Ni bahati nzuri kuwa uchaguzi wetu hapa Tz umefanyika karibu kipindi sawa na ule wa nusu muhula (mid-term) wa marekani. Ni ukweli usiopingika kuwa umaarufu wa Barack Obama umeshuka na hivyo chama chake kupoteza viti vingi na nguvu ya utawala kwenye bunge nchini humo. Lakini Barack Obama hajakataa kushindwa kwa chama chake, ingawa imemuuma na ameona ni changamoto(He called the election a Democratic "shellacking" and lamented that "we lost track of the ways we connected with the folks who got us here in the first place." ) na kusema kuwa atatilia mkazo kukuza uchumi na ajira kipindi hiki kilichobaki. Aliendea kusema kuwa amethibitisha alichosikia toka kwa wapiga kura nchi nzima, watu wamefadhaishwa, (kama ni kiswahili sahihi)((Obama said Tuesday's results confirmed what he's heard from voters across the country: People are frustrated. He said the lesson of election was that he hasn't made enough progress in creating jobs). Jambo kuu hapa ni kuwa amekubali kushindwa kwa misingi ya kidemokrasia, ile iliyomuweka yeye madarakani kwa kishindo. Huu ni mfano mzuri toka kwa taifa lilioendelea ambalo tumekuwa tukienda kila siku kuomba misaada toka kwao. Swali ni Je, viongozi wetu wamefanya hili uchaguzi huu kutokana na matukio yanayotokana na matokeo ya kura yanayoendelea kutangazwa? Sidhani... Kwa nini hatuamini kuwa Rais anaweza asipendwe tena kama mwanzo? Kwa nini mawakala wa upinzani wanakuwa macho kulinda kura zao? Ni ishara kuwa waliopo madarakani hawataki kushindwa kwa haki! Kwa nini tusikubali kuwa wananchi walioelimika na wenye ufahamu wa ushindani wa demokrasia hawatukubali tena kama hapo awali? Tafakari, chukua hatua..
Huko kote ni kuheshimu mfumo mzima wa demokrasia. Kuanza kuchakachua kura na uwezo wa kufanya hivyo ni uthibitisho tosha kuwa viongozi waliopo madarakani ndio wanaotengeneza mfumo huo mbovu na kutuhadaa. Maana yangu ni kwamba kama kunaa mtu anafikiria Tanzania kuna haki na demokrasia, au mfumo tulionao utatuletea maendeleo afikirie zaidi ya mara moja. Na wale wanaoshabikia mfumo wetu nawafananisha na mbu aliyefikiri anapigiwa makofi kumbe anawindwa
nani alikuambia TZ kuna demokrasia, ni uongo wa CCm kusema kuna demokrasia utulivu na amani au TZ ni kisiwa cha amani, ukweli ni kwamba hata kwenye nchi 15 zenye demokrasia na utawal bora tz haipo, nafikiri una mfahamu Ibrahim MO, katika ranking ambazo kazitoa mwezi uliopita Tz haipo katika nchi 15 za afrika zenye demokrasia na utawala bora, kama unakumbuka Chisano alimbwaga mkapa kwa viongozi marais waadlifu kutoka afrika, leo tunadangannywa kuwa kuna demokrasia, in fact kuwa na demokrasia ni pamoja na kuwa na tume huru ya uchaguzi among other things:yield: