Mbio za mewnge wa Uhuru Hueneza UKIMWI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbio za mewnge wa Uhuru Hueneza UKIMWI

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kilasara, Jul 7, 2012.

 1. Kilasara

  Kilasara JF-Expert Member

  #1
  Jul 7, 2012
  Joined: Dec 21, 2008
  Messages: 578
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mwenge wa Uhuru mwaka mmoja ulilala katika uwanja wa mpira katika kijiji chetu. Kesho yake, katika uzio wa kiwanja ziliokotwa sio chini ya mia moja ya mipira ya kondom iliyotumika katika ngono za fujo usiku ule.

  Inasemekana kwamba katika mkondo wa njia unapopitia Mwenge wa Uhuru kila mwaka, kunakuwa na milipuko ya gonjwa hili, na vijana wengi huangamia miaka michache baadae.

  Kama madhumuni ya Mbio hizi za Mwenge wa Uhuru ni kuhamasisha wananchi kuchangia miradi ya maendeleo, ni maoni yangu kwamba tubuni mbinu m'badala isiyoambatana na ngono za fujo kwa vijana wetu. Kama madhumuni ni kutukumbusha historia ya Tanzania, basi tuandike kumbu kumbu zetu na tudhamirie kwa dhati kuzikumbuka kwa njia nyingine.

  Tukiendelea na staili hii ya kukusanya vijana wetu katika makundi yanayohimiza ngono zembe tutajiangimiza kama taifa.
   
 2. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #2
  Jul 7, 2012
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  This is true 100%. Nimewahi shuhudia with my naked eyes michesha ya mwenge inakuwa kama Ngoma za kizaramo maeneo ya pwani, msongola, mvuti, mwanambaya, mkuranga etc. Ni ngono usiku kucha
   
 3. m

  mhondo JF-Expert Member

  #3
  Jul 7, 2012
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 970
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Ni kweli kabisa vitendo vya ngono ukithiri sehemu ambazo mwenge ukesha.
   
 4. m

  mwinukai JF-Expert Member

  #4
  Jul 7, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 1,448
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  uPELEKWE TUU MAKUMBUSHO
   
 5. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #5
  Jul 7, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Kuna mwaka uliwai kesha maeneo fulani kule ILALA asbi ziliokotwa ndoo 2 za Kondom!
  Nyingiz zikiwa zimepasuka na zingine not used kbisaa.
  Tafakari na uchukue hatua
   
 6. mnyongeni

  mnyongeni Senior Member

  #6
  Jul 7, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 137
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Very true, juzi umelala kijiji cha miono(bagamoyo- chalinze), asubuhi yake, nikajipitisha tu UWANJANI, huku naongea na simu......... Daa, mabox/ kondomu ndo zimetapakaa, sasa sijui kwa wale wanaopenda kav kav, ilikuwaje.
   
 7. tatanyengo

  tatanyengo JF-Expert Member

  #7
  Jul 7, 2012
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 1,140
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Nashauri kwamba usiwepo mkesha wa mwenge. Mwisho wa muda kukimbiza mwenge iwe saa 12.00 za jioni halafu ukalale eneo ambalo hakutakuwa na mkesha wowote.
   
 8. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #8
  Jul 7, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,127
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Viongozi wa mbio za mwenge wa Enzi zile wameshatangulizwa na gonjwa hili...Ngono ilikua ni moja ya kauli mbiu iliyokuwepo kimya kimya. Ndio maana viongozi wa chama kijani ambao walikua youth league ni maarufu katika hii fani.
   
 9. Kaitampunu

  Kaitampunu JF-Expert Member

  #9
  Jul 7, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,682
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 145
  Sawa mbio ziwepo ila zianze asubuhi saa2 mwisho iwe saa 10jioni.
   
 10. Kaitampunu

  Kaitampunu JF-Expert Member

  #10
  Jul 7, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,682
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 145
  Hivi kwani lazima ukimbizwe nchi nzima kila mwaka? Nashauri ukimbizwe mkoa mmoja mmoja.
   
