Mbivu na mbichi za TRL, ATCL kujulikana leo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbivu na mbichi za TRL, ATCL kujulikana leo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Jan 22, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jan 22, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,606
  Likes Received: 5,781
  Trophy Points: 280
  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu leo inakutana na Waziri wa Miundombinu, Profesa Shukuru Kawambwa, kupata taarifa za utendaji wa kampuni za Reli (TRL) na Ndege (ATCL).

  Kulingana na ratiba ya Kamati hiyo ambayo tangu ianze vikao chini ya uenyekiti wa Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango-Malecela, kikao na Waziri kitafanyika kabla ya majumuisho ya miswada na kukamilisha maoni ya Kamati.

  Kikao hicho kinafanyika Dar es Salaam ukiwa ni mfululizo wa vikao vya kamati za kudumu za Bunge, huku kukiwa na mkanganyiko kutokana na kauli mbili tofauti zilizotolewa wiki iliyopita juu ya uvunjaji wa mkataba kati ya Serikali na Kampuni ya Rites inayoendesha TRL.

  Wiki iliyopita, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Omari Chambo, aliiambia Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Hesabu za Serikali (PAC) kwamba mkataba huo utavunjwa mwezi ujao, baadaye Waziri Kawambwa akakaririwa na baadhi ya vyombo vya habari, akisema mchakato unaendelea na haijafahamika ni lini utavunjwa.

  Uendeshaji wa TRL inayotoa huduma katika Reli ya Kati, umegubikwa na migogoro ya mara kwa mara kati ya menejimenti na wafanyakazi.

  Alipokuwa akitoa taarifa kwa PAC, Chambo aliweka bayana kwamba migogoro inayoikabili kampuni hiyo inatokana na uongozi mbovu wa Rites ya India, yenye hisa 51 TRL.

  Vilevile utendaji wa kampuni hiyo umekuwa ukinyooshewa vidole na watu mbalimbali hususan watumiaji wa reli hiyo, kutokana na kushindwa kuboresha huduma. Mambo hayo yanatarajiwa kuhojiwa na wabunge ikiwamo hatma ya mkataba.

  Kuhusu ATCL, Kamati ya PAC iliambiwa kwamba wanaendelea kutafuta mbia atakayeiendesha.
   
 2. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #2
  Jan 28, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Sikufuatilia hii issue kwa ukaribu imefikia wapi? tuhabarishe hasa we uliyoitoa hii mada utakuwa na details zake.
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Jan 31, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,606
  Likes Received: 5,781
  Trophy Points: 280
  Song of lawino
  hawakuonekana nasikia wakadai watapeleka bungen
  pdd awa wameshachka achaana nao tuangalie tutasaidiaje walioathirika na mafuriko haiti/kilosa
   
Loading...