Mbona Barrack Obama anakubali kushindwa..?! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbona Barrack Obama anakubali kushindwa..?!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by mi_mdau, Nov 4, 2010.

 1. mi_mdau

  mi_mdau JF-Expert Member

  #1
  Nov 4, 2010
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 563
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Ni bahati nzuri kuwa uchaguzi wetu hapa Tz umefanyika karibu kipindi sawa na ule wa nusu muhula (mid-term) wa marekani. Ni ukweli usiopingika kuwa umaarufu wa Barack Obama umeshuka na hivyo chama chake kupoteza viti vingi na nguvu ya utawala kwenye bunge nchini humo. Lakini Barack Obama hajakataa kushindwa kwa chama chake, ingawa imemuuma na ameona ni changamoto(He called the election a Democratic "shellacking" and lamented that "we lost track of the ways we connected with the folks who got us here in the first place." ) na kusema kuwa atatilia mkazo kukuza uchumi na ajira kipindi hiki kilichobaki. Aliendea kusema kuwa amethibitisha alichosikia toka kwa wapiga kura nchi nzima, watu wamefadhaishwa, (kama ni kiswahili sahihi)((Obama said Tuesday's results confirmed what he's heard from voters across the country: People are frustrated. He said the lesson of election was that he hasn't made enough progress in creating jobs). Jambo kuu hapa ni kuwa amekubali kushindwa kwa misingi ya kidemokrasia, ile iliyomuweka yeye madarakani kwa kishindo. Huu ni mfano mzuri toka kwa taifa lilioendelea ambalo tumekuwa tukienda kila siku kuomba misaada toka kwao. Swali ni Je, viongozi wetu wamefanya hili uchaguzi huu kutokana na matukio yanayotokana na matokeo ya kura yanayoendelea kutangazwa? Sidhani... Kwa nini hatuamini kuwa Rais anaweza asipendwe tena kama mwanzo? Kwa nini mawakala wa upinzani wanakuwa macho kulinda kura zao? Ni ishara kuwa waliopo madarakani hawataki kushindwa kwa haki! Kwa nini tusikubali kuwa wananchi walioelimika na wenye ufahamu wa ushindani wa demokrasia hawatukubali tena kama hapo awali? Tafakari, chukua hatua..
   
 2. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #2
  Nov 4, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  Mkuu, mimi siku zote huwa natamani Tanzania pia tuwe na chaguzi kama Amerika ambako wapigara wanaheshimika sana.

  Tatizo hapa kwetu watu wanajua kuukwaa uongozi ni kuukwaa ulaji.

  Leo Makongolo Mahanga ni Mbunge wa kufinyanga huko Segerea, na kwa maneno yake alitamka amewekeza "pesa nyingi sana" asingependa kuona "zinapotea".

  Any way. I shut-up
   
 3. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #3
  Nov 4, 2010
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,547
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  hawa republican watakuwa wamechakachua matokeo,
   
 4. mi_mdau

  mi_mdau JF-Expert Member

  #4
  Nov 4, 2010
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 563
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Angesema au angehoji kama angehisi amechakachuliwa.
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  Nov 4, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Kule kura ya mtu inapewa due respect, ndiyo maana ya demokrasia!
   
 6. mi_mdau

  mi_mdau JF-Expert Member

  #6
  Nov 4, 2010
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 563
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Na kuchezea kura na matokeo yake inamaanisha kuchezea wananchi, na kuwaonyesha kuwa kura zao ni kama kuongeza chumvi baharini, kamwe hazitoleta tofauti
   
 7. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #7
  Nov 4, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Huwezi kulinganisha uchaguzi kule Marekani na uhuni unaofanywa hapa kwetu! Kule Marekani mwaka 2000 wizi wa kura ulilikumba jimbo la Florida lililompa Bush ushindi mduchu ambao ulipingwa na Al Gore wa Democrat.

