Aman Mulagizi
Senior Member
- Jul 28, 2015
- 155
- 22
Kama mlivyoungana na Cuf mwanzo mliwaita mashoga nahskuna aliye wahi kukanusha sasa tujue nani shoga na nani basha?
Babu seya ni mojawapo ya wengi waliokosa Haki ambao wapo magerezani, mtashuhudia maajabu yakiwemo ya Balali kurejeshwa Tanzania, Magufuli kudaiwa zile billion 251 alizolipa makandarasi hewa pale wizara ya Ujenzi pia ukawa wataidai chenji ya vivuko Rada, vivuko, mabehewa Feki, sukari, bomba la Gesi, mgodi wa buzwagi, mgodi wa meremeta, escrow, EPA, chenji iliyobaki baada ya bunge la katiba iliyokataliwa nk
Hilo Gazeti ni la CCM ni gazeti mama la Uhuru ni sawa na ACT na CCM baba na mwana si Gazeti la kulisoma kabsa.
Kama mlivyoungana na Cuf mwanzo mliwaita mashoga nakuna aliye wahi kukanusha sasa tujue nani shoga na nani basha?
Bila kupoteza muda wala kuwachosha nimefanya utafiti kupitia mitandao ya kijamii kwa kuangalia watu 5,000 ambao wanaoinga mkono CCM. Hao ni wale ambao hawajatoka nje ya Tanzania hata kwenda tu nchi jirani na nyinginezo kuona ambavyo nchi nyingine zilivyopiga hatua.
Watu waliotembea nje na kuona nchi zilivyoendelea wengi hawaiungi CCM. Pia utafiti umegundua mikoa masikini zaidi ya Tanzania ndio bado wanaiunga mkono sababu wengi hawajatembea nje ya Tanzania kuona nchi nyingine zilivyopiga hatua hivyo wakiwekewa barabara ata ya udongo wao huona ndio maendeleo.
Wengi sana tunaichukia CCM tatizo ni kuwaleta hao Viongozi wa CCM kwenye chama chetu cha CHADEMA na kuwapa nyazifa kama Uraisi, UBunge na udiwani huu ni udhaifu mkubwa na unawapa credit CCM Wakati ndio waliotufikisha hapa leo tukiwa na maisha magumu.
Kwenye siasa njia zozote huwa zinatumika mkuu. Hakuna adui wala rafiki wa kudumu kwenye siasa, isipokuwa maslahi ya kudumu. Kutumia watu kutoka CCM sio shida mkuu. Ujue CCM sio chama cha siasa km unavyodhani, kile ni chama dola. Hata tungetumia watu wetu wenyewe isingekuwa kuwa rahisi kuishinda CCM. Ni wazoefu na wana mbinu nyingi za kushinda chaguzi. Huu ndio wkt mwafaka kwa kuwa sasa CCM imepasuka vipande vipande, hata km hawataki kukiri
kabisa. Mabadiliko tuliyokuwa tunayahitaji siyo ya huyu fisadi. Hana utashi wowote wa kuikomboa Tz kwani ni mtaalam wa ufisadi kwa muda mrefu. Na UKAWA wanajidanganya kuwa wataweza kumfundisha 'mbwa mzee mbinu za uwindaji'. Wamechemsha. Fisadi ni fisadi tu, na amebobea ktk hilo hawezi kuishi maisha ya tofauti. Sisi tunataka top awe na utashi wa kweli wa kupambana na mafisadi na kuinua uchumi wa wa-TZ. Sio eti "nachukia umaskini". Kwani mtu kuuchukia umaskini kunamfanya mwingine awe tajiri????!!. Cheap politics hizi tunapeleka wapi!!!! Hana uwezo wa kupambanua mambo, CDM tumejichanganya hatua za mwisho kumleta huyu fisadi. Tutakosa Ikulu na chama ameshakiua.
kabisa. Mabadiliko tuliyokuwa tunayahitaji siyo ya huyu fisadi. Hana utashi wowote wa kuikomboa Tz kwani ni mtaalam wa ufisadi kwa muda mrefu. Na UKAWA wanajidanganya kuwa wataweza kumfundisha 'mbwa mzee mbinu za uwindaji'. Wamechemsha. Fisadi ni fisadi tu, na amebobea ktk hilo hawezi kuishi maisha ya tofauti. Sisi tunataka top awe na utashi wa kweli wa kupambana na mafisadi na kuinua uchumi wa wa-TZ. Sio eti "nachukia umaskini". Kwani mtu kuuchukia umaskini kunamfanya mwingine awe tajiri????!!. Cheap politics hizi tunapeleka wapi!!!! Hana uwezo wa kupambanua mambo, CDM tumejichanganya hatua za mwisho kumleta huyu fisadi. Tutakosa Ikulu na chama ameshakiua.
- Chadema sasa wakwepa ajenda ya ufisadi
- Kauli ya kumwachia Babu Seya yashtua polisi
MKUTANO wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) uliofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Luanda jijini Mbeya wiki iliyopita, umeacha simulizi na mikanganyiko miongoni mwa wakazi wa jijini hapa.
Umati uliohudhuria mkutano huo umeacha simulizi kutokana na wingi wa watu wakiwa kutoka wilaya zote za Mkoa wa Mbeya, na wengine kutoka mikoa ya Rukwa, Iringa na Ruvuma.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, ujio wao ulikuwa mahsusi kwa ajili ya kutafuta wadhamini wa mgombea wao, Edward Lowassa, ambaye naye alihutubia mkutano huo kwa muda usiozidi dakika ishirini.
Hotuba ya mgombea huyo iliacha mkanganyiko pale alipotoa ahadi ya kumwachia mwanamuziki nguli wa dansi nchini, Nguza Vicking anayetumikia kifungo baada ya kukutwa na hatia, ikiwamo ya kuwanajisi watoto.
Baadhi ya watu waliokuwapo mkutanoni hawakusubiri kuitafakari ahadi ile baadaye, bali walianza mjadala muda ule ule, wakihoji mantiki ya ahadi ya mgombea huyo kumwachia huru mtu ambaye hata Mahakama ya Rufaa nchini ilimtia hatiani.
kumwachia Babu Seya tena, hii kali ya mwaka, wale majaji wa Mahakama ya Rufaa wako vizuri sana, asingekuwa na hatia wangemwachia,alisikika askari mmoja wa Jeshi la Polisi aliyekuwapo mkutanoni pale mara baada ya ahadi hiyo kutolewa.
Mbali ya ahadi hiyo yenye shaka kutoka kwa mgombea huyo wa Ukawa, ahadi yake hiyo, iwapo itatekelezwa, inatajwa kuwa ni sawa na uvurugaji wa utawala bora, lakini pia naye Mwenyekiti wa Chadema alifanya tukio lililodhihiri baadaye kuwa ni kituko cha aina yake.
Mbowe, kwa mbwembwe, aliwatangaza wanachama wapya waliojiunga na chama hicho siku hiyo ya mkutano, na miongoni mwao ni wabunge wawili waliomaliza muda wao, Mchungaji Luckson Mwanjale, Jimbo la Mbeya Vijijini na Modestus Kilufi, Jimbo la Mbarali. Wote wakiwa kutoka CCM.
Hata hivyo ni Kilufi pekee aliyejitokeza uwanjani pale na kutambulishwa, wakati Mwanjale aliitwa mara kadhaa na Mbowe pasipo kutokeza. Akiwatambulisha, Mwenyekiti huyo wa Chadema alisema; walipokuwa katika chama chao cha zamani walitufanyia nanihino, tuwapokee!
Mwenyekiti huyo aliitikiwa na umati uliokuwepo wakisema wapokee, lakini muda wote huo Mchungaji Mwanjale hakuwepo uwanjani hapo, hatua iliyosababisha Mbowe kutoa kauli nyingine tata akidai inawezekana mbunge huyo amechelewa kutokana na msongamano wa magari lakini angefika uwanjani hapo.
Kutokana na tukio hilo la kutangazwa na kutonekana, waandishi wa habari walianza kumtafuta Mwanjale ili kupata kauli yake na alipopatikana alionyesha kushangazwa na taarifa hizo za yeye kujiunga Chadema, akisema hajawahi kuwaza jambo hilo na kwamba asingeweza kujiunga na chama hicho kabla ya kushauriana na familia yake.
Katika mahojiano yake na Raia Mwema kwa njia ya simu, Mchungaji Mwanjale alisema kuwa wakati msafara wa Lowassa ukiwasili katika Uwanja wa Ndege Songwe, naye alikuwepo akiwa pamoja na jamaa zake na kwa sababu ni mtu wanayefahamiana alisalimiana naye.
Mchungaji Mwanjale anasema inawezekana lile tukio la yeye kusalimiana na Lowassa lilichukuliwa kimakosa na baadhi ya watu wakiwemo viongozi wa Chadema, kwamba kwao alikuwa amejiunga tayari na chama hicho. Makamo haya unaenda Chadema ili iwe nini, pamoja na makosa ya chama, wengine kutotendewa haki, sina mawazo ya kuhama chama, alisema Mwanjale.
Wakati mchungaji huyo akikanusha, baadhi ya wadau wa siasa za Mbeya nao wanahoji mantiki ya kiongozi mkuu wa Chadema kutangaza jambo ambalo hana uhakika nalo. Wanabainisha kuwa kama ni kweli hakukuwa na mawasiliano basi viongozi hao wanawakosea wenzao staha.
Wakati Mchungaji Mwanjale akitangazwa kwenye mkutano wa hadhara, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, John Mwakipesile naye alizushiwa kuhamia Chadema lakini katika kipindi kifupi kiongozi huyo alikanusha, akisema hajawahi kuwazia jambo hilo na kwamba bado yupo CCM na hajabadilika.
Kwa umri wetu huu, sio kuhama vyama, bali unampigia yule unayemuona anafaa na mwenye uwezo wa kutuongoza, anasema Mzee Mwakipesile katika mahojiano ya simu na mwandishi wetu, na kuongeza; Lowassa tunafahamiana na alikuwa kiongozi wangu, tumefanya naye kazi akiwa Waziri Mkuu mimi nikiwa Mkuu wa Mkoa, tulikuwa naye bungeni kwa miaka 10, inawezekana watu wanatumia vibaya uhusiano wetu huo.
Taarifa za kuhama kwa wanasiasa hao zilikuwepo kabla ya ujio wa Lowassa Mbeya, na wote, sababu kuu ya kuzushiwa ikiwa ni ukaribu wao na mgombea huyo wa Chadema. Tatizo Chadema wanatafuta watu wote waliokuwa jirani na Lowassa akiwa CCM, wanachanganya urafiki na itikadi, huo ni udhaifu mkubwa, anasema Charles Mwakipesile aliyekuwa miongoni mwa watangaza nia wa CCM na kushika nafasi ya tatu katika kuwania ubunge Jimbo la Mbeya Mjini.
Mwakipesile ambaye pia anashikilia nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya CCM anasema kuwa wanachama wenzao wanaokimbilia Chadema baada ya kushindwa kwenye kura za maoni wanadhihirisha umamluki wao walipokuwa ndani ya chama hicho.
Mtu amekuwa kiongozi wa miaka mitano, leo anaondoka baada ya kuanguka huku akitoa kashfa lukuki kwa chama kile kile alichokitumikia, ni udhaifu mkubwa, anasema Mwakipesile na kuongeza; .mimi nawaheshimu sana wanaohama bila ya msukumo wa kuanguka kwenye uchaguzi, hao ni wakomavu wa kisiasa.
Chanzo cha ndani, waliokuwapo Uwanja wa Ndege Songwe kumpokea Lowassa vinabainisha kilichojitokeza Mchungaji Mwanjali alipokwenda kumsalimia Lowassa ni utani uliokuwepo akihamasishwa kuhamia Chadema naye akajibu, tupo pamoja.
Chanzo hicho kinabainisha kuwa yawezekana Chadema walichukulia kauli ile kama jibu la kukubali kwa Mchungaji huyo kuhamia kwao. Katika kuthibitisha hilo, chanzo hicho kinasema ndio maana hata Mbowe alitoa kauli mbili, kwanza akisema yupo hapa, kwa maana ya mkutanoni na ilipobainika hayupo akasema inawezekana amekwama njiani kutokana na msongamano wa magari.
Katika mkutano huo walikuwepo viongozi mbalimbali wa vyama vinavyounda Ukawa akiwamo, Mgombea Mwenza katika urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Juma Duni, Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia na Dk. Emmanuel Makaidi.
Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi alikuwa miongoni mwa wazungumzaji katika mkutano huo, ambapo pamoja na mambo mengine alikituhumu Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuingiza mkoani humo shahada 5,000 za kupigia kura na kutishia akisema; wakijaribu kufunga goli la mkono tutatuma beki kuzuia, kule pembezoni akifunga tunakata kiganja kwa nyengo, mteule wa CCM kaingizwa bweni la zeluzelu.
Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia alimshauri Rais Jakaya Kikwete kuwa mtulivu na msikivu pamoja na chama chake katika kipindi hiki. Pamoja na ushari kwa Rais Kikwete, aliwasihi pia wananchi wa Mkoa wa Mbeya kuhubiri amani ili uchaguzi uwe wa amani pasipo kubaguana.
Hata hivyo Mwenyekiti Mwenza kwenye Ukawa, Freeman Mbowe alisema umoja huo hautapiga magoti kuwabembeleza Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) iwapo wataona wanaonewa bali watajibu kwa vitendo.
Ukawa hatutopiga magoti tukiona tunaonewa, tutachukua , akajibiwa na umati uliohudhuria action!
Pamoja na ahadi yake ya kumwachia Babu Seya iwapo ataingia madarakani, Lowassa pia aliahidi kulibadili Jiji la Mbeya na kuwa la kimataifa pamoja na Uwanja wa Ndege wa Songwe nao uwe wa kimataifa. Nao baadhi ya wasikilizaji katika mkutano huo wakasemezana wakihoji; kwani sasa sio wa kimataifa?
Katika jambo lililowashangaza baadhi ya wafuatiliaji wa siasa mkoani humo, ni hatua ya viongozi wa Ukawa kukwepa ajenda yao ya ufisadi, ajenda iliyowajenga na kuwapambanua kama viongozi makini wanaochukizwa na hali hiyo nchini ambayo imekuwa ikifichuliwa karibu kila mwaka na ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Katika mkutano wa Mbeya, sio Mbowe wala Mbatia au Makaidi aliyethubutu kutamka neno, fisadi au ufisadi. Hatua hiyo iliwafadhaisha baadhiya wapenzi wa mageuzi mkoani humo, wakibainisha kuwa wametelekezwa na viongozi wao.
Watu wamepoteza maisha, Mwalukali alipigwa risasi hapa na leo hii ana ulemavu wa mkono, tuliwaamini kuwa wanapigania haki, tukaingia barabarani, leo hii wamethamni pesa zaidi kuliko sisi, siasa chafu kabisa hizi, alisikika mkazi wa Soweto beya akilalamika
Chanzo: Raia Mwema Toleo la 419, 19 Aug 2015
Sasa km humpendi huyo chagua mabadiliko mengine kupitia CCM, pia viko vyama vingine vingi vina wagombea. Mimi sidhani km UFISADI wa CCM ni wa mtu mmoja mkuu. Tangu jamaa ajiuzulu Uwaziri Mkuu tumeshuhudia Ufisadi wa kutisha ndani ya mifumo ya CCM na serikali yake km Escrow hapo majuzi
Sasa ufisadi wa wengi usikufanye na wewe ubebe ufisadi wa mmoja wao halafu huyo mmoja amekija na watu wake ambao ni mafisadi mbaya zaidi wanakiuka hadi taratibu za kidemokrasia za chama mfano kumpitisha Msindai Jimbo la Singida Mjini wakati hakugombea hata kwenye KURA za maoni huoni kama ni tatizo? Naye Bu;laya Bunda hivyo hivyo halafu mnasema EL atabadilishwa na mfumo Akiwa Raisi wakati saa hizi kabla ya Uraisi anaanza kuharibu mfumo akiwa Raisi itawezekana . Namtakia kila la kheri EL ila baada ya Octoba tutaanza kusikia ufisadi wa ccm ndanui ya CDM maana EL 4U MOVEMENT NA FRIENDS OF LOWASA wamwekeza hela zao na nio lazima warudishe pesa zao. Yale ya JK tutashuhudia kwa EL. Tuombe uzima.