Ukweli kuhusu biashara ya pesa za zamani

Broadcast

Member
Jun 19, 2022
60
195
Ni kawaida sana kupita sehemu ukasikia tangazo la mtu kununua pesa za kigeni, pesa mbovu au pesa za zamani. Yes, pesa hizi zinanunuliwa kulingana na thamani; mfano elfu 10 mbovu atakupatia elfu 8 yeye akipeleka bank anapata elfu 10 ile ile na yeye anakuwa kapata faida ya shilingi elfu 2 mana bank hawakatai pesa eti kisa mbovu.

Je, umewahi kusikia kuwa pesa hizo (mia tano) za zamani kuna watu wananunua na kuna wengine wanatangaza kuwa wananunua mpaka shilingi milioni moja kwa noti moja? Ngoja kwanza nikupe darasa kidogo.

Ukweli ni kwamba hizo hela hazina kazi yoyote, na hakuna anaezinunua. Ila wajanja wenzangu watoto wa town kila kukicha wanaamka na akili ya kupata pesa, maana ajira zenyewe hakuna na kama unavyojua wajinga wa kuibiwa mjini huwa hawaishi.

Wanachofanya anatokea mtu mmoja anatangaza ananunua hizo noti kwa shilingi elfu 2 kila moja. Yoyote aliekuwa nazo atajitokeza tuu, kisha watakuja kununua kwako kwa labda watasema wanataka noti 20 jumla watakupatia shilingi elfu 40. Kisha watakuacha unachelelea na wao watajifanya wajinga wanaondoka na hizo noti, kisha watachukua namba zako na kukuomba ukipata noti nyingine uwapigie.

Baada ya siku 3 utapigiwa simu na mtu yoyote (kumbuka walichukua namba zako) kisha atajitambulisha kuwa ni wale wanaonunua pesa za zamani za 500 na wanaomba kama ukipata nyingine uwaambie maana kwa sasa wamepata soko kubwa zaidi na watanunua kila noti kwa shilingi elfu 50 badala ya shilingi elfu 2 ya mwanzo.

Kwanza ukiskia hivi utawaamini, maana walishakuja kwako kununua na hawana longo longo, so kisaikolojia watakuwa wakekupa kazi mbili.

Kwanza kutafuta hizo noti kwa udi na uvumba, pili utakuwa tayari hata kwenda kukopa pesa ili ununue hizo noti mtaani kisha uje kuwauzia hao matajiri.

Baada ya kukata tu simu jioni ya siku hiyo, eidha kuna kijana atakuja kwenu au pale mlipokutana na wateja wako wa mwanzo akiwa na noti za 500 za kutosha tu, kisha atakuulizia umsaidie kutafuta soko kama unajua zinaponunuliwa.

Kumbuka wateja wa mwanzo ulikutana nao kwako au kijiweni kwako so wanajua pa kukupata na kama mlikutana tuu mtaani basi utapokea simu toka kwa mtu atasema anazo noti za 500 za zamani na anaomba umtafutie soko ila yeye anataka elfu 20 tuu kwa kila noti.

Wewe ukipiga hesabu wateja wako pendwa mwanzo walinunua kwa elfu 2, yaani katika noti 20 zenye thamani ya shilingi elfu 10 wao walikupa elfu 40 na kwa sasa wanataka kila noti kwa shilingi elfu 50 yaani kwa noti 20 za 500 ya zamani zenye thamani ya shilingi elfu 10 wao watalipa jumla ya shilingi milioni moja.

Hapo ndio unaamua kukopa pesa unanunua hizi noti za huyu aliekuja kukuomba umtafutie soko, maana zake anauza kwa elfu 20 kila noti, tena unanunua zote ili ukauze kwa elfu 50 kwa kila noti, maana wateja wako nao wanapiga simu kila mara kuulizia ila usichofahamu ni kwamba wote lao moja na ukishatoa hela ukanunua hizi noti za huyu jamaa kwa Lengo la kuja kuwauzia wateja zako basi ishakula kwako.

Yaani wakipata taarifa umeshanunua tu, maana yake hela yao imerudi na faida juu na kuanzia hapo unakula block hadi kwenye komwe lako kwakuwa walikupatia elfu 40 mwanzo ukajiona mjanja ila wao wamekuuzia tena zote kwa shilingi laki 8 .
 
Sasa kama wapo mitaani wakitangaza wananunua pesa za zamani si wapigwe pin kuwa wanatapeli watu?
 
PXL_20231121_141558810.jpg
hii pesa bado inatumika..?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom