Mbio za Lowassa kuelekea 2010 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbio za Lowassa kuelekea 2010

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Halisi, Sep 13, 2009.

 1. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #1
  Sep 13, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Haya jamani, KUMEKUCHA, tunaambiwa Lowassa atamng'oa JK 2010 kwa kuwa tayari "Ametakasika" katika lile kashfa la Richmond. Tujadili kama Taifa.

  Hao wadadisi wa mambo wa Tanzania Daima Jumapili, ni wakali wa kupima upepo na wanaona mbali, na huyo Mbunge aliye mstari wa mbele kupambana na ufisadi anayemuunga mkono Lowassa kuwa Rais labda ni kivuli cha "Dk. Mwakyembe".

  Lowassa tishio CCM

  • Nguvu ya kundi lake yatawala ndani ya NEC


  na Mwandishi wa Tanzania Daima

  KUNA kila dalili kwa aliyekuwa Waziri Mkuu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa, kupitishwa na vikao vya juu vya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa mgombea urais wa chama hicho katika Uchaguzi Mkuu ujao, mwaka 2010.

  Taarifa za kuaminika kutoka kwa vigogo kadhaa ndani ya CCM na kwa baadhi ya wabunge wa chama hicho kikongwe nchini, zimethibitisha nia ya Lowassa kuwania kiti hicho, huku kukiwa na uwezekano mkubwa wa kupitishwa na vikao vya juu kuwa mgombea pekee badala ya Rais Jakaya Kikwete, anayetarajiwa kuomba tena nafasi hiyo ili kumalizia kipindi kingine cha miaka mitano cha kuliongoza taifa.

  Taarifa hizo zimefafanua kuwa nafasi ya Kikwete kupitishwa na CCM kuwa mgombea urais haitabiriki iwapo Lowassa ataamua kuwania nafasi hiyo ambayo pia humpa nafasi kiongozi kuwa mwenyekiti wa chama.

  Ikiwa imesalia miezi 13 kabla ya kufanyika kwa uchaguzi huo, tayari Lowassa anaonekana kuwa na nguvu kubwa ndani ya chama, huku akiungwa mkono na wajumbe wengi wa vikao vya juu, hususan wale wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho (NEC).

  Siku moja tu baada ya Rais Kikwete, kuzungumza na wananchi kwa staili mpya ya kujibu maswali ya papo kwa papo, Tanzania Daima Jumapili, ilizungumza na mbunge mmoja maarufu wa CCM, juu ya mustakabali wa chama hicho kuelekea Uchaguzi Mkuu 2010, kwa sharti la kutotajwa jina lake.

  “Kwa NEC hii niliyoiona kwenye kikao kilichopita, Lowassa anaweza kabisa kupitishwa kuwa mgombea urais wa CCM 2010 badala ya Bwana Mkubwa (Kikwete). Maana kwanza urais anautaka na jinsi nilivyoiona hii NEC, wajumbe wengi tayari wamesha declare interests kwa Lowassa …wengi wanamuunga mkono na ndiyo maana tumekuwa na vita kali ya makundi ndani ya chama.


  “Kwa kweli Bwana Mkubwa sijui hali itakuwaje, nafasi ya kupitishwa kwake eti kwa sababu ni rais anayemaliza muda wake itakuwa ngumu sana, niseme tu kwamba haitabiriki,” alisema mbunge huyo aliyejizolea umaarufu kwa kupambana na ufisadi.

  Nguvu ya Lowassa ndani ya NEC ndiyo inayodaiwa nusura imwangushe Spika wa Bunge, Samuel Sitta, baada ya wajumbe wengi kudai kwamba anaihujumu serikali bungeni, hivyo kupendekeza avuliwe uanachama, hali inayotafsiriwa kuwa walikusudia kulipiza kisasi dhidi ya hatua ya spika huyo kuunda Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza sakata la Richmond na ripoti yake kusababisha Lowassa kujiuzulu.

  Kwa upande mwingine, baadhi ya vigogo kadhaa wa CCM wamekanusha kauli ya Rais Kikwete aliyoitoa wiki hii kwamba kuna uadui miongoni mwa wabunge na baina ya wabunge na mawaziri, na kufafanua kuwa uadui uliopo ni baina ya baadhi ya wabunge na chama chao.

  “Alichosema rais kwamba wabunge wana uadui hata wanafikia hatua ya kuogopana, kwamba wanaweza kuwekeana sumu, kwa kweli si sahihi, uadui uliopo si kati ya wabunge na wabunge, bali ni kati ya baadhi ya wabunge na chama chenyewe. Kwani waliotaka kumsulubu Sitta kwenye NEC ni wabunge wenzake? Si wabunge wenzake, walikuwa ni wajumbe tu wa kikao kile cha chama, ambao wengi wako upande wa Lowassa. Wao bado wana kisasi na lile suala la Richmond na wako wengi kweli,” alisema kigogo huyo wa CCM.

  Lowassa ambaye inaaminika kuwa ni rafiki wa siku nyingi wa Rais Kikwete, alijiuzulu uwaziri mkuu Februari 2007, kutokana na kuhusishwa na kashfa ya kutoa zabuni ya kufua umeme wa dharura kwa kampuni ‘hewa’ ya Richmod Development Company LLC.

  Baadhi ya watu walio karibu na watu hao wanadai tangu kujiuzulu kwake, amekuwa katika kundi tofauti na Kikwete, huku akiwa na nguvu kubwa ya kichama inayodaiwa kuzidisha uhasama wa kimakundi ndani ya chama hicho.


  Mbali ya nguvu hiyo ya kichama, wadadisi wa mambo waliozungumza na gazeti hili, walisema uwezekano wa Lowassa kuwania nafasi hiyo ya juu kabisa serikalini unatokana na ukweli kuwa mwenendo wa hivi karibuni wa utekelezaji wa maazimio ya Bunge kuhusu sakata la Richmond umeonekana kumsafisha mwanasiasa huyo kuwa hakuhusika kabisa katika sakata hilo, kwani tayari serikali yenyewe imeshatangaza kutowachukulia hatua baadhi ya watendaji waliokuwa chini yake kwa sababu ya kile kilichoelezewa kuwa hawakuhusika katika sakata hilo.

  Katika mkutano wa 16 wa Bunge, serikali ilitangaza kuwa haijawachukulia hatua baadhi ya watumishi wake kadhaa ilioagizwa na Bunge, kwa sababu ya kutobainika kuhusika na mazingira ya rushwa na kuwafanya waipe ushindi wa zabuni ya kuzalisha umeme Kampuni ya Richmond.

  Miongoni mwa watumishi ambao kamati teule ya Bunge iliyokuwa chini ya Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe, ilipendekeza wachukuliwe hatua za kinidhamu na kisheria lakini hawakuchukuliwa hatua kama ilivyopendekezwa na Bunge ni Mwanasheria Mkuu, Johnson Mwanyika, huku Mkurugenzi wa Tume ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Edward Hosea, akichukuliwa hatua ndogo ya kuonywa.


  “Lowassa anaweza kabisa kugombea urais, kwa sababu tayari jina lakelimeshatakata, maana serikali yenyewe imeshasema kwamba kina Mwanyika hawakuwa na makosa yoyote katika suala la Richmond. Sasa kama Mwanyika hakuwa na kosa basi ni dhahiri kuwa kwa mtazamo wa watu Lowassa alionewa tu, kwa hiyo anaweza kabisa kufufuka kisiasa na kugombea urais,” alisema.

  Wakati hali ikiendelea hivyo, hatima ya vita hiyo ya makundi sasa inaonekana kumtegemea Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, ambaye ndiye Mwenyekiti wa kamati maalumu iliyoundwa na Kikwete ili kufanya kile kinachoelezewa na baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa kama utafiti wa kutafuta suluhu ya kuinusuru CCM kutoka kwenye vita hiyo.

  Wakati kamati hiyo ina wajumbe wengine kama Abdulhaman Kinana na Pius Msekwa, ni Mwinyi pekee anayeonekana kuungwa mkono na wana CCM wa makundi yote, hivyo kuwa tegemeo pekee katika kutafuta suluhu, kwani wajumbe wenzake bado wanaonekana kuwa ni sehemu ya watu wanaochochea vita hiyo ya makundi.

  Chanzo: Tanzania Daima la Jumapili 13, 2009
   
 2. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #2
  Sep 13, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
 3. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #3
  Sep 13, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
 4. A

  AmaniGK JF-Expert Member

  #4
  Sep 13, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,101
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
 5. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #5
  Sep 13, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  kwani kuna ubaya gani kama mwana CCM na ana sifa akaamua kugombea huko CCM..Idont see if this is an issue here,mwache agombee tu by the way hata JK akipigwa chini 2010 si ajabu maana he fails to prove ngonjera zake za kasi mpya,ari mpya na nguvu mpya.....he better go
   
 6. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #6
  Sep 13, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Nadhani Kibanda hayuko Dar kwa sasa. Lakini Mwananchi wamekuja na Story ya muendelezo wa "Live ya JK" kwa kuhoji " Kikwete awatosa maswaiba wake Rostam, Lowassa?" sasa sina hakika kwanini wameandika facts wakatumia alama ya kuuliza.

  http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=14578
   
 7. M

  Mkulima JF-Expert Member

  #7
  Sep 13, 2009
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 698
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  Halisi,

  Hivi kweli hata wewe unaamini hii habari inaweza kuwa na ukweli?

