiyo janja ya kula pesa zetu bila kazi yoyote eee? As if kwamba bunge zima lilikuwa linahusika na kukusanya maoni ya wananchi. Inawezekana hawakuwa na kazi yoyote katika ratiba ya bunge leo, ndiyo maana Makinda hakutangaza kama shughuli zilizokuwa zifanyike leo zitafanywa lini
   
 11. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #11
  Apr 8, 2011
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Ndugu zangu nadhani ni muhimu tusiwalaumu wabunge wote; wabunge wanaoushabikia muswada huu kama ulivyo karibuni wote ni wa ccm!! Hivyo basi kuliachia bunge hili lenye majority ya wabunge wa ccm hatima ya katiba ya nchi yetu ni kujinyonga mchana kweupe na kamba ya katani!!
   
 12. M

  Mtu wa Mungu JF-Expert Member

  #12
  Apr 8, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 445
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Katiba ya sasa haiwatambui wabunge 19 wa sisiemu kwa sababu hawakuchaguliwa na wapiga kura badala yake wanadai waliingia bungeni bila kupingwa wakati kila mTz anafahamu jinsi kila mmoja wao alivyohonga kuingia bungeni!!!!!!!!!!!!
   
Loading...