Mbinu za kisasa za kuimarisha ndoa

Samcezar

JF-Expert Member
May 18, 2014
13,096
22,625
Katika maisha yangu, nimejitahidi sana kujifunza masuala ya kujenga na kuimarisha mwenendo katika nyanja mbali mbali za maisha.

Eneo mojawapo ninalojifunza pia ni eneo la mahusiano ya uchumba na ndoa.

Leo napenda kushare nanyi mienendo itakayosaidia kujenga, kuimarisha na kuboresha mahusiano. Nitoe tu angalizo kuwa hizi mbinu sio kwa vijana ambao mko katika mapenzi ya kihuni au mnaopotezeana muda bali hizi zipo kwaajiri ya watu wanaojiandaa kufanya maisha serious na wenza wao na wale waliopo katika ndoa.

Amani na utulivu ni kiungo muhimu sana cha ndoa. Na ndicho husaidia kuleta ushikamano na umoja. Si kwamba ukiwa na amani na utulivu basi imaanishe kuwa hakuna matatizo na tofauti baina yenu, la hasha. Ila kimsingi ni kuwa mnachagua kudeal na matatizo kwa hali ya utulivu na staha.

Nilikaa na mzee m'moja na mtoto wake wa kiume brother wa age ya kama 40 hivi, mwenye busara zake na ambaye hadi sana yeye na mkewe wanasheherekea jubilee ya ndoa ya miaka 54 wakiwa pamoja tokea ujana.

Moja wapo ya mambo wamenifunza ni kama ifuatavyo:

1. Unapoelekea nyumbani kutoka popote utokapo, tambua na jijenge kutambua kuwa nyumbani ndipo moyo ulipo (a home is where your heart is), hivyo sehemu unapoweka moyo wako basi ni lazima pawe ni pahala pa utulivu.

2. Mwenza wako si adui wala mshindani wako, ni kivuli au copy yako. Yaani kama vile picha na negative.... Kwahivyo unapotoka yeye aidha umemuacha nyumbani au mlitoka nyote akienda katika mihangaiko, unapofika muda wa jioni ndie unakwenda kumuona na anahamu ya kukuona hivyo tengeneza shauku ya kumuona na kujua ameshindaje, lakini pia tarajia mwenzako anataka kukuona pia so furahia hilo tukio la kwenda kumuona nusu ya wewe.

3. Unapotoka huko utokako, hasira,visa, visirani, jazba na ukorofi, unapoingia getini ama kizingiti cha mlango, vikane kama vile unavyokana mambo mabaya uingiapo nyumba ya ibada. Kumbuka unaingia nyumbani sehemu patakatifu pa familia ambapo amani na upendo hutawala. Hivyo basi unapoingia kila lihusulo upendo na amani ndilo linatakiwa.

Lugha ya upole, lugha ya huruma na upendo. Kujaliana na kuheshimu. Ndio maana simu huwa zinawekwa kando na kuanza kupeana attention ya jumla kwa kufanya maswala ya mahusiano na ya kifamilia zaidi kwa asilimia 80%, sio kwamba usipokee simu au kuzima kabisa.

4. Kila unaporudi basi rejea na jipya la kufanya mwenzako ajue kuwa ulikuwa unamuwaza au anajaliwa na wewe. Yapo mengi ya kufanya. Wazee wetu wanasema wao walikuwa wanarudi na kitoweo cha kesho au hata matunda. Ila vyovyote wakirudi hawakosi kifurushi mkononi ili mke ajue huko ulikotoka basi yeye ulimuwaza yeye na familia yenu......

5. Usiruhusu nyumba ikawa sehemu ya kujadili matatizo ya yenu. Yaani ni vema mkiwa na matatizo mtafute sehemu ya uwazi kama ufukweni, au bustanini, muende mkajadili ili pindi mnaporejea tofauti zenu ziwe zimerekebika na mnapofika katika geti la nyumba au kizingiti cha mlango basi hizo kelele mnaziacha mlangoni na kuingia ndani katika nyumba yenu kuendeleza misingi ya amani na upendo.