  Angalia kamati kuu ya CCM ilivyo halafu niambie kuna mwana CCM tena Lowassa eti atampinga JK, je hilo jina litapitia wapi?

  Ninachokiona hapa kuna kundi linajaribu kwa nguvu zote kutengeneza mgogoro kati ya JK na Lowassa.

  Magazeti yetu yanatumiwa vibaya mno na baadhi ya watu.

  Mimi naamini hii habari sio ya kweli na imeandikwa na upande unaompinga Lowassa kwa nia ya kujaribu kumtafutia mgogoro na rafiki yake.

  Lowassa hawezi kuwa rais tena Tanzania. Ninachokiona ni kwamba atarudi serikalini baada ya uchaguzi wa 2010.
   
 8. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #8
  Sep 13, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Kwamba naiamini ama siiamini hii habari, ni mjadala mrefu na mpana maana sijui chanzo chake halisi cha aliyeiandika. Jambo la msingi ambalo ninaweza kuwa nakubaliana nalo ni kwamba EL anautaka URAIS, ni lini na kwa njia gani hilo nalo sijui.

  Kwamba Lowassa hawezi kuwa Rais wa Tanzania, nalo siwezi kupingana na wewe ama kukubaliana nawe moja kwa moja maana nao ni mjadala mrefu sana kwa mazingira yetu ya sasa. Kuna vigezo vingi vya kuangaliwa na vyote vinaweza kuwa vya kufikirika maana lolote linaweza kutokea.

  Kuhusu habari hii kuandaliwa na wanaompinga Lowassa, hilo naweza kupinga japo si kwa asilimia 100. Nina sababu nzito ambazo baadhi ya wahusika watakubaliana na mimi, na zaidi waandishi wa habari wenye kujua vyumba vya habari vya Tanzania vinavyoendeshwa ikiwamo Tanzania Daima Jumapili. Ni mjadala mrefu na mpana tupeane nafasi tusiubane.
   
 9. K

  Kifuna JF-Expert Member

  #9
  Sep 13, 2009
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 426
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Huyu E.L kasafishika lini? hakuambiwa ajiuzuru,alichoambiwa ni kupima uzito wa maneno na kuchukua maamuzi na kwa kuwa alijiona ni mchafu alivyopima akaona anaangukia kwemye uchafu. ndipo akaachia ngazi!! sasa lini uchafu ule alioupima umesafishika? Ushauri wa bure atulie hadi uchungu wa mgao wa umeme uishe!!au labda mpaka kizazi hiki kipite! kama yeye atakuwepo ndipo agombee
   
 10. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #10
  Sep 13, 2009
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280
  lowassa is far much better than muungwana na ndio ambayo kidogo alifanya serikali ya JK ....mwaka wa kwanza wafikie mafanikio ambayo yamesimama ghafla especially mafanikio ya shule za kata kila kijiji ...ambayo hadi leo jk anayaimba ..its was lowassa"s baby...hilo halina ubishi...,na ukiondoa kasoro za lowassa ..basi lowassa is better kuliko jk hivi alivyo ....kwani kama utasema labda jk sio fisadi sana ..lakini lazima tujuwe sluggishness yake inaligharimu taifa kiasi gani....

  Kuhusu kugombea kwa lowassa sioni kama ni issue kubwa kwani chama kitaamua ..yeye hajatamka tofauti na mtu kama JOHN MAGALE SHIBUDA ambaye yeye kashatamka rasmi interest yake.....
   
 11. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #11
  Sep 13, 2009
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280
  kwa uchunguzi wangu lowassa halmashauri kuu anaweza kupita ....lakini mjuwe kuwa jina lolote huanzia kamati kuu ndio liende halmashauri kuu [kamati kuu kikwete yupo very strategic ,ameikamata kwa namna na mgawanyiko anaoujuwa mwenyewe kwa asilimia 70%...labda lowassa apigane kufa na kupona jina livuke hapo]

  iwapo jina la lowassa litavuka kamati kuu,atapita halmashauri kuu ....na mkutano mkuu hali haitabiriki kabisa......lolote linaweza kutokea, nionavyo kama lowassa atagombea lile la malecela litajirudia [kumbukeni nguvu aliyonayo malecela chamani],....itabidi lowassa achinjiwe baharini haraka na asifike halmashauri kuu...hiyo ndiyo pona ya kikwete!
   
