Mbinu za kisasa za kuimarisha ndoa

Mbinu za kisasa za kuimarisha ndoa

Utakuta mwanaume umeoa mdada anaekupendea hela, kuna ndoa hapo?

Utakuta mwanaume umeoa mdada usiempenda bcoz huyo ndo ulieweza kumpata, kuna ndoa hapo?

Mwanamke umeolewa na mume ulienae bcoz wanaume uliowataka hawakutongozi, kuna ndoa hapo?

Wanandoa wengi wanaishi kwa kuvumiliana, si kwa kupendana Lenie
Hapo shida lazima iwepo sababu tangia mwanzo makosa yalifanyika. Inabidi kufanya juhudi binafsi kuokoa ndoa za hivyo otherwise ndoa inavunjika
 
huo upupu hau apply in real life labda katika maigizo
najua unalijua ilo, na hii mada ni kwa ajili ya kuchangamsha kijiwe, iko kinadharia zaidi, kivitendo ni kwenye filamu
No wonder ni KE tu ndio watasapoti maana wao ndio wana neemeka kwa vitu 2 vikuu:

1. kupatiwa fedha na

2. kufikishwa kileleni
Real life....?! Hivi unajua maana ya neno 'real life'?! So kila kinachotokea katika hii dunia ya leo ikiwemo kuvaa mawigi, uongo, usaliti, unafiki, maumivu na takataka zingine zote kwako ndio real life?!

Masikini, hadi nimekuonea huruma. Ila nikwambie jambo?! Hata mazingira nayo huchangia mtu kuwa wa namna fulani. Yaani kwa mfano, mtoto aliyezaliwa maisha ya kifukara, kwake real life ni mateso, kulala njaa, kukosa mahitaji muhimu, mbaya zaidi mafanikio kwake ni ndoto, real life kwake ni shida. Ila kuna mtoto wa kishua yeye kwake real life ni utelezi, anajiamini, chakula kipo hawazi, na anamatarajio sio ndoto bali matarajio ya kuwa na maisha.

Katika mahusiano ni hivyo hivyo, wakati wewe unaona picha halisi kwako ni usaliti, wivu, kudanganyana, na kukosa mapenzi ya kweli, kwako hiyo ndio real life ila sio life ya hii dunia as u know it. Kuna wengine wanajenga maisha ya furaha na upendo na uaminifu kama nilivyoelezea. Kama kwenu umekuzwa na misingi mibovu na maisha ya ajabu usiamini everyone anapitia hivyo.....

So check yourself again about hicho kipengele unachosema real life.... Ni real kwako but not in real life...
 
Ndo mana mimi hata ulivyokuwa ukinikera naenda kuchukua chumba hotelini kwa ajiri na kukunasa kofi..Haitakiwi kugombana ndani ya nyumba..
Ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha
 
Hivi ndivyo ndoa inapaswa kuwa. Wengi tunpenda ndoa zetu ziwe na amani na furaha, sema hatuweki bidii na jitihada. Ukiona vyaelea vimeundwa.
True. Na ndoa ikiwa hivi utanotice the difference kwenye maisha
 
Wewe hujakutana na mziki omba Mungu sana
Ukiutafuta mziki utakutana nao.... Unavutia cha kufanana na wewe......

Yaaani huko kando una mademu zaidi ya watano then unatafuta mwanamke mwaminifu... Mmmmmmmmhmn inawezekanaje...?!
 
Kwa bahati mbaya kizazi chetu pamoja na millennials hawajaandaliwa kuishi maisha ya ndoa kwa hiyo inapelekea kufanya makosa kila kukicha katika suala zima la ndoa
 
Nasikitika kusema kua ulichoandika ndio maingi imara wa ndoa yoyote.
Lakini baada ya miaka 5 ya ndoa au zaidi sijui kama kuna hata moja litakalofanyika hapo. Shida inaanza na ninyi wanaume kwakuanza kutuchoka sisi kutokana na mabadiliko ya kimaumbile..unakuta mwanaume kakamatika na bint wa 20 hapo humwambii kitu
Nadhani nimelizungumzia hilo swala kuwa katika ndoa, hufikia wakati wa kuzoeana na mkaona hakuna jipya. Hicho ndicho kipindi sasa mke na mume kama hawana hobbies za kufanana walau hata kwa 50% huwa inakuwa changamoto sana kuendelea kuishi pamoja.
 
Ubinafsi unawacost wengi ndio maana wanashindwa kuenjoy mahusiano/ndoa. Na kitu ukishajiwekea kwamba hakiwezekani basi itakua hivyo.
Kweli kabisa. Ndio maana hata katika shule kuna mtu anaamini katika kufeli na yupo anaye amini katika kufaulu.

