Mbilinyi awataka Mbeya wasimtenge Mpesya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbilinyi awataka Mbeya wasimtenge Mpesya

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Dec 31, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Dec 31, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  MBUNGE wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu kama Mr II, amewataka wakazi jijini hapa kutomtenga mbunge wa zamani, Benson Mpesya kwa kuwa bado mchango wake wa mawazo unahitajika ili kufanikisha mikakati mbalimbali ya maendeleo.

  Mbilinyi alisema hayo katika mkutano wake wa kwanza tangu achaguliwe kushika wadhifa huo uliofanyika katika viwanja vya Soko la Sido Mwanjelwa ukilenga kuwashukuru wananchi.

  “Akiwa kama Mwanambeya, mchango wake wa mawazo unahitajika.Tena nawaomba huko mtaani mnapokutana naye msimzomee.

  Ana haki ya kupumzika kwa amani baada ya kututumikia kwa kipindi cha miaka kumi.

  Na ndugu zangu tutambue kuwa kipindi cha siasa kimepita sasa tunapaswa kushirikiana kupata mustakabali wa Mbeya yetu,” alisema Mbilinyi.

  Mbunge huyo ambaye pia ni gwiji la muziki wa kizazi kipya hapa nchini maarufu kama
  Bongoflava, aliwataka wananchi kutambua kuwa uamuzi wa wabunge wa Chadema kutoka nje siku Rais Jakaya Kikwete alipozindua Bunge hakukumaanisha wabunge hao hawamtambui Rais.

  Alidai lengo lilikuwa kutoa taarifa kwake kuwa mchakato uliotumika Katika uchaguzi mkuu uliopita haukubaliki na kudai mabadiliko ili kupata mchakato wa uchaguzi unaokubalika.

  Aliendelea kudai kuwa wengi walijaribu kupotosha kuwa wabunge hao hawamtambui Rais Kikwete lakini baadaye wakashindwa kuthibitisha ukweli wa maneno yao na hatimaye wakakubaliana na hoja ya kufanyika kwa mabadiliko hususani katika Katiba.

  Alisema kubadilishwa kwa Katiba ndiyo njia pekee ya kumaliza malalamiko yaliyopo nchini na kuiomba Serikali kulitafutia ufumbuzi suala hilo.

  Mbilinyi pia aliwashangaa watu wanaotajwa kujiandaa kukwamisha utendaji kazi wake ili aonekane hafai na anyimwe kura mwaka 2015 na kusema wanajidanganya wenyewe kwani hawana uhakika iwapo atagombea tena.

  “Nani kawaambia nataka kugombea tena? Mimi ni mbunge wa miaka mitano ya utekelezaji wa
  mikakati ya maendeleo itakayotekelezwa kwa nguvu ya umma,” alisema.

  Akizungumzia mikakati mbalimbali ya maendeleo, Mbilinyi alisema tayari amekutana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji, Juma Idd na Mkuu wa Mkoa, John Mwakipesile na kuanza kupanga namna ya kuitekeleza.

  Alisema kwa upande wa Mkuu wa Mkoa, wameanza na kuboresha ofisi ya mbunge, ili kuipa hadhi ya mwakilishi wa wananchi tofauti na ilivyo sasa ambapo inaweza kumkatisha mwananchi tamaa ya kutatuliwa shida zake.

  Mikakati aliyoipa kipaumbele ni pamoja na kuinua kipato cha wakazi jijini hapa kupitia sekta ya ufugaji samaki, kuboresha kilimo pamoja na kuhakikisha wafanyabiashara wadogo (machinga) hawanyanyaswi kwa kupigwa na kunyang’anywa bidhaa zao kabla ya kuoneshwa mahali pa kufanyia biashara zao
   
 2. k

  kituro Senior Member

  #2
  Dec 31, 2010
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 176
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Safi sana mbilinyi!. Angalizo isije ikawa nguvu ya soda!. Jitahidi inopowezekana shilikisha na wasomi ili mpange pamoja uchumi wa jimbo leno!.
   
Loading...