 12. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #12
  Sep 13, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Maneno yako ni mazito sana na yana uzito unaostahili na pengine yanasaidia kwa kiwango kikubwa kutoa ufafanuzi wa habari husika. Huu ndio ubora wa JF.

  Sehemu kubwa ya maneno yako ni yale yanayozungumzwa na wafuasi wa Lowassa ambao wanaamini kwamba Lowassa ana uwezo mkubwa wa kuongoza. Imani hiyo wamewaambukiza hata akina JK na wenzake ambao wanaamini mafanikio yote ya Elimu ni ya EL. Hebu turejee matamko na maandiko kabla ya utawala wa JK kuingia madarakani kuhusiana na elimu tukichukua mfano mdogo tu wa sekta hiyo utabaini kwamba haukuwa uamuzi wake binafsi kama Lowassa japo kwa sasa kukwama kunaweza kuwa na mkono wake. Kwa ufupi EL hata uteuzi wa watendaji karibu wote akishirikishwa na JK huwapigia simu yeye binafsi na kuwaambia kwamba yeye ndiye amewapendekeza na hilo limemfanya aonekane kila kitu amefanya yeye kuanzia uteuzi hadi utendaji kazi na utekelezaji wa mipango ya serikali na sasa udhaifu na matatizo ya serikali ya kimfumo yanaenezwa kwamba ni kwa sababu ya kutokuwapo kwake serikalini. Huu ni udhaifu mkubwa sana maana hata Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alipoondoka serikalini wapo walioamini kwamba nchi haitatawalika bila yeye. pamoja na matatizo mengi makubwa nchi inatawalika. Tupunguze mapenzi ya kupepewa na upepo unaotengenezwa kwa makusudi na wataalamu kama Lowassa ambaye alifanikiwa sana kutufanya sote tuone JK ni chaguo la Mungu na sasa atatufanya tumuone kama takataka na yeye shujaa.
   
 13. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #13
  Sep 13, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Halisi,

  Nilisema awali kabisa kuwa kosa pekee tunaloweza kumkamata nalo Lowassa ni Uzembe kutokana na hii Richmond, na zaidi tukitaka sana ni kutumia madaraka na kukiuka kanuni za kazi, jinsi Yona, Mramba na Mgonja walivyofanyiwa.

  Lakini tofauti ni kuwa Lowassa, hawawajibishwa kwa uzembe wake wala kulitia Taifa hasara. Alichokifanya kwa kujiuzulu, kimechukuliwa kama adhabu tosha.

  Sasa kwa sisi wengine ambao hupima mambo kwa undani, je haya yote ni changa la macho na tangu awali ilikuwa ni makubaliano yao hawa wawili kuwa Kikwete atawale kwa kipindi kimoja kisha amwachie Lowassa au imelazimika kukatisha safari ya Kikwete kwenda kipindi cha pili kutokana na kinachotokea sasa hivi nchini?

  Kwenye thread yangu ya mgongano wa Katiba https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/38265-mgongano-wa-katiba-na-majukumu-katiba-ya-tanzania-na-katiba-ya-ccm.html nimeuliza ikiwa CCM leo wataridhia kuwa Kikwete hawafai, wanaweza kumvua Uanachama na Uongozi kiurahisi na kuondokana na mfumo wa kiserikali ambao ungeshurtisha Bunge na Mahakama kuu zihusike.

  Ni kutokana na udhaifu huu wa kuhakikisha kuna uwajibikaji na Kikwete kukosa Sauti na Mamlaka ndani ya chama, leo hii kina Sitta na Mwakyembe wanatapatapa na kupiga kelele za kuhujumiwa kutokana na haya ya kuonyesha kuwa Lowassa kajipanga vyema na yuko tayari kukichukua Chama mikononi mwake.

  Mimi sisikitiki kwa linalotokea CCM, wacha litokee ili tuone sura za kweli za wale wanaodai wao ni Wanamapinduzi na wale wanaotuhumiwa kuwa ni Mafisadi.