  Kilichotokea? Kesi ikatinga mahakamani katika ngazi zote hadi Supreme Court ambapo iliamua kwa kura 5 kwa 4 kusitisha zoezi la kurudiwa kurudiwa kuhesabu kura na hivyo hatimaye kumpa ushindi Bush kwa kura 537 tu. Mchakato wa Mahakama ulichukuwa zaidi ya mwezi mmoja na nusu.

  hapa kwetu kuna uhuni na ubabe.: Hakuna kupinga matokeo ya urais lakini unaweza kupinga matokeo ya Ubunge. Hapo kwanza ni ukiukwaji wa Katiba katika kutafuta haki -- na wanasheria waliangalie hili kwa namna ya kulipeleka mahakamani.

  Pili hapa kuna haraka ya zima moto ya kumuapisha mshindi wa urais -- wakati wenzetu kwingine hakuna haraka hiyo -- na wao hufanya hivyo ili kutoa fursa kwa asiyeridhika kwenda mahakamani.

  Katika chaguzi, huwezi kulinganisha uhuni wa hapa na ustaarabu wa nchi zingine.
   
 8. b

  bulunga JF-Expert Member

  #8
  Nov 4, 2010
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 290
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  ni lazima Obama ayaseme hayo, kwanzu tume ya uchaguzi si ya serikali na yeye hawezi kutia pua yake huko(tume), lakini hapa Tz utamsikia Jk akiiipongeza tume yake aliyoichagua(what a shame)m ulimwenguni kote computer ni chombo cha kurahisisha kazi lakini kwa NEC TZ the opposite is true, imani kwa wannchi imepotea ndo maana watu wanaweza kulala nje wakilinda kura ama kweli peoples pwr :hippie:
   
 9. mi_mdau

  mi_mdau JF-Expert Member

  #9
  Nov 4, 2010
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 563
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Huko kote ni kuheshimu mfumo mzima wa demokrasia. Kuanza kuchakachua kura na uwezo wa kufanya hivyo ni uthibitisho tosha kuwa viongozi waliopo madarakani ndio wanaotengeneza mfumo huo mbovu na kutuhadaa. Maana yangu ni kwamba kama kuna mtu anafikiria Tanzania kuna haki na demokrasia, au mfumo tulionao utatuletea maendeleo afikirie zaidi ya mara moja. Na wale wanaoshabikia mfumo wetu nawafananisha na mbu aliyefikiri anapigiwa makofi kumbe anawindwa
   
 10. L

  Lorah JF-Expert Member

  #10
  Nov 4, 2010
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 1,193
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nyerere - Baba wa Taifa
  Mwinyi - Mzee Ruksa
  Mkapa uwazi na ukweli
  KIwete- Fisadi wa nchi na Fisadi wa kura... poor you sijui unajisikiaje unapotawala watu wanaojua wewe ni mwizi wa kutupaaa?? tulikupiga mawe.tukakuzomea, kwa sasa tutakushoot tu! miaka mitano na mganga wako yuko mbioni kuelekea ahera tutaona ......
  usitembelee huku kwetu .................
  tutakumaliza,
   
 11. b

  bulunga JF-Expert Member

  #11
  Nov 4, 2010
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 290
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  nani alikuambia TZ kuna demokrasia, ni uongo wa CCm kusema kuna demokrasia utulivu na amani au TZ ni kisiwa cha amani, ukweli ni kwamba hata kwenye nchi 15 zenye demokrasia na utawal bora tz haipo, nafikiri una mfahamu Ibrahim MO, katika ranking ambazo kazitoa mwezi uliopita Tz haipo katika nchi 15 za afrika zenye demokrasia na utawala bora, kama unakumbuka Chisano alimbwaga mkapa kwa viongozi marais waadlifu kutoka afrika, leo tunadangannywa kuwa kuna demokrasia, in fact kuwa na demokrasia ni pamoja na kuwa na tume huru ya uchaguzi among other things:yield:
   
 12. mi_mdau

  mi_mdau JF-Expert Member

  #12
  Nov 4, 2010
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 563
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Mkuu kama umenisoma hapo namaanisha Marekani ndiko kwenye demokrasia
   
 13. b

  bulunga JF-Expert Member

  #13
  Nov 4, 2010
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 290
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  najua kuonyesha tofauti na tulivyo, nakuunga mkono kimtindo, tuko pamoja
   
Loading...