Kitendo cha kupuuza huu msingi kumefanya wengi kugeuza nyumba kama uwanja wa vita, matokeo yake hata baada ya marumbano mtu anaporejea kesho yake roho wachafu wa mafarakano na hasira zilizotolewa zinakuwapo katika kila kona ya chumba na nyumba nzima. Ndio ile mtu anapofika mtaani tu akiitazama nyumba yake au pahali anaishi tayari anachafukwa roho na kujiandaa kwa shari kumkabiri mwenzake.

Anapoingia ndani akatazama vitanda, mashuka, kuta za eneo fujo na kelele zimefanyikia, basi atakumbuka kwa urahisi madhira yaliyotokea na hii itamfanya aone sura ile ile ya shari ya jana na hapo hapo neno amani na utulivu huwa linakuwa halina uwiano na eneo alipo na ndipo wengine anabadili nguo na kutoka zake kwenda bar na kurejea usiku sana.

6. Tendo la ndoa huwa ni kiashiria cha msisimko wa mwili wenye amani na utulivu. Lakini watu wengi hutia nguvu katika tendo la ndoa tu kabla ya kutazama msisimko wa kihisia ambao unahitaji umakini sana kuumaintaini. Msisimko wa hisia huenda sambamba na kujaliana hisia, kuoneana huruma, kupeana attention, kusikilizwa na kusikiliza, na kufanyiana matendo mema.

Mtu anayejufanyia hivi, akiketi pembeni yako, ukijumlisha na amani na upendo katika nyumba, na kuacha maumivu nje ya mlango, huyu mtu lazima upate hamu ya kumtaka joto lake muda huo huo sababu uwepo wake hutengeneza ubaridi wa upweke wa nafasi kiasi kwamba utataka asogee karibu yako akupe joto. Hilo likitokea ni wazi mtaangukia katika tendo la ndoa na kutaka kupeana mahaba.

7. Chakula ni sehemu ya ibada katika maisha ya mwanadamu. Wanawake wanaelekezwa kujifunza kupika vyakula vyenye maudhui ya kuimarisha na kurutubisha miili ya wanaume zao na watoto kuwapa afya. Mwanamke anaepika chakula bila kuzingatia haya huiangamiza familia yake mwenyewe kwa maradhi ya mwili kama pressure, kisukari, kiribatumbo, utapiamlo, upungufu wa nguvu za kiume na kadhalika. Hivyo basi kwa kuendelea kwa technology kwasasa tunayonafasi ya kujifunza na wake zetu mapishi mbali mbali ya vyakula asili na kufanya nao mazoezi pale tunapopata nafasi na wakati.

Hii husaidia familia kuwa na ulinzi wa kiafya na kuisaidia familia kuondokana na kero za maradhi, misiba, na kukosekana kwa stamina ya mume kwa mkewe.

8. Vijana wengi hutumia vibaya neno "Dating" kwao kumaanisha kulala na mwanamke au kwa mabinti wao ni muda wa kuchuna au kudanga. Hii sio maana ya halisi ya kudate. Kudate ni kipindi binti na mvulana wanapata wakati wa kufahamiana kwa undani kwa maana ya tabia, mienendo, hobbies na kusomana mapungufu. Hii yote inaweza fanyika bila ya kukutana nimwili, wakaishia mabusu, na hug basi bikra ikabakia salama. Kipindi cha dating ndipo unaweza soma tabia za awali za mwenzako na kumjua hata kabla ya kuanza uhusiano. Kitu muhimu cha kuobserve nyakati hizi ni swala la hobbies.

Yaani yale mambo ya ziada ambayo unapenda kufanya. Mfano unapenda kupika, unapenda kutengeza bustani, unapenda kusoma vitabu, unapenda kutazama movies, au unapenda sikiliza muziki, au unapenda kufanya muziki, any type of hobby. Ikitokea hobbies zina match kwa asilimia above 50% then huyo mtu utakuwa na nafasi kubwa sana ya kufanya nae maisha sababu ya kufanana upande wa hobby. Hobbies husaidia sana watu waliozoeana kwenda sambamba (getting along) kipindi wakizoeana wakati wa ndoa na wakiwa katika maisha ya ndoa.

