Mbeya: Walimu wakamatwa na TAKUKURU kwa kula rushwa za Tsh 500!

Filipo Lubua

JF-Expert Member
Nov 18, 2011
339
578
Wadau,

Nimeshtushwa sana na habari ya walimu wawili wa Shule ya Sekondari Forest, huko Mbeya kukamatwa na TAKUKURU kwa kuchukua rushwa ya shilingi 500 kwa wanafunzi waliochelewa (Mwananchi, 6 Feb. 2013).

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), mkoani Mbeya imewanasa walimu wawili wa Shule ya Sekondari ya Forest kwa tuhuma za kushawishi na kupokea rushwa ya kati ya Sh500 na Sh1,000 kwa wanafunzi wanaochelewa asubuhi.

Imeelezwa kwamba kutokana na mtindo huo, walimu hao wamekuwa wakijikusanyia wastani wa Sh150,000 kwa siku.

Walimu hao walikamatwa saa 8.30 mchana jana shuleni hapo baada ya baadhi ya wanafunzi kutoa taarifa Takukuru za kuwapo kwa tabia hiyo ya kulazimishwa kutoa fedha wanapokuwa wamechelewa kufika shuleni asubuhi.

Kamanda wa Takukuru wa Mkoa wa Mbeya, Daniel Mtuka, aliwaambia waandishi wa habari ofisini kwake kwamba walimu hao (majina tunayo), walitiwa mbaroni wakati wakiwatoza wanafunzi hao fedha hizo.

Hadi wanakamatwa, walimu hao walikutwa na kiasi cha Sh64,000 walizokuwa wamezikusanya kutoka kwa wanafunzi hao, huku pembeni kukiwa na rundo la fimbo lililokuwa likitumika kuwachapa.


Mtuka alisema waligundua kuwa walimu hao walikuwa wanatengeneza kiasi cha 150,000 kwa siku kutokana na wastani wa wanafunzi 300 waliokuwa wanawachapa. Shule hiyo ina wanafunzi 900.

"Walimu hao wamekuwa na mradi huo wa kuwalipisha wanafunzi na wanaoshindwa kulipa walikuwa wanachapwa viboko visivyokuwa na idadi," alisema na kuongeza:

"Kwanza walimu hao walikuwa wanachukua majina ya wanafunzi waliochelewa kutoka kwa walimu walioko zamu na kuanza kuwaita kwenye chumba walichokuwa wanakiita ‘Gwantanamo' na kutoza fedha hizo."

Walimu hao walichukua jina hilo kutoka Kambi ya Guantanamo Bay iliyoko karibu na Kisiwa cha Cuba, ambako Marekani imeweka kambi ya kijeshi.

Kambi hiyo ilianzishwa Januari, 2002 wakati Marekani ikiwa chini ya George Bush kwa ajili ya kuhifadhi mateka wa kivita kutoka Afghanistan na Iraq.

Kwa nyakati tofauti, wanafunzi walisimulia vituko vya walimu hao.

Mwanafunzi wa kidato cha kwanza, (jina tunalihifadhi), alisema kuwa mwanafunzi ambaye alikuwa hana fedha za kuwapatia, alikuwa anaambiwa kuweka kichwa chini, miguu na miguu juu kisha mwalimu huyo anamchapa kwenye makalio hadi sehemu unapopita uti wa mgongo.

"Baada ya kuona vitendo hivyo vinaendelea, huku uongozi wa shule ukiwa umekaa kimya, tukaamua kuwaambia viongozi wa serikali ya wanafunzi na ndiyo waliokwenda Takukuru," alisema.

Hata hivyo, Mkuu wa Shule hiyo, Cecilia Kakela alisema alikuwa hajawahi kuviona vitendo hivyo na alikuwa hajui lolote.

Alisema kuwa wanaendelea na mahojiano na walimu hao na baada ya hapo watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani.


Jamani, Tanzania imefikia hapa sasa? Au ndo ule msemo wa kila mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake? Au ule wa Biblia kuwa wa madhabahuni hulia madhabahuni?

Walimu hao wameona mahali pao nao pa kupatia "allowances''.


