Jamani nisaidieni ushuri Kwa hili kuna mrembo nilikutana nae kitaa fulani akanivutia Mara moja ikanilazimu kutumia mbinu ili apate kuniziea.
Nikafanikiwa Kwa hatua fulani baada ya kukubali tubadilishane namba za simu, baada ya hapo tuliachana lakini ikawa tunachat sana na wakati mwingine ananipigia cm tukawa tumejenga ukatibu sana katka mawasiliano. Ikafika kipindi fulan nikawa safarini ila kwakweli alikwa haishi muda anapiga cm kama si kunsms. Nikatoa yangu ya moyoni ukweli alinipokea vyema Kwa kuniambia hata yeye amekuwa akifikiri kuwa ataniambiaje maana amenipenda sana nikamwambia sawa ikawa sasa ni kunitaka Mimi nirudi jijini DSM maana anahamu na Mimi nikamfariji kuwa mda si mrefu nitarudi kweli siku si nyingi nikawa narudi jijini nikamwambia kuwa ajipange maana nakuja akasema yupo full. Nilivyofika nikamwambia nishafika sasa apange muda tukutane akaniambia nisiwe na hofu nipange Mimi nikamwambia siwezi kumpangia maana yupo Kwa wazazi mtoto akanisomea ratiba yote ya kwao akaniambia niwe huru nikamkubalia.
Nikapanga kweli mrembo akakubali siku niliyoipanga nikamwambia tukutane wapi akaniambia tukutane Mlimani city nikasema si mbaya kweli siku na saa na hata dakika zikatimia huku tunawasiliana mrembo anatokea mbezi msela natokea zangu kiwalani nikaamua kupitia ubungo nipo buguruni kwenye mataa mtoto kansms nipo kimara hny nikamjibu poa nafika ubungo kwenye mataa kasweet aknsms tena baby nipo hapa ubungo nikmwambia poa hayujapishana sana baby akaniambia poa mimi nikawahi kufika. Nikamusms mi nipo getin naingia ushashuka kwenye gari akniambia bado ila nisubiti mlango wa kuingilia ndani nikamwambia poa sasa nikawa namtega kuwa je annikumbuka? Nikayulia huku naperuzi nakusoma post za Jf Mara nikahisi nikageuka Kwa mbali nikamuona anaingia getini halafu Mimi nipo mbali hajaniona nikasimama sehemu tofauti na makubakubaliano Mara akatoa simu mfukoni baada ya kufika pale nikageukia huko upande mwingine nikiwa bize na sim wakati nasubiri cm yangu iite bila mfanikio nikasema mbona hapigi tena nikatulia vile vile sasa simu ya ina mirror nikawa na mtazama Kwa kumuiba sana ghafla naona anakuja alivyo nikaribia akawa ananyata akanirukia na kunifunga macho nikamgeukia yaratibu bila wasiwasi nikamkumbatia akaniachia machoni naye akanikumbatia akanishangaa nakusema baby umejuaje ni Mimi? Nikamtania kuwa nimehisi mwili unahitaji nikajua si mwingine bali yeye tukacheka kisha tukasalimiana.
Sasa baada ya hapo nikamwambia eeh tuanzie wapi akaniambia tuingie ndani kwanza baby! Nikamkubalia tukaingia ndani ila nikamwambia mimi sina kazi kule ndani ila naenda Kwa ajili yake aksema poa tukazama ndani tukaenda moja Kwa moja kwenye vitu mgando baridi akachukua kimkebe kimoja akanambia twende nikamwbia imetosha aniambia ndio hii ndiyo napendelea sana nikamwambia poa nikamwambia sasa akaniambia kuanzia sasa nipo chini yako twende kokote nikasema mambo haya sasa nikaonelea ni vyema tukapate lunch kwanza maana muda huo saa sita na nusu tayari tukaingia sehemu moja ya heshima na baby tukaagiza kila mtu alichopenda wakati tunakula tukawa tunapiga story mbili yatu tulivyo maliza nikamwambia sasa tupande taks twende sehemu tukapumzike duh!! Ikawa balaa akaanza ooh mi sikujipanga nikamwambia mbona tulishapanga sasa kwann wewe hujipanga akaniambia kwanza mi nina MTU WANGU nikamwambia mbona hukusema mapema mpaka umeniamsha nyege zangu bhanaa? Akanimbia nisamehe ila Kwa hilo sitaweza nikamkubalia kuwa sawa kama umeamua hivyo sipendi nikulazimishe akanambia sawa tukaondoka nikampatia nauli akasepa nikamchunia kwa siku kafhaa akaanza mwenyewe! Mambo baby Mimi kimya. Akaniyumia SMS ya kuomba msamaha nikamwambia hujakosea Mimi ndio mwenye makosa kukupenda mpenzi wa MTU nae akanambia hata ni mimi sina kosa ni haki yangu kumpenda basi Mara yukajikuta tumerejesha mawasiliano tena. Mara nikataka tukutane tena niakubaliwa ila Kwa mashart ya kutokuwa faragha nikamgomea nakumpotezea baada ya yeye kuonyesha nsimamo Mara siku moja akaniambia anaomba nimuongezee kiasi cha pesa alikuwa na shida nayo nikamtumia akajirudisha tena nikaamua kukaza buti nia yangu asiendelee kunifuatilia kweli nikaganikiwa maana nilamkazia buti mpaka akachukia vibaya sana nikampotezea. Naye akawa kimya kirefu jidogo sasa juzi kati wiki hii inyiusha kanianza na visms nikamjibu Kwa uzuri tu Mara akaanza Nina shida ila nakuogopa nikamwambia unafopa nn akaniambia naogopa tuu nikamwambia haijakubana vizuri akasema IPO shingoni nikamwambia utapike akaanza naomba uniongezee hela kuna issue nataka niganye nikajua lambda elf kumi ishirini nikamuuliza ngapi? Kaniambia laki 2 nikamwambia saivi sin ila subiri nitafute kama nikipata, akaniambia sawa najua umeninyima Kwa sababu zako tu. Nikamuuliza zipi hizo? akanijibu unazijua wewe nikamwambia kwani unaitaka irudi lini best akaniambia sijui kama nitaweza kuirudisha nikamwambia basi vumilia nutafute mwisho kachukia hatuna mwasiliano tena ila bado ananitumia SMS Mara Kwa Mara nimfanyeje huyu MTU wa hivi? nimemuuliza kama kamuomba boy wake ananiambia hana sasa mi nimfanyeje?