Mbolea ya Kinyesi cha Binadamu

Mbolea ya Kinyesi cha Binadamu

lukatony

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2011
Posts
701
Reaction score
604
Napenda kujua ni kwa nini kinyesi cha Binadamu hakitumiki kama mbolea?Maana sehemu nyingi ambazo uwa kuna mtitiriko wa kinyesi na kukawa na ulimaji Wa mboga mboga,uwa zinastawi sana.Sasa ni kwa nini kisitumike kama mbolea?
 
Kinaweza kutumika sema vingine ni hatari sana. Hapana chezea
 
Mbona vinatumika mkuu sema mbolea bado haijaanza kutengenezwa, mkusanyo wa maji taka
 
binadamu anabeba magonjwa mengi......hivyo kupitia kinyesi unaweza sambaza magonjwa!
 
Tafta kitabu kilichoandikwa! Toilet that make composite hapo utajua kama zinatumika tena sana tu
 
Kuna kipindi cha miaka ya elf2 na kitu. Maeneo flani jijini Dar iliwemo UKonga, wachina walikuwa wanapita kwenye nyumba za familia kisha wanakuomba eneo af wanakujengea choo bure, huwa ni cha mabati af hakiwi cha shimo, wanatumia matofali kwenda juu toka usawa wa ardhi(km kalo hv) af wanalisakafia juu na kuweka tundu moja tu la choo af mbele ya hlo shimo kunasehemu ya kukingia mkojo usichanganyikane na kinyesi(kuna mpira unapeleka mkojo nje kwenye dumu). Nyuma ya hilo kalo lililosakafiwa(tank la choo) kuna kimlango kwaajiri ya kutolea hicho kinyesi. Choo hicho hakiruhusu kitumia maja, huwa wanasupply magazeti ya kichina kwaajiri ya kujisafishi, halafu bembeni pia kuna kisehemu cha kutawadhia ambacho maji pia huenda kwenye dumu la mkojo. Kila baada ya miezi kadhaa walikuwa wanakuja kuzoa mbolea yao. Baadae sijui hyo project iliishia wapi lkn nilikuja kugundua Wachina walikuwa wanatumia kwenye ulimaji wao wa mboga mboga kwenye bonde la mto msimbazi. Mboga hizi walikuwa wanazipeleka kwenye mahoteli na Shoprites mjini.
 
Tafta kitabu kilichoandikwa! Toilet that make composite hapo utajua kama zinatumika tena sana tu

Niliwaona wachina wanazalisha nyanya na cabbage kubwa mara mbili ya zile tunazoziaona sokoni na wakasema wao wanatumia samadi yao wenyewe
 
Napenda kujua ni kwa nini kinyesi cha Binadamu hakitumiki kama mbolea?Maana sehemu nyingi ambazo uwa kuna mtitiriko wa kinyesi na kukawa na ulimaji Wa mboga mboga,uwa zinastawi sana.Sasa ni kwa nini kisitumike kama mbolea?
Itaunguza mimea, [emoji2] [emoji2] [emoji2]
 
Niliwaona wachina wanazalisha nyanya na cabbage kubwa mara mbili ya zile tunazoziaona sokoni na wakasema wao wanatumia samadi yao wenyewe
haswaa, chinesse zaidi ya miaka elfu moja walikua wanatumia kinyesi cha wanyama na binadamu, miaka ya 1952 inasemakana 75% kinyesi cha binadamu kilikua kinakusanywa majumbanj kwa ajili ya mbolea mashambani hasa kwenye mpunga, japo baadae miaka ya 1956 zaidi ya 90% ambapo inakadiliwa 300 million tons, inasemekana maeneo ya vijijini nguruwe pia walikua wanapewa kinyesi kama sehemu 😛 chakula chao. Study zinaonyesha zaidi kuwa mnamo mwaka huo huo 1956 jiji la Canton kuna idad kubwa ya watu walikua wanakusanya kinyesi kwa majumbani kwenye ndoo kwa ajili ya mbolea hii ilipelekea movement iliyojulikana kama collectivization movement ya 1956.

Inasadikika kuwa zaidi ya ya peasants 15, 000 community members walikua wanaingia mijini kila siku wakati wa usiku kukusanya kinyesi majumbani hii ilipelekea kusambaa kwa vinyesi vingi mtaani kutokana na vifaa vya kubebea kupasuka au kuvuja mpaka ikabidi taasisi maalumu zisajiliwe na watu wakawa wanauza kabisa kinyesi chao. japo kinyesi kilikua kinakua treated na kinaifadhiwa sehemu takribani mwezi na zaidi kwa ajili ya matumizi ua shamba baadae..
 
Nimeipenda sana hii Mkuu
 
waliosoma ShyBush nadhani kuelekea upande wa Bweni la Simba mwishoni kulikuwa na Mtanbo wa kuchoma maji taka ya kinyesi kwa kutumia Umeme then yanakorogwa na kuwa maji Safi kwa muonekano halafu tulikuwa tunamwagilia Bustani ukiyaona maji yale huwezi jua kuwa ni ya kinyesi cha Mwanadamu..............!!!!
 
Hahahaha wazo zuri, lakini ukifanyie treatment kwanza kwa kukiozesha kwa kukichimbia kwanzaa, bila hivyo bustani itakuwa inanuka kama mtu kajamba
 
mbona tunatumia sana tu! hizo mbogamboga hapa jijini mnazionaje
 
Nilipokua ndogo nilikula matunda aina Fulani sasa siku moja nikiwa shambani nikahisi haja, nikachimba shimo nikahifadhi mzigo, ule mzigo ulichanganyikana na zile mbegu za matunda. Baada ya mda Fulani zile mbegu ziliota zilikua nyingi kweli na zina afya ya kutosha. Nilicho fanya ni kuzitenganisha na kuziotesha karibu na miti maana Yale matunda yakisha kua yana tabia ya kutambaa na matawi ya miti.
 
Umepita pale umekula tikiti,mbele kidogo ukapiga mchuzi wa pweza na pweza wake. Home ukapiga ugali,dagaa,ngulu wa kukausha na juisi ya ukwaju.

Yani icho kinyesi kikifanywa mbolea itakuwa na rutuba ya kutosha...ila harufu yake mtafutana. Bora cha wanyama wengine tu.
 
Back
Top Bottom