Mbinu mpya ya CCM; Tuwe makini

Mbinu mpya ya CCM; Tuwe makini

Paul Alex

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2012
Posts
4,344
Reaction score
9,845
Jana kilifanyika kikao cha dharura Ikulu baada ya Mbatia kumaliza kuhutubia, na walikubaliana yafuatayo;

1. January Makamba amjibu Mbatia ili kupunguza concentration ya watu kwenye hotuba ya Mbatia. (Hili limetekelezwa).

2. Magufuli atumie brand name ya M4C ili kuwachanganya wapiga kura. Wanaamini kuna wapiga kura hawamjui Magufuli lakini wakiambiwa M4C watampigia kura. Hii idea ilitolewa na January. (Hili limeanza kutekelezwa kwa kuchapisha mabango mengi yenye lebo ya M4C wakidai ni Magufuli 4 Change).

3. Mama Maria Nyerere atumike kuongea na mke wa Magufuli ili akubali kuambatana na mumewe kwenye mikutano ya Kampeni. Ikumbukwe mke wa Magufuli (mama Mawalwa) amekataa kuambatana na mumewe kwa sababu anazodai ni za kifamilia. Mama Salma Kikwete, Tunu Pinda na Magreth Sitta (ambao wote ni waalimu) wamejaribu kuongea na mwalimu mwenzao lakini amekataa. So karata ya mwisho iliyobaki ni Maria Nyerere.

4. Dr.Wilbroad Slaa apandishwe jukwaani wiki mbili za mwisho kumnadi Magufuli. Akirudi kutoka Marekani atafanya press aeleze kuwa baada ya kutafakari ameona mgombea anayefaa ni Magufuli. Baada ya hapo ataanza kutembea nae kumnadi huku akitumia hoja ya ufisadi kumchafua Lowassa. Wanaamini hii itapunguza sana nguvu ya UKAWA.
 
Paul Alex

Mimi binafsi nakushukuru kwa hilo ila kwa slaa naona wamechelewa sana maana hakuna mtanzania anaye msikikiza tena slaa
 
Last edited by a moderator:
CCM ndio watakaosababisha mchafuko nchi hii.
 
Nimeamini sasa ccm wanaelekea shimo la thewa
 
ok tumesikia... hiyo ya dr ni nzuri lakini ushindi wa ccm ni wazi bila hata mpango huo.
 
Ebu fikiria kidogo kaka.. Kwa suala la u first lady wapi utakapokosa likizo hata ikibidi isiyokuwa na malipo..

lakini akipanda jukwaani ,mtasema oh huyu mtumishi wa umma ,analipwa Na serikali why ashiriki siasa!!


lakini ni Wapi inaweza kuthibitishwa kama kweli amekataa?!

labda hana ule uwezo wa public speaking!!
 
CCM hawana sababu ya kufanya hvyo.Ile kuimanipulate M4C haıkuwa kuitumia km slogan.Unapokuwa kwenye jukwaa la siasa licha kukazana na wanaokuunga mkono,ni lazima ujitahdi kuwavuta wale wasıokuunga mkono.Km UKAWA hamna mtazo huo mmekwisha.
 
Nani atashinda Uchaguzi huu kati ya Lowasa na Magufuli?Ni kizunguzungu tupu.Bora uchaguzi upite.Uchaguzi wa mwaka huu ni Kipimo cha LIMUS kwa Tanzania
 
CCM hawana sababu ya kufanya hvyo.Ile kuimanipulate M4C haıkuwa kuitumia km slogan.Unapokuwa kwenye jukwaa la siasa licha kukazana na wanaokuunga mkono,ni lazima ujitahdi kuwavuta wale wasıokuunga mkono.Km UKAWA hamna mtazo huo mmekwisha.

Mnaenda kulala tulipoamkia halafu mnajiona wajanja?
 
Back
Top Bottom