Mbolea ya Super Gro

wayaboi

Member
Mar 23, 2023
37
53
Habari ndugu wakulima na wafugaji, kumekuwa na sintofahamu nyingi kuhusu super gro, nilikuwa naomba msaada wa mawazo wewe kama mkulima unaitambua kama mbolea? Na Kwa wale waliotumia mavuno yake yalikuwaje?
-Kuna machapisho mengi yanaonesha kuwa sio mbolea sasa Kwa waliothinitisha nahitaji mawazo yenu
 
MKUU ACHANA NA HUU UOZO WA SUPER GRO
Hivi karibuni kumekuwa na wimbi la watu wanaoshawishi matumizi ya super gro kama mbadala wa either mbolea za msingi au mbolea za majani (boosters). Wakulima wengi kwa kutokujua wamekuwa wakinunua kemikali hii kwa bei kubwa.Lita 5 wamekuwa wakiuziwa mpaka sh. 180,000/ wakiaminishwa na mawakala wa hii kemikali kwamba itawapa matokeo makubwa sana kwa sababu ni mbolea/kirutubisho Cha asili (organic fertilizer)
OKAY... super gro ni nn?..hebu tuanzie hapa kwanza..
Super gro ni kemikali ya kilimo (japo haijathibitishwa na mamlaka za kilimo nchini..TPRI,TFRA,TPHPA, Wala TBS) inayotengenezwa na kampuni ya GNLD Neo life international. Ndani ya super gro kuna kiambata kinachoitwa Ethoxylated Alkylphenol pamoja na Polysiloxane... viambata hivi vipo kwenye kundi linaloitwa kitaalamu Surfactant au wetter..hakuna kiinilishe chochote Cha msingi (NPK) kilicho ndani ya super gro (kwa mujibu wa mtengenezaji na sio maneno ya mawakala)
So kazi ya surfactant ni nn?
Okay . fikiria kwa mfano unapofua nguo zako..huwa unaweka nn Ili nguo zitakate kiurahisi?...yes huwa unaweka sabuni..sabuni huyafanya maji yapenye vizur na kwa urahisi kwenye nyuzi za nguo kwa kuvunja mshikamano wa asili wa maji (surface tension).. sabuni ni kemikali inayotengenezwa kwa surfactant..nadharia hii ilete kwenye mazao...inachokifanya super gro (surfactant) ni kuyafanya maji yenye viwatilifu au booster kupenya zaidi kwenye majani ya mmea wako hivo kuongeza ufanisi wa viwatilifu au booster kwenye mmea.
Surfactant sio hitaji la msingi la mmea Ili uweze kustawi...ni kisaidizi tu katika management ya mazao..ikipigwa peke yake Haina faida yyte...pia Kuna product nyingi sana kwenye maduka ya pembejeo zilizo katika kundi la surfactant na zinauzwa bei rahisi tu...(mfano. Aquawet 15SL kutoka kampuni ya Osho) nadhani inauzwa tsh 5000 kwa ml 200...so kama unaona Kuna haja ya kutumia surfactant kwenye mazao y'all tumia zilizopitishwa na mamlaka za kilimo
Super gro haijasajiliwa na mamlaka ya mbolea Tanzania TFRA Wala haitambuliki na mamlaka ya afya ya mimea na viwatilifu Tanzania (TPHPA)
 
Nashukuru sana kaka maelekezo yako yamejitoaheleeza mnoo
 
Back
Top Bottom