WrestlerRSF254
JF-Expert Member
- Jan 30, 2023
- 1,199
- 2,003
Ndugu zangu GT nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya salamu niingie moja kwa moja kwenye mada.
Nisikitike kwamba Serikali yetu ya JMT chini ya Jemedari wetu mwana mama, Dr. Samia Suluhu Hassan anapambana usiku na mchana kuhakikisha mtoto wa kike anapata elimu, lakini bado wapo watu wachache ambao ni viongozi wasio wema wanazidi kumkwamisha.
Rushwa iliyokithiri miongoni mwa viongozi wachache walioaminiwa na Serikali yetu, imekuwa ni tatizo kwa mtoto wa kike kupata elimu ili atimize ndoto zake, ni jambo la kufehedhesha kwakweli, inatia huruma na inahuzunisha sana.
Mimba imekuwa ni tatizo sugu linalorudisha nyuma maendeleo ya mtoto wa kike, kwa kukatiza ndoto yao kabisa, na baadhi ya mimba hizi kwa watoto wa kike, wahusika wake ni walimu waliopewa dhamana ya kuwalea watoto hawa.
Katika shule ya sekondari ya Ikunguigazi yenye namba za usajili S4000, iliyo katika kijiji cha Kagera na kata ya Ikunguigazi, tarafa ya Ilolangulu, Wilaya ya Mbogwe, mkoa wa Geita.
Watoto wengi wa kike wamekuwa wahanga wa kupigwa mimba lakini hakuna msaada kwao, Mkuu wa shule ya sekondari ya Ikunguigazi, ndugu Abdillah Hassan Kayago, mtendaji wa kata ndugu Renatus na diwani wa kata ya Ikunguigazi ndugu Paulo Lutandula hawa ndio magwiji wa rushwa na kukandamiza haki kwa mtoto wa kike.
Hao viongozi waliotajwa hapo juu, wamezidi kwa kupokea rushwa na kuzuia sheria isichukue mkondo wake, haki ya mtoto wa kike katika kupata elimu inadidimizwa na viongozi hawa wasioaminifu katika kata ya Ikunguigazi.
Kidato cha nne waliohitimu mwaka jana karibia wanafunzi wanne wametoka na mimba shuleni, kidato cha pili wengi walishindwa kufanya mtihani wao wa FTNA kwa kupigwa mimba.
Mfano mzuri ni mwanafunzi, Naomi ameshindwa kufanya mtihani wake wa FTNA mwaka jana, kwa kupigwa mimba tena na Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Buzigozigo, Mwl John Mpare.
Badala ya kusimamia haki, kuhakikisha mwathiriwa anapata usaidizi ili ndoto yake ya kupata elimu isipotee, ndugu Abdillah Hassan Kayago ambaye ndiye Mkuu wa shule kwa sasa, mtendaji wa kata ndugu Renatus na diwani wa kata ya Ikunguigazi ndugu Paulo Lutandula, ndio wamezuia haki kupatikana kwa kutanguliza matumbo yao mbele kwa kuzuia sheria isichukue mkondo wake dhidi ya mtuhumiwa mwalimu John Mpare.
Tunaomba msaada (wananchi wa kata ya Ikunguigazi) wa taarifa hii kufikishwa kwa waziri wa Elimu Tanzania, ndugu Adolph Mkenda, waziri wa TAMISEMI, Mkoa wa Mkoa wa Geita, Afisa Elimu Mkoa wa Geita, Mkuu wa Wilaya Mbogwe, Mkurugenzi wa Wilaya ya Mbogwe na Afisa Elimu-Sekondari Wilaya ya Mbogwe kwa msaada na hatua zaidi.
Imekuwa ni desturi kwa viongozi hawa waliotajwa hapo juu, kuficha uhalifu unaofanyiwa watoto kike katika eneo lao, wamekuwa ni wanufaika wa rushwa badala ya kusaidia jamii yetu ya Ikunguigazi, kama kuna kiongozi yeyote humu aisaidie jamii ya Ikunguigazi kutuma malalamiko yetu haya ifike kunako stahili na sheria ichukue mkondo wake.
Tunapendekeza (wananchi wa kata ya Ikunguigazi) hawa viongozi waondelewe kwenye nyadhifa zao mara moja, ili kupisha uchunguzi utakao pelekea sheria kuchukua mkondo wake na haki kupatikana kwa wahanga wa unyanyasaji wa kujinsia, kimwili na kisaikolojia wanaopitia watoto wa kike waliopigwa mimba na viongozi hawa kula pesa na kufunika tu pasipo kuchukua hatua yoyote.
Jina la mwanafunzi Naomi Thomas Busagara likionesha hakufanya mtihani