Ukweli kuhusu sakata la Viongozi wa Ikunguigazi Wilaya ya Mbogwe Mkoani Geita

Mayombya Jr

Member
Oct 24, 2022
25
30
Habarini wadau wana jf, poleni sana na majukumu mazito ya ujenzi wa Taifa.

Kuna uzi humu jamvini inayohusu viongozi wa kata ya Ikunguigazi, Wilaya ya Mbogwe, Mkoani Geita.

Kusema ukweli mleta mada alikuwa sahihi kwa asilimia mia moja, kuna uozo na uchafu mwingi ndani ya ofisi ya mtendaji wa kata ya Ikunguigazi.

Wananchi wamelalamika sana hadi ilifika sehemu walimgomea (walimkataa) mtendaji wao, lakini kwa busara na hekima ya Mh. Diwani wa kata ile, ndio maana mtendaji yule yupo pale hadi leo, ila hawamtaki na huo ndio ukweli.

Naijua vizuri sana mazingira ya kata ya Ikunguigazi, Wilayani Mbogwe, kwa sababu nimewahi kuishi maeneo yale, mtendaji wa kata ni tatizo na hana maelewano mazuri na wananchi anao waongoza.

Serikali na viongozi wa halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe, Mkoani Geita, wafuatilie kwa makini sana malalamiko yale ya wananchi wa kata ya Ikunguigazi, kuna viongozi wasio wema kabisa kwenye ofisi hizi za umma.

Lakini pia hatua zichukuliwe, kama kiongozi hakubaliki kwa wananchi ni vyema ofisi ya Mkurugenzi mtendaji wa Wilaya, iweze pia kumweka pembeni kwa kumuhamishia sehemu nyingine na sio kusubiri hadi akataliwe na wananchi.
 
Mkuu kama unaweza kuweka mawasiliano yake humu ama PM fanya hivyo ili apate ujumbe kwa viongozi wa juu yake.
 
Back
Top Bottom