Mimi sina mengi ya kusema, lakini ngoja nione tuipelekapo hii nchi.
 
Huu mtindo wa kuwachukua failure kuwa Waalimu unaigharimu Nchi.
 
Takukukuru au********?
maana rushwa za mabilioni hawakamati wahusika, hata wakitajwa kwa majina na vielelezo vikiwepo.
Nakumbuka Kikwete alisema ana majina ya wala rushwa wakubwa, naona wakamshughulikia kabla hajawashughulikia.
Thats why takukuru inaona fahari kukamata wala rushwa wa sh, mia tano.
 
Takukukuru au*******/?
maana rushwa za mabilioni hawakamati wahusika, hata wakitajwa kwa majina na vielelezo vikiwepo.
Nakumbuka Kikwete alisema ana majina ya wala rushwa wakubwa, naona wakamshughulikia kabla hajawashughulikia.
Thats why takukuru inaona fahari kukamata wala rushwa wa sh, mia tano.


Nduguye, mbona tusi kubwa hivyo? Angalia wasitume maofisa wao kukuchunguza :)
 
Nduguye, mbona tusi kubwa hivyo? Angalia wasitume maofisa wao kukuchunguza :)
Lubua, tusi liko wapi> hebu andika neno M'kwere (kama linavyotamkwa, siokama nilivyo andika) ------ kisha post utaona matokeo yake.
sidhani kama nimemtusi mtu au nimemkwaza mtu. Nimeongelea madhaifu kuanzia kwenye top level
 
Lubua, tusi liko wapi> hebu andika neno M'kwere (kama linavyotamkwa, siokama nilivyo andika) ------ kisha post utaona matokeo yake.
sidhani kama nimemtusi mtu au nimemkwaza mtu. Nimeongelea madhaifu kuanzia kwenye top level

Haya kamanda, nshakuelewa. Nadhani litakuwa deshideshi tu kama ------ .... :)
Kanuni mpya za uandishi ni sharti zitumike hapo
 
Wanafiki wakubwa, rushwa kubwakubwa zinafanyika freely wao wanafumbwa macho. Rushwa iko idara zote nchini ila hawa jamaa wakaona watoke na walimu.. After all hivyo vijisenti havitoshi mgawo. Haya tuone kama kesi hii itapelekwa kwa DPP. Zakina Chenge ziko kwa DPP bwana. Hata hivyo siungi mkono walimu kupokea rushwa.
 
king'amuzi cha TAA..KUKUU kinanasa vidagaa tu hakina uwezo wa kunasa mapapa!
binafsi sioni kama tuna haja ya kuwa na TAA...KUKUU maana imezibwa kinywa na mafisadi!
 
Yuko mwl. mwingine pande za huku kwetu yeye huchukua kuku kwa wazazi/walezi kwa utoro wa watoto wao, mbona hawamkamati! Na jamaa anajiita kamanda wa operesheni wa kuchukua kuku za watu mtaani...!
 
Wakati watu wengine wakituhumiwa kuficha Mamilioni ya Dola Uswis na wengine kuwa na tuhuma za kifisadi za mabilioni {vijisenti}, Walimu wawili wamekamatwa na TAKUKURU huko Mbeya ktk Shule ya Sekondari Forest. Walimu hao inasemekana walikutwa wakipokea rushwa za shillingi 500 na 1000 toka kwa wanafunzi wachelewaji.

Hii inarejea kwenye ule msemo kuwa kila mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake. Polisi na bodaboda, mahakama na watuhumiwa, daktari na wagonjwa na sasa walimu nao (baadhi mf hao) wameona wawageuze mradi wanafunzi. Hii hali inasikitisha sn. Labda ni kutokana na hali ya kipato kwa walimu, lakini si jambo la kulifumbia macho.

Mwalimu anapaswa kuwa mfano mwema ktk jamii hasa kukemea maovu kwa watoto ili wapate jifunza toka kwao.

TUUNGANE KUKEMEA RUSHWA.
 
Unafikiri kazi ya takukuru ni nini? Ndio hiyo,,daktari mmoja kanda ya ziwa alishikwa na takukuru akipokea rushwa ya elfu 30 kaenda jela
 
Back
Top Bottom