  CCM kumekuwa na upuuzi na ujinga tangu mchakato wa urais 1995. Na mbaya zaidi ni alichokifanya Mkapa 2005 kwa kufunika Demokrasia kwa ajili ya kutoa upendeleo na kulindana.

  Kama Lowassa ataendelea na moto wake wa kutaka Urais ndani ya CCM, sitarajii kusikia Kikwete akisema ataendelea na kipindi cha pili.

  Tetesi za kusema kuwa yeye ataondoka baada ya kipindi kimoja zitatimia hata kama sababu nyingine zinavumishwa ni kuhusu hali yake kiafya.

  Swali ni jee, Wapiganaji wanajiandaa vipi kujibu hili? na nani kati yao yupo tayari kugombea kumpinga Kikwete hata kama Lowassa hatachukua fomu?
   
 14. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #14
  Sep 13, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  [​IMG]
   
 15. MawazoMatatu

  MawazoMatatu JF-Expert Member

  #15
  Sep 13, 2009
  Joined: Sep 6, 2008
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Haya mambo yoote tunadhaania tu (Speculate) hakuna mtiririko wa matukio a,b,c.... ambao mwishoe tunaweza kutoa hitimisho kua Kikwete atakua rais wa muongo mmoja, au Lowasa atagombea 2010! Muamuzi wa yote ni muda tu!
   
 16. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #16
  Sep 13, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Nakumbuka Mtabiri maarufu sana Tanzania Shekhe Yahaya aliwahi kusema kuwa Lowassa atarudi katika Ulingo wake wa Kisiasa hata kushika madaraka katika Serikali tena, Labda ndio yanakaribia kufikia, Lakini kuna ushaidi wa kutosha katika hili
   
 17. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #17
  Sep 13, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  hakuna jipya mbona.. everything is according to the script...
   
 18. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #18
  Sep 13, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Je mtu anaweza kutabiri kilicho dhahiri? (can one predict the obvious?)
   
 19. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #19
  Sep 13, 2009
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Kama Lowasa akitokea kuwa Rais wa Taifa langu, nitatumia sehemu kubwa ya maisha yangu yaliyobaki kupiga vita vyama vyote vya upinzani Tanzania hadi vitoweke kwani ndivyo vitakuwa vimemweka madarakani.
   
 20. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #20
  Sep 14, 2009
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Hapa alinukuliwa akisema hajatangaza jambo hilo lakini hakukanusha au kukubali nia yake ya kugombea uraisi 2010.

  Lowassa avunja ukimya urais 2010

  Na Ramadhan Semtawa
  9/14/2009


  MBUNGE wa Monduli, Edward Lowassa amesema hajafikiria wala kutangaza kokote kuwa ana mpango wa kugombea urais katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2010, licha ya kuwepo taarifa kuwa anaweza kujitosa kwenye kinyang'anyiro hicho kuvaana na Rais Jakaya Kikwete.

  Lowassa, ambaye alilazimika kujiuzulu nafasi ya uwaziri mkuu baada ya kutajwa kwenye kashfa ya utoaji zabuni ya ufuaji umeme wa dharura kwa Richmond Development (LDC), ameshawahi kuwania nafasi hiyo ya juu ya kuongoza nchi mwaka 1995 wakati Benjamin Mkapa alipoibuka kidedea kwenye chama hicho tawala na baadaye kushinda urais.

  Mwaka 2005, Lowassa hakuingia kwenye mbio za urais ndani ya CCM kutokana na kile kilichoonekana kuwa ni kumwachia Kikwete, lakini tangu aachiwe uwaziri mkuu amekuwa akichukuliwa kama mtu ambaye anaweza kupambana na rafiki huyo mkubwa kuwania kugombea urais mwaka 2010 kwa tiketi ya CCM.

  Hata hivyo, Lowassa, ambaye ameshashika nafasi mbalimbali kwenye serikali za awamu ya pili, tatu na ya nne, alisema hajafikiria wala kumwambia mtu yeyote kwamba ana mpango huo ambao unaweza kusababisha mvutano mkubwa kwenye chama hicho tawala.

  Akionekana mchangamfu, waziri huyo mkuu wa zamani alijibu maswali ya Mwananchi bila ya kusita, lakini akiweka tahadhari.

  "Sijafikiria wala kutangaza popote jambo hilo unalouliza (la kugombea urais). Niacheni jamani nipumzike," alisema Lowassa alipoulizwa kuhusu habari zinazozidi kusambaa kuwa atapambana na rafiki yake Kikwete mwaka 2010.


  SOURCE:
  Mwananchi
   
Loading...