 11. Kilasara

  Kilasara JF-Expert Member

  #11
  Jul 7, 2012
  Joined: Dec 21, 2008
  Messages: 578
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hivi Mbio za Mwenge zinaandaliwa na Serikali au na Chama cha Mapinduzi? Nimeona maagizo ya wakuu wa vijiji wakikusanya fedha, eti kwa ajili ya miradi ya maendeleo, na kwamba hizo fedha zitakabidhiwa Mkuu wa Wilaya wakati Mwenge ukifika !!!!! Kwa hiyo J.K., Mukama, Msekwa na Pinda wanahusika!!!!

  Nashauri viongozi makini na wazalendo wa CHADEMA watangaze kuwa CDM ikichukua dola, watapiga marufuku Mbio za Mwenge, kwa vile vijana wengi wanaathirika na hili gonjwa linaloongezeka kutokana na hizi mbio.

  Najua kutahitajika hatua nyingine zaidi kushughulikia tatizo la Ukimwi. Lakini kwa sasa, kila jambo linaloongeza usambazaji wa Ukimwi lipingwe.
   
 12. Planner

  Planner JF-Expert Member

  #12
  Jul 7, 2012
  Joined: Apr 5, 2011
  Messages: 296
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  very very true! mi nshawah kuhudhuria mkesha nikiwa na NGo ya mambo ya HIV/AIDS tuliamua kushiriki huo mkesha ili tu-intervene hayo mambo..ila tulichoshuhudia ilikua ni balaa! ikiwa ni kushauri nadhani kama vp mbio ziwepo na kufungua miradi ila schedule iwe revised usiku mwenge ulindwe tu na mikesha isiwepo,hasa ukanda wa pwani ndo mikesha inakua balaa tupu!
   
 13. S

  Simbaarobaini7 Member

  #13
  Jul 7, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama madhumuni ya Mbio hizi za Mwenge wa Uhuru ni kuhamasisha wananchi kuchangia miradi ya maendeleo, ni maoni yangu kwamba tubuni mbinu m'badala isiyoambatana na ngono za fujo kwa vijana wetu. Kama madhumuni ni kutukumbusha historia ya Tanzania, basi tuandike kumbu kumbu zetu na tudhamirie kwa dhati kuzikumbuka kwa njia nyingine.

  Tukiendelea na staili hii ya kukusanya vijana wetu katika makundi yanayohimiza ngono zembe tutajiangimiza kama taifa.
  [/QUOTE]

  Kilasara you are really a great thinker for bringing this important issue. Umesema kweli kabisa kwani kule Tanga mwaka fulani mwenge ulilala mahala panaitwa Mwamboni ni mjini mjini na kesho yake uwanja wa Mwamboni wa shule ya Msingi kuliokotwa zaidi ya ndoo 4 za kondomu zilizotumika na zilizo hai. Ina maana hizi hai ziliachwa baada ya kutumia raundi ya kwanza libeneke lililofuata ni kavu kavu tu what do you think was next. Leo huko Mwamboni ndugu yangu kumechafuka nadhani unanielewa.Unakumbuka Marehemu Ditopile akiwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi alipiga marufuku kukesha kwa ajili ya Mwenge baada ya sekeseke hilo hilo la kuokota Kondomu ndoo kadhaa. Tufikirie njia mbadala aidha upokelewe mchana ulale uendelee tena kusherehekewa kesho yake mchana. Hata hivyo Kilasara Maana nzuri ya Mwenge alio-advocate Baba wa Taifa sio maana yake leo ni kama mwenge unapalilia ufisadi na wizi mtupu maana mamilioni yanachangwa na yanaliwa na wajanja na hata unapokimbizwa unamulika masikini na kuwaficha wezi watupu. Its time tuachane na mwenge tubuni kitu kingine kama Taifa cha kuweza kutuunganisha irrespective of our political ideologies. Bado mwenge unaonekana kukaa Ki-CCM zaidi maana hata unapopita sehemu nyingi unaona nguo za Chama cha Magamba ndio zimejaa.
   
Loading...