Mbinguni ni wapi?

Sijabahatika kuona na wala sipati picha...!

Ni kitu gani ama nini hufuata baada ya Ndege (Aeroplane) kutanda juu ya Wingu...!

Nini hufuata juu yake..?

NB: Kwa walio bahatika kuona...
 
Mbingu na mbinguni ushajua tofauti yake ,nimkanganyo. Alafu watu hawana majibu wanasingizia mamb ya mungu hayachunguziki.
 
Mbingu za kwanza ni hapa duniani yaani jinsi unavyoishi ktk matendo mema yanayompendeza Mungu na watu wake hapo unakuwa na mbingu yako hapa duniani maana kwa kuwa mtakatifu basi unanafasi ya kushinda majaribu mengi, yanayoonekana tabu na shida kwa wenzio sio tatizo kwako.

Mbinguni halisi (kulingana na experience ya shuhuda za watu waliokwenda huko kwa muda) ni mbali na sayari yetu ya dunia...kumbuka sayari zinazoulikana (ziko nyingi tusizijua hadi sasa) zinaelea juu angani...huko kwingine ni ulimwenguni (universe) basi unapitalizaa weeeee unapandaa weeee mpaka mbinguni.

Tutende mema na kuwa watakatifu tutakutana huko siku moja
 
Mkuu mbinguni ni juu angani, ndio maana hata Yesu alipoenda mbinguni hakuingia chini ila alienda hukohuko Juu, tatizo ni hatujui ni umbali gani ila ukielekea huko juu siku utafika tu.

"Mbinguni na mahali popote duniani" hii inaonyesha kuwa mbinguni sio Duniani
 

Ni kina nani hao Mkuu walienda na wakarudi.???
 
Wengi sana pita Youtube andika heaven testimonies...haijalishi kuna uthibitisho au la...ila inakupa picha then ukichanganya zako na za kuambiwa.

Twaweza kupiga maombi pia kama huamini basi upate experience ya mbinguni au jehanam ikiwa litampendeza aliye juu ya vyote, Mungu.
 
Ulimwengu hauna juu wala chini.
 
Ulimwengu hauna juu wala chini.

Mkuu nipe tafsiri ya Juu na Chini ili twende sawa maana ake unaweza kuwa hata hujui maana zake.?? na kama unaamini Dunia ni tufe sababu zipi zinafanya ushindwe kutambua kuwa kuna Juu na Chini as long as sisi tunaishi nje ya Dunia.?
 
Mkuu nipe tafsiri ya Juu na Chini ili twende sawa maana ake unaweza kuwa hata hujui maana zake.?? na kama unaamini Dunia ni tufe sababu zipi zinafanya ushindwe kutambua kuwa kuna Juu na Chini as long as sisi tunaishi nje ya Dunia.?
Muuu ili ujue juu na chini ya kitu lazima uwe na point of reference asa kwa ulimwengu unavosema juu una refer kitu gani? ukishakuwa kwenye space pande zote ni sawa ingekuwa kuna juu kama unavofikiria wanasayansi wangetuaje mwezini si wangeanguka tena huku chini duniani.
 

Sasa mkuu reference si wewe mwenyewe. tunapo zungumzia Juu tuna maanisha Juu ya sisi binadam au chini ya sisi binadamu. kwahyo hata mawingu yako chini yako au upande upi?? Legeza kichwa kdgo utaelewa.
 
Kama Umbo la dunia ni duara tambarare, Biblia inatuambia Mbinguni ni hapa hapa tunapoishi wanadam wanyama maji na mimea na Mungu yupo juu ya anga yaani Angani,

kwanilivyoelewa ni kama tupo ndani ya nyumba moja na Mungu awepo darini.
Ila kama umbo la dunia ni hili la elimu ya darasani yaani duara mviringo, mbinguni ni sehem yakufikirika kwa kuwa juu hapajulikani ni wapi ama kuna nini maana muda huu juu ya watanzania inaweza kuwa ni kina cha wamarekani.

Zaidi naamini kupitia kitabu cha Biblia Mwanzo 1 mahali ilipo Mbingu pameoneshwa. Ni maharifa tuu tukitumia tutapajua!!
 
Sasa mkuu reference si wewe mwenyewe. tunapo zungumzia Juu tuna maanisha Juu ya sisi binadam au chini ya sisi binadamu. kwahyo hata mawingu yako chini yako au upande upi?? Legeza kichwa kdgo utaelewa.
Asa kwa akiri yako kidogo hunoi mtu aliye upande mwingine wa globe huko juu mbinguni kwangu si kutakuwa chini kuzimu kwake.
 
mbinguni ni wapi wananzengo?
 
Hujamuelewa mtoa mada anauliza kama mbingu haionekani au ipo kiroho kivipi Mnara wa babeli ulitaka kufika mbinguni yaani kama nimrod alitaka kufikia mbingu kwa jengo refu ila Mungu akazuia kwanini basi leo hii tuna marocket lakini hatufiki mbinguni??

Mbinguni na Mawinguni. Haya maneno watu wanayachanganya sana, ki ala ya utamshi yanalandana kwa mbali ila ni sehemu mbili tofauti. Mawingu au Mawinguni kila mtu timamu mwenye macho yanayoona anapajua kwa ile hali ya kupaona na kila siku tunapaona. Kivipi? Itazame anga, hali ya juu utakayoiona ipo katika hali ya maumbile ya moshi yanayoelea angani. Hayo ndiyo yanayoitwa mawingu na ndiyo taswira ambayo unayoizungumzia wewe kuhusu mnara wa babeli.

Kuhusu Mbinguni, huwa kuna shabihishwa na masuala ya imani. Kuhusu space na vilivyoma ndani yake, kama sayari,nyota, vimondo, galaxies n.k. Hapo bado haujaizungumzia Mbingu. Imani ya kiislamu ili ufike mbinguni utoke katika galexy yetu na si hizo tu, Bali galaxies zote unazozijua na usizozijua ambazo wanasayansi wanasema zipo zillions na zillions of galaxies. Baada ya hapo ndipo unafika mbingu ya kwanza. Kwa tafsiri nyengine ili ufike mbinguni kwa imani ya kiislamu, hii Space ambayo mwanadamu kwa upeo wake anasema haina mwanzo wala mwisho. Wala haina kusema hapa ndipo kulia na hapa ndipo kushoto. Kwa imani ya kiislamu uivuke hiyo space ndipo unafika pahala pengine, panapoitwa Mbinguni. Na nasema utapavuka kwa sababu hakuna sayari tena huko, wala hakuna mifumo tuliyoizoea kama ya kwenye anga yetu. Huko ni pengineko, huko ni Mbingu juu ya Mbingu. Hapo utapiga mahesabu mwenyewe ili ufike huko utatumia chombo chenye kasi gani na utatumia muda gani kufika huko.
 
Swai la anga lilotokea kwenye mada hii
 
Mimi najua ni wapi, ambatanisho niliweka linafana sana na ninavojua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…