Mbinu mpya Wanawake hutumia kuhalalisha ndoa...

muzi

JF-Expert Member
Jun 17, 2016
1,039
1,453
Maisha yamekuwa magumu sana siku hizi. Wanume suruali nao hawaoni haja ya kuoa kwa kuepuka majukumu yaliyo juu ya uwezo wao. Lakini kadri silu zinavyokwenda wadada wamekuwa warevu na wabunifu katika kutekeleza azma ya kuitwa mama fulani.....Hii yote ni katika kuwateka wanaume na ku-influence wakubalike na kushika himaya ya mwanaume.
Urafiki wa mwanaume na mwanamke huanza kimzaha, ikifika kipindi mwanamke ameshakuwa na uhakika kuwa mwanaume hana mchepuko mwingine zaidi yako au hata kama wapo lakini sio zaidi ya wawili hutafuta namna ya kukamta himaya. Zifuatazo ni baadhi ya tikitaka wanawawe hutumia kuhalalisha ndoa slowly
Siku ya kwanza atakuja na chupi 2, moja anaifua anaacha bafuni,nyingine anavaa asubuhi anaondoka…
Siku ya 2 anakuja na khanga,anaivaa usiku,asubuhi anaianika nyuma ya mlango anaondoka…

Siku ya 3 anasahau pete na hereni juu ya meza anakwambia ‘Hny nitunzie nimesahau hereni zangu mezani

Siku ya 4 anakuja na nguo 2 na vipedo vya kubadilisha na viatu pea 2,anavua high heels anaweka kwenye Shoe rack,asubuhi anaondoka na flat shoes kwenda chuo. Baada ya mwezi chumba chako kinakuwa na vitu kadha wa kadha,na ole wako uvihamishe alipoacha,kesi zinaanza…
Sasa kwa wanume wengine kuona chakula kipo mezani muda wowote anaotaka anajipakulia kwa kiasi anachotaka...ndo kwisha kabisa maana bibie ataweka manjonjo mpaka uwasahau wengine wote. Huduma za kufuliwa nguo, kupikiwa chakula MUBASHARA mwanaume kwishney habari yake.
Hao ndo Wanawake wa kileo,akija na begi zima si utamuuliza Vipi mwenzangu na utamkimbiza…Anahamia taratibu.. Mwisho wa siku dressing table yako iliyokuwa ina perfume na mafuta ya Rays inakuwa imejaa hereni na ‘Foundation’…


My Brother,huna haja ya kuuliza,NDO KASHAHAMIA HUYO….
Kifuatacho utaambiwa,”Honey I miss my days’,:D:D:D:D:D:D
Zamani nilijua ni simu za mkononi tu ndo zina missed calls, siku hizi kuna missed days,ukiambiwa hivi tu jua imekula kwako, inawindwa ndoa hapo

Ila kwa wanawake wenzangu inabidi ufanye hivi ukishajirishisha kuwa sio mume wa mtu......maaana mbeleni utaumia zaidi ya ulivyokuwa single. Hii ni kwasababu siku hizi mwanume kufanya kazi Mbeya na ameacha familia DAR imeshakuwa maisha ya kawaida sababu ya changamoto za ajira
Sorry wadada wezangu kwa kuliweka wazi hili ili ni kwa manufaa yetu sote katika harakati ya kupata mume unayempenda na sio wa kutafuta kiki na kuachwa mjane na mzigo wa kulelea watoto
 
Mbona rahisi sana kumsimisha hiyo tabia. Akiacha kanga Leo, kesho yake akikuambia anakuja, chukua ndoo, weka maji nusu, iingize hiyo kanga ndani ya ndoo.
Mpimie muda, ukiona bado dk3 aingie, anza kupiga deki kutumia hiyo kanga yake. hapo sijui nini kitafuata.
Akiacha chupi moja, wewe nenda kanunue chupi nyingine moja ya kike, kisha iweke pale alipoiacha chupi yake. Akikuuliza habari ya hiyo chupi asiyoijua, mjibu "ni yeye ndiyo aliyoziacha hizo chupi" Tena sisitiza hiyo uliyoinunua wewe ukimuona kaivaa huwa inampendeza sana!
Tumeambiwa tuishi nao kwa akili. yeye akilazimisha, sisi tunatumia akili.
 
Mbona rahisi sana kumsimisha hiyo tabia. Akiacha kanga Leo, kesho yake akikuambia anakuja, chukua ndoo, weka maji nusu, iingize hiyo kanga ndani ya ndoo.
Mpimie muda, ukiona bado dk3 aingie, anza kupiga deki kutumia hiyo kanga yake. hapo sijui nini kitafuata.
Akiacha chupi moja, wewe nenda kanunue chupi nyingine moja ya kike, kisha iweke pale alipoiacha chupi yake. Akikuuliza habari ya hiyo chupi asiyoijua, mjibu "ni yeye ndiyo aliyoziacha hizo chupi" Tena sisitiza hiyo uliyoinunua wewe ukimuona kaivaa huwa inampendeza sana!
Tumeambiwa tuishi nao kwa akili. yeye akilazimisha, sisi tunatumia akili.
Hahahahaha umenipa mbinu mkuu asante
 
Watakaokuelewa wachache,wengi wanapenda sifa za kuonekana wana vyumba vizuri,maisha ya juu(hata kama kaazima chumba)
Sio kila mwanamke unampeleka kwako haswa sisi wenye watt nyumbani unajaribu kutunza heshima utampeleka kwako kama umeshakuwa na malengo nae
 
Back
Top Bottom