Post yangu inaomba michango ya watu, ungeweza tu kusema katiba mpya bila kusema nazuga watu.
Hivyo vitu viwili huwezi kuvifanya wakati mmoja. Ukiidhoofisha CCM wakati vyama vya upinzani bado havijawa imara unatengeneza power vacuum kitu ambacho ni hatari kwa nchi na kinaondoa usalama. Huwezi kuimarisha vyama vya upinzani wakati CCM tayari iko imara. Itafanya kila mbinu kudhoofisha upinzani na kubaki madarakani. Ndiyo maana siasa za vyama vingi ni rahisi kuanza nchi ikiwa changa. Ukivileta baada ya chama kimoja kukaa madarakani miaka mingi ni vigumu kukitoa na ndiyo matatizo ya nchi nyingi za Afrika pamoja na Tanzania. Ilitakiwa wakati ule wa nchi za Afrika zinapata uhuru zianze na vyama vingi. Zingeweza, leo demokrasia ingekuwa imara sana Afrika.Habari za asubuhi wanajamvi.
Nimekuwa nikitafakari sana hali ya kisiasa nchini. Ni ukweli ulio wazi kuwa Chama tawala (CCM) ni chama kikubwa, chenye rasilimali watu na fedha pamoja na kufanya kazi kwa ukaribu na vyombo vya ulinzi na usalama, bila kusahau tentacles zake ziko kwenye kila eneo la serikali. Hizi ni facts, ni hali halisi kwa ground ambazo hatuwezi kupingana nazo au kujidanganya kuwa hazipo.
Kwa kutambua hilo, mbinu zozote za kupambana na CCM ni lazima zijumuishe ukweli huo. Ningependa kupata mawazo ya wadau, kama una mbinu yoyote inayozingatia hali halisi niliyoeleza tushauriane hapa. Mimi naanza na moja;
Kwa kuwa CCM ina watu kwenye vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na serikali, nashauri vyama vya upinzani navyo kuanza ku-recruit au kupandikiza watu huko. Mfano, kunapotokea kuna ajira za polisi/TRA/Uhamiaji nk...vyama vya upinzani vichukue jukumu la dhati kuhakikisha kuwa vijana wa chama, wenye imani na vyama hivi wanapata nafasi hizo. Kuanzia kwenye kuhimiza wajiunge mpaka ku-lobby pale inapowezekana ili navyo viwe na watu wao huko.
Je, wewe unashauri mbinu gani itumike kuidhoofisha CCM na/au kuimarisha vyama vya upinzani?
Zanzibar walipata Katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi tena inayojumuisha watu kutoka vyama vyote vya siasa.
Lakini mpaka leo hawajapata wanachokitaka pamoja na kuwa serious kuliko kawaida yenyewe.
Coalition Govt Haina future kwa watu wa kawaida.Kipi ambacho hawajakipata na wapo tayari ni coalitions government ambayo ndio future ya new democracy.
Shukrani sana kaka. Follow up question, je inawezekana ku-accelerate hili la Mataga mfano?
[/ rafiki unauonea Huruma upinzani ... Wameshindwa kufanya siasa za Wtz na kukosa umaarufu.. Mfano wa Cdm ya Dr Slaa waliupiga mwinyi ... Ikaja hii Cdm ya wafadhili .. Lkn muda upon wafanye siasa za Watz ... Mnashindwa hats na jeshi la MTU mmoja Gwajima
Hapo mwisho bado si swali sahihi. Kabla umesema vizuri kabisa kwamba lengo ni kuweka level playing field kwa vyama vyote. Sasa tatizo au suala la kushughulikiwa ni kuondoa ukiritimba (monopoly) wa chama kimoja ambacho kina hadhi batili ya chama dola na sio kutafuta namna ya vyama vya upinzani kuishinda CCM. Isije kuwa tunaondoa CCM na kuweka chama dola kingine. Demokrasia inataka uwazi (transparency) na ushiriki wa wananchi katika kuondoa chama dola na kuweka level playing field; sio mbinu za “uchochoroni”.Nadhani nimeeleza kidogo, kwa sasa uwanja haupo plain - mfano, mwenyekiti wa CCM (kila 5 years ni mgombea pia) anateua waamuzi (Tume). Kuidhoofisha kunalenga kufanya level plainfield kwa vyama vyote ili wananchi waweze kuchagua wamtakae.
However; sina attachment yoyote na maneno (heading) niliyotumia. Tusijikite sana kwenye maneno yaliyotumika, please tumia swali hili tupate mchango wako > Je ni mbinu gani vyama vya upinzani vinaweza kutumia kuishinda CCM?