Yupo anayeamini katika bidii ya kutafuta na yupo anayeamini katika kubahatisha. Hawa wana maisha ya tofauti sana.
 
Utakuta mwanaume umeoa mdada anaekupendea hela, kuna ndoa hapo?

Utakuta mwanaume umeoa mdada usiempenda bcoz huyo ndo ulieweza kumpata, kuna ndoa hapo?

Mwanamke umeolewa na mume ulienae bcoz wanaume uliowataka hawakutongozi, kuna ndoa hapo?

Wanandoa wengi wanaishi kwa kuvumiliana, si kwa kupendana Lenie
Sasa hapo shida si umeshaiona. Ukiingia katika ndoa kwa misingi ya tofauti hiyo kitu ni nadra sana kukutana nayo.....

Ule muda unajipanga kuanza mahusiano ndio muda wa kuzingatia mambo ya msingi kama hayo kuwa unaingia katika ndoa kwasababu gani,unaingia na nani?!
 
Hapo shida lazima iwepo sababu tangia mwanzo makosa yalifanyika. Inabidi kufanya juhudi binafsi kuokoa ndoa za hivyo otherwise ndoa inavunjika
Kabisa..... Ukishakosea katika msingi tayari unauwa kabisa future....
 
Unataka kuniambia hamna watu wanaofurahia ndoa zao kwenye hii nchi?
Unajua ukizungukwa na kampani ya walevi.... Utaamini kila mtu ni mnywaji, ukizungukwa na kampani ya wapenda wanawake na umalaya utaamini maisha ni kufanya umalaya.

Ukizungukwa na kampani ya watu walio katika mahusiano serious na kuheshimiana utaona maisha ni kuwa na mtu m'moja na kujiheshimu. Maisha ni vile vinavyokuzunguka.....
 
Na wapo wanaume wengi wanajielewa na wanajua nini maana ya ndoa.
Watu kama hao ndio mwisho wa siku akiwa anaona wewe na mwenzako mnajenga maisha mnagonga miaka tu mnachapa mwendo huku mnaimarika zaidi wao wanabakia kutoa macho na kutoamini kinachoendelea.

Kwa kifupi wanajifunza kwa matendo zaidi...... Na moyoni huwa wanastaajabu sana......
 
Mtoa mada umeongea mambo mazuri ila swala la communication ni muhimu sana kwa wanandoa kwa kuzingatia 5Ws;Who,where,what, when and how.
 
Katika maisha yangu, nimejitahidi sana kujifunza masuala ya kujenga na kuimarisha mwenendo katika nyanja mbali mbali za maisha.

Eneo mojawapo ninalojifunza pia ni eneo la mahusiano ya uchumba na ndoa.

Leo napenda kushare nanyi mienendo itakayosaidia kujenga, kuimarisha na kuboresha mahusiano. Nitoe tu angalizo kuwa hizi mbinu sio kwa vijana ambao mko katika mapenzi ya kihuni au mnaopotezeana muda bali hizi zipo kwaajiri ya watu wanaojiandaa kufanya maisha serious na wenza wao na wale waliopo katika ndoa.

Amani na utulivu ni kiungo muhimu sana cha ndoa. Na ndicho husaidia kuleta ushikamano na umoja. Si kwamba ukiwa na amani na utulivu basi imaanishe kuwa hakuna matatizo na tofauti baina yenu, la hasha. Ila kimsingi ni kuwa mnachagua kudeal na matatizo kwa hali ya utulivu na staha.

Nilikaa na mzee m'moja na mtoto wake wa kiume brother wa age ya kama 40 hivi, mwenye busara zake na ambaye hadi sana yeye na mkewe wanasheherekea jubilee ya ndoa ya miaka 54 wakiwa pamoja tokea ujana.

Moja wapo ya mambo wamenifunza ni kama ifuatavyo:

1. Unapoelekea nyumbani kutoka popote utokapo, tambua na jijenge kutambua kuwa nyumbani ndipo moyo ulipo (a home is where your heart is), hivyo sehemu unapoweka moyo wako basi ni lazima pawe ni pahala pa utulivu.

2. Mwenza wako si adui wala mshindani wako, ni kivuli au copy yako. Yaani kama vile picha na negative.... Kwahivyo unapotoka yeye aidha umemuacha nyumbani au mlitoka nyote akienda katika mihangaiko, unapofika muda wa jioni ndie unakwenda kumuona na anahamu ya kukuona hivyo tengeneza shauku ya kumuona na kujua ameshindaje, lakini pia tarajia mwenzako anataka kukuona pia so furahia hilo tukio la kwenda kumuona nusu ya wewe.