9. A family that pray together, stays together. Utamaduni wa kusali au kufanya ibada huwa unahusisha na kupata muda na kuelimishana juu ya maswala ya matendo mema ya kumpendeza MUNGU. Nimegundua mtu anaweza kuwa mwepesi kumlaumu mkewe au mumewe kutokwenda nyumba za ibada ila akasahau kuketi nae chini na kujitathimini mienendo yao ya kila siku na kupeana mafunzo na maelekezo. That is part of praying for the two. Sio tu kwenda kanisani na kupiga goti kusali. Keti kitako na mkeo na mumeo muelimishane kwa utaratibu na kwa upendo juu ya mifumo isiyofaa ya kimaisha ya ujana.

Muishi kwa namna za kumpendeza MUNGU, ulinzi wa kweli wa kiimani huanza na tathmini ya kimatendo na mienendo yetu ya kila siku. Si vibaya kumuelimisha mkeo juu ya madhara ya kuwa na tamaa ya kupewa lifti na wanaume wenye tamaa za fisi ambacho kutwa wao kazi kuwinda wake za watu na kutaka kuwavua chupi kisha kuachana nao.

Wanawake wengi huingia na ujinga na ulimbukeni vichwani mwao ya kwamba pamoja na kuwa wapo katika mahusiano ya uchumba au ndoa ila bado wanahaki ya kuleta mazoea ya kipuuzi na wanaume wengine jambo ambalo ni kosa kubwa. Pia ni vema wanawake kuketi kitako na wanaume zao wakiwaelezea namna nzuri ya kuwasaidia ili wawe karibu na kuongeza mvuto kwao na sio kuishi kwa kununiana au kutegemea vitendo vitaongea.....

10. Tazama na kuwa makini sana na nani unaemleta katika nyumba yako. Awe ni rafiki, ndugu, jirani, au nani sijui. Watu huja na baraka zao lakini pia watu huja na matatizo yao ambayo yanaweza kuwavurugia amani na utulivu wenu mlioutengeneza. Unaweza mleta mama yako mzazi, kutokana na mwenendo wake akageuka kuwa tatizo, inaweza kuwa mdogo wako, au mtoto wa nduguyo wote hawa wakawa tatizo katika nyumba yako. Sisemi watu ni wabaya no bali nasema kuwa makini na nani anaingia katika nyumba yako yenye amani na utulivu.

Haya ni baadhi ya machache tulijadili na mimi nikawa natake note ya yale muhimu tulikuwa tunajadili na kuamua kushare nanyi.
 
Kitabu cha kanuni ya ndoa Mungu alikifuta tangu hawa alipokula tunda LA mti was kati. Kanuni ya maisha nayo Adamu aliiacha eden. Kwahiyo mafanikio na furaha ya ndoa vyote sasahivi havina kanuni
 
Vizuri saana but hujafafanua unazungumzia wanawake wa kufanyiwa hivyo vitu wanapatikana wapi maana waliopo ni money first and then othors follow
 
Hizi mbinu labda malaika toka mbinguni washuke wabadilike kuwa wanawake ndio wataziweza
 
Umeongea vyema sana japo wakati mwingine kuna hasira huwa zinakuwepo tu hasa ukikuta mke mwenye mdomo kama chiriku
Hapo ndipo shida yenyewe.... Ndio maana nikasema ni marufuku kugeuza nyumba sehemu ya kutatua magomvi, mnamkaribisha shetani katika nyumba na akiingia kumfukuza katika kuta za nyumba ni kazi...... Heshimu sana nyumba, pale ndipo taasisi takatifu yaani familia huwa inajengwa.
 
Hata hapa bongo inawezekana mkipendana kwa dhati na kama kila mtu akitambua nafasi ya mwenza wake kwenye maisha yake.
Kabisa....

Watu wanapenda kukata tamaa na kusubiria mrejesho tokea kwa mwenzake......yaani mtu anasema anataka mapenzi ya ukweli ile hali yeye hataki kuwa na upendo kwa mwenzake anataka yeye ndio apendwe kwanza....... You receive what you give...... Ni kama kwenye biashara ukitoa pesa ndipo utapata pesa...
 
Kitabu cha kanuni ya ndoa Mungu alikifuta tangu hawa alipokula tunda LA mti was kati. Kanuni ya maisha nayo Adamu aliiacha eden. Kwahiyo mafanikio na furaha ya ndoa vyote sasahivi havina kanuni
Mmmmmmhmn wewe hebu usitupoteze sasa. Yaani unataka kusema kuwa ndoa ni kitu haramu na MUNGU hakitambui au?!
 
Back
Top Bottom