Sijatembelea Mbeya siku za karibuni lakini masoko ya Mbeya yamekithiri kwa uchafu na msongamano. Miaka michache iliyopita nilikuwa na tabia ya kwenda kununua ndizi kwenye lile soko lililoungua (Mwanjelwa?), kwa kweli kujua mahali ndizi zinapouzwa ilikuwa inabidi upelekwe na mtu ili kupita kwenye vichochoro vichafu ambavyo watu wawili wanapata shida sana kupishana. Ukitaka kutoka huko ndani tena ni lazima mtu akusindikize kukuonyesha barabara iliko.