Mbinu za kujitangaza msanii bila kiki

mcmzungu

Member
Jul 11, 2015
48
65
Binafsi Kama mdau wa sanaa na mwenye mahaba na Sanaa ya Muziki na filamu napenda kujitokeza kuleta mbinu ambazo zitasaidia Wasanii kujitangaza na kukuza sanaa zao bila kutumia Kiki.

Msanii unatakiwa kufanya kitu kizuri kutoa nyimbo nzuri au filamu nzuri ili kuchukua aina ya Watu ambao watakukubali hapa nina mfano wa Legendary wa Bongo fleva 'Dully Sykes' jamaa tangu enzi hizo aliamua kuimba kuhusu 'mabinti tu' na 'mapenzi'hii ilifanya apate nafasi ya kusikilizwa mno maana kuna msemo Unasema ukitaka sanaa yako ipendwe basi fanya Juu chini iguse wanawake na watoto hapo Utapenya tuu.

Katika filamu kuna jamaa Anaitwa Jimmy Mafufu binafsi Nampongeza sana yeye kaja na Style ya filamu za ubabe wa uswahilini,kiukweli anauza kuliko wasanii wakubwa japo soko la filamu linayumba jamaa Nina hakika anagonga copy tafuta movie zake Kama 'Ishakua soo',Kimenuka au 'Ndondo' hakika hutojuta ni ubunifu mzuri mno hii imesababisha jamaa anafanya vizuri sokoni.

Jambo lingine ni kujituma maana mwenye jukumu la kusimamia na kutangaza kazi zake ni msanii binafsi,Naumia sana Ninapofuatilia habari za wasanii Kama Ferooz,Daz Baba,Joselin,Q Chillah,Godzilla nk hawa ni baadhi ya wasanii Nikifuatilia katika mitandao ya kijamii ni 0 kabisa Hawajajua wana nguvu kiasi gani hamna habari zao za kuvutia zipo za zamani igeni mfano wa Ray C nyimbo zake nyingi zipo youtube hivyo Tukimkumbuka Tunadownload tu siku zote anakuwepo.

Ferooz juzi kati aliachia wimbo 'Nimejifunza'feat Maromboso japo sio kali hivyo mashabiki zako wa kweli Tulifanya juu chini kuupata huo wimbo lakini baadae Hatukusikia chochote si interview wala updates mpaka wimbo Umekufa kimya Kimya,hata Kama Radio hawapigi nyimbo kwa nini Usitumie youtube,instagram au face book yaani mpo zii hapana Bwana wekeni jitihada unaweza kuja ukaanza kutoa taarifa mitandaoni kupitia web mbalimbali Kama Bongo 5,millardayo,sam missago,dj mwanga nk sidhani Kama jamaa wanahitaji hela au magazetini nenda katafute mahojiano Mwenyewe.

Tunawapenda sana ila Mnatulostisha mashabiki wenu,movie pia ni vilevile fanyeni jitihada kutoa kazi nzuri kuonyesha si kwamba mnaziba pengo la Kanumba bali Kanumba hajaacha pengo, Gabo alikuwa anakuja vizuri lakini filamu za Watu anazocheza zinamshusha mfano movie gheto la uswazi hakustahili kucheza Zinamshusha.

Kingine Msanii Unapaswa uvae vizuri jukwaani au katika kazi yako kuvaa Kulimnyanyua sana Inspekta Haroun aka Babu,Mr Blue na H Baba jamaa walikuwa wanapendeza sana na ilikuwa utambulisho wao.katika filamu Ray,Kanumba na Tinno jamaa walikuwa wananyuka pamba si mchezo na ndio jambo kubwa Linambeba D kwa sasa (Kuvaa kupendeza),kuna msemo Unasema if you want success be different (Ukitaka kufanikiwa kuwa tofauti),Wanaijeria wamechukua beats za Wasanii wa zamani wa Tanzania kama Mr Nice nyimbo Kin'gasti,Ali kiba nyimbo Usiniseme,Mpenzi Bubu wa H Baba nk Wakaboresha tu why Wasanii wetu msije na Style mpya.

Tuna makabila 120 na zaidi kwa nini msitumie tafuteni nyimbo za wasafwa muone zilivyo tamu Kama Hawajatuiga hawa wanaijeria,Kihaya au Kizanaki ni nyimbo nzuri mno njooni na vitu vyetu wenyewe na nyie wa movie njooni na filamu zetu wenyewe za mashujaa wetu Nyerere,Sokoine nk au hamjui watoto wa. Com hawawajui waasisi wa Taifa letu tokeni hata na movie kuhusu wachuna ngozi ah ah ah Natania.Mwisho kwa kumalizia Wasanii waige utendaji wa kazi wa Diamond na Ali Kiba mpaka wameua soko la muziki wa congo.

Nakaribisha maoni na Nilipokosea ruksa kuongeza Nitafurahi Sana.

Wenu MC SIMON MZUNGU.

1477406069847.jpg


1477406137492.jpg


1477406146928.jpg
 
Mkuu ni ngumu kwa style hiyo angalia ata humu jf team zimeshika hatamu me nadhani wasanii wanadharau radio za mikoani kama msanii kila ataamua kufanya tua kila mwaka kupitia radio zote nchi zima atajijengea jínà sasa wasanii wadar wanathaminiwa lakini wao wana dharau
 
Kweli Mapensho star,radio za mikoani zina nguvu sana Nakumbuka Mbeya miaka kadhaa nyuma ilikuwa ukimzungumzia Izzo B Unazungumzia staa mkubwa sana sababu media za nyumbani zilimpa sapoti kiukweli wakitenga muda wa media tour za mkoani zitawajenga
 
Back
Top Bottom