Mbeya: Soko la Majengo laanza kujengwa

Mwanongwa

Senior Member
Feb 15, 2023
169
198
Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Dkt.Tulia Ackson na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo tarehe 01.07.2023 ameanza ujenzi wa kuwatengenezea soko wakazi wa Kata ya Majengo jijini Mbeya mara baada ya kusikia kero zao zilizokuwa zinawakabili wakazi wa kata.

Kwa mujibu wa msimamizi wa ujenzi wa soko hilo amesema mpaka kufika siku ya Alhamisi watakuwa wamepaua mabati.

Kwa upande wa Diwani wa kata hiyo Mhe. Maulid Jamadari amempongeza Mbunge kwa kujali wananchi wake kwa kuwajengea soko ambalo lilikuwa limechoka kutokana na uchakavu uliokuwepo pia ameiomba Halmashauri ya jiji hilo likatimize wajibu wake wa kujenga vibanda kama walivyokuwa wameahidiwa.
 
Back
Top Bottom