Makosa ya udhalilishaji na ukatili yaliyoripotiwa Februari 2023 hadi Machi 2023 Mkoani Mbeya jumla ni 284, yakiwemo ya 70 ya ubakaji na Ulawiti matukio 37.
Mchanganuo wa takwimu hizo ndani ya kipindi hicho, Makosa ya Ubakaji; Mbeya Jiji ni 70, Mbalizi (37), Chunya (77), Rungwe (33), Kyera (34) na Mbarali (33).
Makosa ya Ulawiti, Mbeya Jiji (20), Mbalizi (7), Chunya (0), Rungwe (4), Kyera (3), Mbarali (3).
Wizi wa Watoto; Mbeya Mjini (2), Mbalizi, Chunya, Rungwe, Kyera na Mbarali kote (0)
Makosa ya Kutupa Watoto; Mbeya Jiji (5), Kyera (2) kwingine kote hakukuwa na kesi hizo.
Mkuu wa Dawati la Jinsia Mkoa wa Mbeya, Loveness Mtemi amesema “Fikiria makosa yote hayo na hapo ni kesi zilizoripotiwa Polisi, kuna wengine hawajafika Polisi kuripoti, je, jamii yetu ipoje?
"Watoto wanabakwa, wanalawitiwa, mimi na wewe tusimame, tuone hili ni tatizo."