3. Unapotoka huko utokako, hasira,visa, visirani, jazba na ukorofi, unapoingia getini ama kizingiti cha mlango, vikane kama vile unavyokana mambo mabaya uingiapo nyumba ya ibada. Kumbuka unaingia nyumbani sehemu patakatifu pa familia ambapo amani na upendo hutawala. Hivyo basi unapoingia kila lihusulo upendo na amani ndilo linatakiwa.
Lugha ya upole, lugha ya huruma na upendo. Kujaliana na kuheshimu. Ndio maana simu huwa zinawekwa kando na kuanza kupeana attention ya jumla kwa kufanya maswala ya mahusiano na ya kifamilia zaidi kwa asilimia 80%, sio kwamba usipokee simu au kuzima kabisa.

4. Kila unaporudi basi rejea na jipya la kufanya mwenzako ajue kuwa ulikuwa unamuwaza au anajaliwa na wewe. Yapo mengi ya kufanya. Wazee wetu wanasema wao walikuwa wanarudi na kitoweo cha kesho au hata matunda. Ila vyovyote wakirudi hawakosi kifurushi mkononi ili mke ajue huko ulikotoka basi yeye ulimuwaza yeye na familia yenu......

5. Usiruhusu nyumba ikawa sehemu ya kujadili matatizo ya yenu. Yaani ni vema mkiwa na matatizo mtafute sehemu ya uwazi kama ufukweni, au bustanini, muende mkajadili ili pindi mnaporejea tofauti zenu ziwe zimerekebika na mnapofika katika geti la nyumba au kizingiti cha mlango basi hizo kelele mnaziacha mlangoni na kuingia ndani katika nyumba yenu kuendeleza misingi ya amani na upendo.

Kitendo cha kupuuza huu msingi kumefanya wengi kugeuza nyumba kama uwanja wa vita, matokeo yake hata baada ya marumbano mtu anaporejea kesho yake roho wachafu wa mafarakano na hasira zilizotolewa zinakuwapo katika kila kona ya chumba na nyumba nzima. Ndio ile mtu anapofika mtaani tu akiitazama nyumba yake au pahali anaishi tayari anachafukwa roho na kujiandaa kwa shari kumkabiri mwenzake. Anapoingia ndani akatazama vitanda, mashuka, kuta za eneo fujo na kelele zimefanyikia, basi atakumbuka kwa urahisi madhira yaliyotokea na hii itamfanya aone sura ile ile ya shari ya jana na hapo hapo neno amani na utulivu huwa linakuwa halina uwiano na eneo alipo na ndipo wengine anabadili nguo na kutoka zake kwenda bar na kurejea usiku sana.

6. Tendo la ndoa huwa ni kiashiria cha msisimko wa mwili wenye amani na utulivu. Lakini watu wengi hutia nguvu katika tendo la ndoa tu kabla ya kutazama msisimko wa kihisia ambao unahitaji umakini sana kuumaintaini. Msisimko wa hisia huenda sambamba na kujaliana hisia, kuoneana huruma, kupeana attention, kusikilizwa na kusikiliza, na kufanyiana matendo mema. Mtu anayejufanyia hivi, akiketi pembeni yako, ukijumlisha na amani na upendo katika nyumba, na kuacha maumivu nje ya mlango, huyu mtu lazima upate hamu ya kumtaka joto lake muda huo huo sababu uwepo wake hutengeneza ubaridi wa upweke wa nafasi kiasi kwamba utataka asogee karibu yako akupe joto. Hilo likitokea ni wazi mtaangukia katika tendo la ndoa na kutaka kupeana mahaba.

7. Chakula ni sehemu ya ibada katika maisha ya mwanadamu. Wanawake wanaelekezwa kujifunza kupika vyakula vyenye maudhui ya kuimarisha na kurutubisha miili ya wanaume zao na watoto kuwapa afya. Mwanamke anaepika chakula bila kuzingatia haya huiangamiza familia yake mwenyewe kwa maradhi ya mwili kama pressure, kisukari, kiribatumbo, utapiamlo, upungufu wa nguvu za kiume na kadhalika. Hivyo basi kwa kuendelea kwa technology kwasasa tunayonafasi ya kujifunza na wake zetu mapishi mbali mbali ya vyakula asili na kufanya nao mazoezi pale tunapopata nafasi na wakati.

