Mbinu Chafu Vyuoni ni Kaburi la CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbinu Chafu Vyuoni ni Kaburi la CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lilombe, May 19, 2012.

 1. L

  Lilombe JF-Expert Member

  #1
  May 19, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 242
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM inaelekea kupotea miongoni mwa watanzania hiyo imethibitishwa na mbinu chafu wanazojaribu kuzitumia ili kunusuuru machoni mwa wasomi hatahivyo kazi ni pevu sana: hapa ni kielelezo cha ouvu wao uliposhindwa huko Iringa:-

  [TABLE="width: 879"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD] Mwanafunzi RUCO akamatwa  na Happiness Matanji, Iringa


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"][​IMG] [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] [TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD] Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Tumaini mkoani Iringa amekamatwa akijaribu kuvuruga uchaguzi wa serikali ya wanafunzi wa Chuo hicho Kikuu cha Ruaha (RUCO) unaofanyika leo chuoni hapo.

  mwanafunzi huyo, Sirion Kinunda, ambaye ni mwanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) alikamatwa majira ya saa nane usiku akibandika mabango ya kumchafua mgombea mmoja kati ya watu wanaowania kiti cha urais chuoni hapo.

  Imedaiwa kuwa usiku huo katika nyakati tofauti mwanafunzi huyo ambaye anadaiwa kuingia eneo la chuo kwa kuruka ukuta, alikamatwa na walinzi, na baada ya kuhojiwa kikamilifu akikiri kutumwa na watu wanaoaminika kuwa viongozi wa CCM mkoania hapa.
  Waziri wa ulinzi wa serikali ya RUCO, Benjamin Robert, alisema walimtilia mashaka mwanafunzi huyo, ndipo kamati ya ulinzi kwa kushirikiana na walinzi wa chuo hicho walimkamata akiwa na mabango ya kumchafua Rufiri William mwanafunzi wa elimu ya juu mwaka wa 2 anayewania kiti cha urais chuoni hapo.
  Akihojiwa na Tanzania Daima akiwa chini ya ulinzi chuoni hapo mwanafunzi huyo alisema kuwa aliagizwa na watu wawili mmoja wa mkoani Iringa na kigogo mwingine wa jijini Dar es Salaam ambao hata hivyo hakuwataja, kutekeleza mpango huo.
  “Mimi ninatekeleza agizo nililotumwa. Nimetumwa na viongozi wa CCM wawili mmoja wa hapa Iringa na mmoja ni kutoka Ofisi Kuu ya Dar es Salaam kuwa nifanye mbinu yoyote ili nimchafue mgombea wa kiti cha urais Rufiri William wakiwa wameniahidi kunipa donge nono,” alisema bila woga.
  Hata hivyo, hakuwa tayari kuwataja waliomtuma huku akisisitiza kuwa ni makada wa CCM.
  “Juu ya nani amenituma, siwezi kuwataja ila tu ujue kuwa ni makada wa CCM ambao mmoja ni wa hapa mkoani na mwingine ambaye ni wa ngazi ya juu yuko Dar,” alisema Kinunda.
  Mwanafunzi huyo alikutwa na kitambulisho cha chuo chenye namba (ID No) BSc.IT.07138 ambacho kitakwisha muda wake mwaka 2013, na kadi ya uanachama wa CCM yenye namba 3956641 iliyotolewa Februari 9, 2011, katika tawi la Chuo Kikuu cha Tumaini.
  Mwanafunzi huyo alifikishwa kituo cha polisi akiwa ndani ya gari namba T 311 AHR mali ya Chuo Kikuu cha Tumaini.

  Mkuu wa mkoa alipotafutwa ili kutoa maelezo juu ya mwingiliano wa kauli kwa Tume ya Uchaguzi katika chuo hicho, kuonekana kwa mwenyekiti wa CCM wilaya Abed Kiponza chuoni hapo akiwa kwenye ari T 422 BFE ambapo inadaiwa kuwa alipigwa na wanafunzi huku gari lake likivujwa vioo, hakupatikana ikidaiwa yuko kwenye mkutano wa halmashauri ya mkoa na hata alipopigiwa simu yake ya mkononi haikupatikana.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #2
  May 19, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,029
  Likes Received: 3,052
  Trophy Points: 280
  Hii nchi itakombolewa tu ama kwa kutaka ama kwa lazima .,Nnauye na fitina zake zitakwisha tu.
   
 3. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #3
  May 19, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  chama cha mapinduzi.
  jina halina maana,halina malengo,halina dira,halina mwelekeo na litakufa kifo cha aibu.
   
 4. p

  pomoni Member

  #4
  May 19, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  hivi kwanini wanalazimisha punda kunywa maji? waache demokrasia itawale, mambo ya kulazimisha yamepita muda wake kwa sasa, let them choose what they want and not what you want.
   
 5. j

  joely JF-Expert Member

  #5
  May 19, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 1,030
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  dogo badala ya kujisomea unaangaika kutumikia dead bodies.
  shukuru MUNGU ningekuwepo ningekupigia mwano wa mwizi
  RIP STUPID BOY
   
 6. majorbuyoya

  majorbuyoya JF-Expert Member

  #6
  May 19, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 1,815
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Malofa wapo wengi katika chama cha nyinyiemu. Huwezi kutumwa kufanya ujinga na wewe bila ya kushirikisha ubongo wako ukaenda kufanya eti kisa umetumwa na kiongozi wa nyinyiemu. Sioni thamani ya elimu yako ya chuo kama hata kufikiria uu ya vitu vidogo hivyo inakuwa tatizo.
   
 7. m

  makungas Member

  #7
  May 19, 2012
  Joined: Jul 23, 2011
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hilo lilianza muda lakini mpaka kufikia hapo,kweli watu wamemaanisha kuleta mabadiliko na hawataki ujinga.huyo kijana atakuwa ni wale wanaoahidiwa ukuu wa wilaya akidhani ni rahisi hivyo.mjinga kwelkweli
   
Loading...