Mbio za Urais: DC aungana na Wasira

Mbio za Urais: DC aungana na Wasira

POST BELLE

Member
Joined
Feb 20, 2015
Posts
75
Reaction score
30
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Nyerembe Sabi, amempigia debe Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira, pale alipoeleza kuwa yeye siyo waziri na mbunge tu, bali ni mtarajiwa.

Alisema hayo katika mkutano wake na Watafiti wa Taasisi ya Maendeleo na Utafiti wa Mazao Uyole, uliofanyika mwishoni mwa juma.

Mkuu huyo wa wilaya alitoa kauli hiyo alipokuwa akimkaribisha Waziri Wasira kwenye hafla ya kufunga utafiti wa mbegu bora za viazi mvirigno, uliokuwa ukifanywa na taasisi ya Ari Uyole kwa udhamini wa Nchi ya Ufini (Finland)

Utafiti huo ulianza 2011 na ulimalizika mwishoni mwa juma na wakulima wataanza kutumia mbegu hizo bora katika msimu huu wa kilimo. Mbegu hizo zinatoa tani 18 kwa ekari badala ya tani tano au nane za awali.

"Mheshimiwa Waziri, mbunge ambaye pia ni mtarajiwa'' alisema mkuu huyo wa wilaya bila kumalizia ni mtarajiwa wa nini na kusababisha watu kuangua kicheko.

Ingawa mkuu huyo wa wilaya hakutaka kusema Wasira anatarajia nini, tayari mbunge huyo wa Bunda amewaambia baadhi ya wanaCCM kuwa anatarajia kugombea urais katika uchaguzi mkuu ujao.

Nia hiyo ya Wasira kuutaka urais, inathibitishwa pia na uamuzi wa CCM kumwadhibu kwa kuanza kampeni mapema, sambamba na makada wengine watano wa chama hicho, akiwamo Bernard Membe, Frederick Sumaye, Edward Lowassa, Januari Makamba na William Ngeleja.

Alipoulizwa na mwandishi kwa nini anaitwa mtarajiwa, Wasira alijibu kwa kifupi, " Kamuulize DC mwenyewe atakueleza".

Katika hotuba na mazungumzo yake kwenye hafla hiyo, Wasira hakugusia suala la uchaguzi ama urais bali alijikita zaidi kwenye umuhimu wa suala la utafiti wa mbegu bora kwa manufaa ya wakulima.

Pia Wasira aliwalaumu maofisa kilimo nchini, akisema wameshindwa kazi waliyotumwa na Serikali ya kwenda kubadili maisha ya wananchi wa vijijini kwa kuwaongoza katika kilimo chenye tija.

Chanzo:Mwananchi.
 
Mkuu wa wilaya ana akili sana wala hajampiagia kampeni Wassira kwasababu kuitwa mtarajiwa kuna maana nyingi kwa mfano mgombea mtarajiwa, mshindwa mtarajiwa, mstaafu mtarajiwa hivyo mkuu wa wilaya angeulizwa ni mtarajiwa yupi?
 
Kati ya ma dc wachapa kazi mnasa nyirembe ni mfano wa kuigwa pia anamwona wassira kama mkombozi wa watanzania hasa wale wanyonge wenye kuhitaji rehema za MUNGU kuletewa rais mzalendo kama wassira.
 
Kati ya ma dc wachapa
kazi mnasa nyirembe ni mfano wa kuigwa pia anamwona wassira kama
mkombozi wa watanzania hasa wale wanyonge wenye kuhitaji rehema za MUNGU
kuletewa rais mzalendo kama wassira.

Mh Dc amesoma nyakati mapema,,,,,,,,ni mjanja sana,kwan Mh Wasira ni mzee wa kimya kimya.
 
Mkuu wa Wilaya
ya Mbeya, Nyerembe Sabi, amempigia debe Waziri wa Kilimo, Chakula na
Ushirika, Stephen Wasira, pale alipoeleza kuwa yeye siyo waziri na
mbunge tu, bali ni mtarajiwa.

Alisema hayo katika mkutano wake na Watafiti wa Taasisi ya Maendeleo na
Utafiti wa Mazao Uyole, uliofanyika mwishoni mwa juma.

Mkuu huyo wa wilaya alitoa kauli hiyo alipokuwa akimkaribisha Waziri
Wasira kwenye hafla ya kufunga utafiti wa mbegu bora za viazi mvirigno,
uliokuwa ukifanywa na taasisi ya Ari Uyole kwa udhamini wa Nchi ya Ufini
(Finland)

Utafiti huo ulianza 2011 na ulimalizika mwishoni mwa juma na wakulima
wataanza kutumia mbegu hizo bora katika msimu huu wa kilimo. Mbegu hizo
zinatoa tani 18 kwa ekari badala ya tani tano au nane za awali.

“Mheshimiwa Waziri, mbunge ambaye pia ni mtarajiwa’’ alisema mkuu huyo
wa wilaya bila kumalizia ni mtarajiwa wa nini na kusababisha watu
kuangua kicheko.

