Mbinu mpya ya Wezi ( Tafadhali pitia hapa )

Mbinu mpya ya Wezi ( Tafadhali pitia hapa )

b191

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2016
Posts
742
Reaction score
1,032
Habari wandugu!

Nisipoteze muda, naomba niende moja kwa moja kwenye Topic.

Huku mtaani kwenu kuna mbinu mpya ambayo wezi wamegundua ili kutuibia kiurahisi nyakati za Usiku.

1. Wizi wa Majumbani, wakifika nyumbani kwako na wakaona ndani hakuingiliki na nje kuna Bomba la Maji na maji yanatoka.

Hawa wezi hufungulia maji na kuacha yamwagike. Wewe ukiwa ndani na ukasikia maji yanamwagika utaamua kufungua mlango na kwenda kufunga maji.

Ukifungua tu mlango unakutana na Wazee wa Kazi. Hapo wanaingia ndani kiulaini.

ANGALIZO.
i. Kabla ya kufunga mlango / milango ya nje hakikisha Bomba la maji limefungwa vizuri

ii. Usitoke peke yako nje unaposikia maji yanamwagika

2. Wizi wa simu barabarani, hii inawahusu sana wale wanaotembea barabarani kwa mguu usiku huku wakitumia simu.

Hapa vibaka huja na Ndoo kubwa ya maji (isiyo na maji).

Wanapokufikia hukufunika kwa haraka sana na kukunyang'anya simu.

Unapomaliza kuvua hiyo ndoo ya maji wao wanakuwa wamekwisha kukimbia.

ANGALIZO.
Unapotembea usiku huku ukitumia simu chukua tahadhari.

NB: Unaweza pia kuongezea mbinu nyingine wanayotumia / wanazotumia wezi kutuibia ili kila mtu achukue tahadhari.

Ninawasilisha.
 
pia kuna wale wezi wa waume za watu, wanakuja wakiwa na nguo za kuonesha maungo yao!

ANGALIZO,

Mume tembea na mke wako!
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Daea ya wezi we fuga mbwa tu. Hata asipokua mkali akishahisi mtu tofauti tu lazima abweke.
 
Wiz wakati wa kununua mbao ukienda nunua mbao kabla ya kupimiwa mbao ili ununue kagua futi ya kupimia

Mara nyingi wanakuwa na fut zao za kuunga unga yani ikitoka 1,2 baada ya kufuata 3 fut zao zinafuata na 6 au 7 hapo kuna kama fut 3 au 4 umeshaibiwa.

Na walivyo wajanja wanakuweka mwishon mwa mbao kumbe huku mwanzon unaliwa tu.

Yamenikuta haya pale kimara kwa msuguri kuweni makin pona pona yangu fundi alipo kuja baada ya kumwambia mbona hesabu uliyo nipa ni ndogo huku wananipa hesabu kubwa!!

Fundi alinipa hesabu ya laki 4 wao wakafika laki 6 pumbavu sana hawa nawajua vizur mpaka dukani kwao nilitaka kuwaaribia kwa bos wao sema walinitoa kidogo..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[BALAAA]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli hao wezi wakufunika watu na ndoo wamestaharabika sana! Huku Kwetu unapigwa roba mpaka ujambe ndo wakuachie.
 
Wiz wakati wa kununua mbao ukienda nunua mbao kabla ya kupimiwa mbao ili ununue kagua futi ya kupimia

Mara nyingi wanakuwa na fut zao za kuunga unga yani ikitoka 1,2 baada ya kufuata 3 fut zao zinafuata na 6 au 7 hapo kuna kama fut 3 au 4 umeshaibiwa.

Na walivyo wajanja wanakuweka mwishon mwa mbao kumbe huku mwanzon unaliwa tu.

Yamenikuta haya pale kimara kwa msuguri kuweni makin pona pona yangu fundi alipo kuja baada ya kumwambia mbona hesabu uliyo nipa ni ndogo huku wananipa hesabu kubwa!!

Fundi alinipa hesabu ya laki 4 wao wakafika laki 6 pumbavu sana hawa nawajua vizur mpaka dukani kwao nilitaka kuwaaribia kwa bos wao sema walinitoa kidogo..

Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo dar huwezi kuwa makini na kila kitu, kuna mahali watakupata tu tena kijinga!
 
....Mpaka wafikie bomba la maji ili walifungue kikosi changu cha mbwa ambao hawapendagi kubweka bweka, hao wezi watakuwa wanavuja damu kila mahali.
 
Dah...hiyo ya vibaka kumvisha muhanga wao ndoo na kumuacha akihangaika nayo ilimtokea jamaa yangu maeneo ya Kinondoni Moscow but yeye walimvisha roba kubwa wakachukua simu mbili saa na wallet,jamaa ktk kuweweseka weweseka akajikuta anajipiga mtama akaanguka kwenye mtaro wa maji machafu akapasuka mdomoni.hawa jamaa hawafai kila siku wanabuni style mpya kutuibia.

sent from my Infinix S2 Pro using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom