Uchaguzi 2020 Mbeya: TAKUKURU inamchunguza mpambe wa Sarah Sompo, mgombea Viti Maalum CCM kwa Rushwa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,983
ACHUNGUZWA NA TAKUKURU MKOA WA MBEYA

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Mbeya inamchunguza Bw ADAM HUSSEIN SIMBAYA wakala wa mgombea wa nafasi ya viti maalum UVCCM mkoa wa Mbeya kupitia wilaya ya Chunya Bi. SARAH JOEL SOMPO kwakosa la kushawishi baadhi ya wajumbe wa baraza za UVCCM mkoa wa Mbeya, kinyume na Kif cha 15 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya Mwaka 2007.

Wakala huyo alikamatwa jana tarehe 30/07/2020 katika ukumbi mdogo wa Mkapa akiwashawishi baadhi ya wajumbe ambao ni wapiga kura ili wampigie kura Bi SARAH kwa miadi ya kuwapatia fedha baada ya zoezi la uchaguzi kukamilika.Baada ya kumpekuwa alikutwa na fedha kiasi cha shilingi laki nane na elfu kumi (Tshs 810,000/=) pamoja na note book mbili zenye baadhi ya majina ya wajumbe.

Taarifa kamili itatolewa baada ya uchunguzi kukamilika.

WITO KWA WANANCHI
Tunawashukuru wananchi wa mkoa wa Mbeya kwa kuendelea kushirikiana na Taasisi yetu katika mapambano dhidi ya rushwa. Tunawaomba waendelee kuwasilisha taarifa za wale wote wanaojihusisha na vitendo vya rushwa kwa kupiga simu namba 113, kuandika ujumbe mfupi wa maneno kwenda namba 113 au kubonyeza *113# na kufuata maelekezo Huduma hizi zinapatikana BURE kwa mitandao yote ya simu.

IMETOLEWA NA:

JULIETH MATECHI

MKUU WA TAKUKURU MKOA WA MBEYA

31 JULAI, 2020
 
Ukishangaa ya filauni utayaona ya TAKUKURU unamchunguza mpambe ,unaacha kumchumguza mhusika mwenyewe? Ndiyo yaleyale ya kina Kigwangala na Gambo.
 
Back
Top Bottom