Ingawa mkuu huyo wa wilaya hakutaka kusema Wasira anatarajia nini,
tayari mbunge huyo wa Bunda amewaambia baadhi ya wanaCCM kuwa anatarajia
kugombea urais katika uchaguzi mkuu ujao.

Nia hiyo ya Wasira kuutaka urais, inathibitishwa pia na uamuzi wa CCM
kumwadhibu kwa kuanza kampeni mapema, sambamba na makada wengine watano
wa chama hicho, akiwamo Bernard Membe, Frederick Sumaye, Edward Lowassa,
Januari Makamba na William Ngeleja.

Alipoulizwa na mwandishi kwa nini anaitwa mtarajiwa, Wasira alijibu kwa
kifupi, “ Kamuulize DC mwenyewe atakueleza”.

Katika hotuba na mazungumzo yake kwenye hafla hiyo, Wasira hakugusia
suala la uchaguzi ama urais bali alijikita zaidi kwenye umuhimu wa suala
la utafiti wa mbegu bora kwa manufaa ya wakulima.

Pia Wasira aliwalaumu maofisa kilimo nchini, akisema wameshindwa kazi
waliyotumwa na Serikali ya kwenda kubadili maisha ya wananchi wa
vijijini kwa kuwaongoza katika kilimo chenye tija.

Chanzo:Mwananchi.

Naomba ni msaidie huyo DC wa Mbeya,kuwa ni Mh Rais Mtarajiwa haina ubishi tunasubiri utashi wa kisiasa kum aprove hapo October.........
 
Mh Dc amesoma nyakati mapema,,,,,,,,ni mjanja sana,kwan Mh Wasira ni mzee wa kimya kimya.

Sio kimya kimya tu bali ni mtu mwenye uwezo, mchapa kazi, mzalendo na mwadilifu.Pia ni mtu mwenye kutii maagizo ya viongozi wake, kwa mfano tangu waambiwe wasifanye kampeni kabla ya wakati ni yeye tu ametii lile agizo wakati wengine wanaendelea na kampeni kwa staili tofauti tofauti.

Mimi binafsi namwona wassira as a best candident kati ya wote waliotangaza nia!
 
mkuu wa wilaya ya mbeya, nyerembe sabi, amempigia debe waziri wa kilimo, chakula na ushirika, stephen wasira, pale alipoeleza kuwa yeye siyo waziri na mbunge tu, bali ni mtarajiwa.

Alisema hayo katika mkutano wake na watafiti wa taasisi ya maendeleo na utafiti wa mazao uyole, uliofanyika mwishoni mwa juma.

Mkuu huyo wa wilaya alitoa kauli hiyo alipokuwa akimkaribisha waziri wasira kwenye hafla ya kufunga utafiti wa mbegu bora za viazi mvirigno, uliokuwa ukifanywa na taasisi ya ari uyole kwa udhamini wa nchi ya ufini (finland)

utafiti huo ulianza 2011 na ulimalizika mwishoni mwa juma na wakulima wataanza kutumia mbegu hizo bora katika msimu huu wa kilimo. Mbegu hizo zinatoa tani 18 kwa ekari badala ya tani tano au nane za awali.

"mheshimiwa waziri, mbunge ambaye pia ni mtarajiwa'' alisema mkuu huyo wa wilaya bila kumalizia ni mtarajiwa wa nini na kusababisha watu kuangua kicheko.

Ingawa mkuu huyo wa wilaya hakutaka kusema wasira anatarajia nini, tayari mbunge huyo wa bunda amewaambia baadhi ya wanaccm kuwa anatarajia kugombea urais katika uchaguzi mkuu ujao.

Nia hiyo ya wasira kuutaka urais, inathibitishwa pia na uamuzi wa ccm kumwadhibu kwa kuanza kampeni mapema, sambamba na makada wengine watano wa chama hicho, akiwamo bernard membe, frederick sumaye, edward lowassa, januari makamba na william ngeleja.

Alipoulizwa na mwandishi kwa nini anaitwa mtarajiwa, wasira alijibu kwa kifupi, " kamuulize dc mwenyewe atakueleza".

Katika hotuba na mazungumzo yake kwenye hafla hiyo, wasira hakugusia suala la uchaguzi ama urais bali alijikita zaidi kwenye umuhimu wa suala la utafiti wa mbegu bora kwa manufaa ya wakulima.

Pia wasira aliwalaumu maofisa kilimo nchini, akisema wameshindwa kazi waliyotumwa na serikali ya kwenda kubadili maisha ya wananchi wa vijijini kwa kuwaongoza katika kilimo chenye tija.

Chanzo:mwananchi.

anafaa kuwa rais mh. Wassira
 
kama watanzania wanataka rais basi mgombea anayefaa ni wassira.
 
images
RAIS Wasira
 
Back
Top Bottom