Hii husaidia familia kuwa na ulinzi wa kiafya na kuisaidia familia kuondokana na kero za maradhi, misiba, na kukosekana kwa stamina ya mume kwa mkewe.

8. Vijana wengi hutumia vibaya neno "Dating" kwao kumaanisha kulala na mwanamke au kwa mabinti wao ni muda wa kuchuna au kudanga. Hii sio maana ya halisi ya kudate. Kudate ni kipindi binti na mvulana wanapata wakati wa kufahamiana kwa undani kwa maana ya tabia, mienendo, hobbies na kusomana mapungufu. Hii yote inaweza fanyika bila ya kukutana nimwili, wakaishia mabusu, na hug basi bikra ikabakia salama. Kipindi cha dating ndipo unaweza soma tabia za awali za mwenzako na kumjua hata kabla ya kuanza uhusiano. Kitu muhimu cha kuobserve nyakati hizi ni swala la hobbies. Yaani yale mambo ya ziada ambayo unapenda kufanya. Mfano unapenda kupika, unapenda kutengeza bustani, unapenda kusoma vitabu, unapenda kutazama movies, au unapenda sikiliza muziki, au unapenda kufanya muziki, any type of hobby. Ikitokea hobbies zina match kwa asilimia above 50% then huyo mtu utakuwa na nafasi kubwa sana ya kufanya nae maisha sababu ya kufanana upande wa hobby. Hobbies husaidia sana watu waliozoeana kwenda sambamba (getting along) kipindi wakizoeana wakati wa ndoa na wakiwa katika maisha ya ndoa.

9. A family that pray together, stays together. Utamaduni wa kusali au kufanya ibada huwa unahusisha na kupata muda na kuelimishana juu ya maswala ya matendo mema ya kumpendeza MUNGU. Nimegundua mtu anaweza kuwa mwepesi kumlaumu mkewe au mumewe kutokwenda nyumba za ibada ila akasahau kuketi nae chini na kujitathimini mienendo yao ya kila siku na kupeana mafunzo na maelekezo. That is part of praying for the two. Sio tu kwenda kanisani na kupiga goti kusali. Keti kitako na mkeo na mumeo muelimishane kwa utaratibu na kwa upendo juu ya mifumo isiyofaa ya kimaisha ya ujana. Muishi kwa namna za kumpendeza MUNGU, ulinzi wa kweli wa kiimani huanza na tathmini ya kimatendo na mienendo yetu ya kila siku. Si vibaya kumuelimisha mkeo juu ya madhara ya kuwa na tamaa ya kupewa lifti na wanaume wenye tamaa za fisi ambacho kutwa wao kazi kuwinda wake za watu na kutaka kuwavua chupi kisha kuachana nao. Wanawake wengi huingia na ujinga na ulimbukeni vichwani mwao ya kwamba pamoja na kuwa wapo katika mahusiano ya uchumba au ndoa ila bado wanahaki ya kuleta mazoea ya kipuuzi na wanaume wengine jambo ambalo ni kosa kubwa. Pia ni vema wanawake kuketi kitako na wanaume zao wakiwaelezea namna nzuri ya kuwasaidia ili wawe karibu na kuongeza mvuto kwao na sio kuishi kwa kununiana au kutegemea vitendo vitaongea.....

10. Tazama na kuwa makini sana na nani unaemleta katika nyumba yako. Awe ni rafiki, ndugu, jirani, au nani sijui. Watu huja na baraka zao lakini pia watu huja na matatizo yao ambayo yanaweza kuwavurugia amani na utulivu wenu mlioutengeneza. Unaweza mleta mama yako mzazi, kutokana na mwenendo wake akageuka kuwa tatizo, inaweza kuwa mdogo wako, au mtoto wa nduguyo wote hawa wakawa tatizo katika nyumba yako. Sisemi watu ni wabaya no bali nasema kuwa makini na nani anaingia katika nyumba yako yenye amani na utulivu.

Haya ni baadhi ya machache tulijadili na mimi nikawa natake note ya yale muhimu tulikuwa tunajadili na kuamua kushare nanyi.
Nimelipenda somo lako.Nitajitahidi kufanyia kazi huu ushauri.Wengi wameua wake/waume zao.Wengi wameacha watoto wakiwa yatima,wengi wametalakiana ,wengi wamepata ukilema na wengi wamefirisika ila chanzo ni kushindwa kuheshimu kanuni za ndoa/mahusiano."NAKUPENDA MKE WANGU,HESHIMU MAHUSIANO YETU,NAMI NAAHIDI KUYAHESHIMU.Amiin."
 
Back
Top Bottom