Mbeya: Mwanamke auawa kikatili

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,483
54,850
Mwanamke mmoja Mbeya auawa kikatili ,akutwa na kamba shingoni na majeraha makubwa ya moto.

Hali ya taharuki imewakumba wakazi wa eneo la Iwambi Block F jijini Mbeya kufuatia mauaji ya kikatili ya mwanamke mmoja yaliyofanyika usiku wa kuamkia leo ambapo mwanamke huyo amekutwa akiwa na majeraha, kamba shingoni jambo ambalo linaashiria kunyongwa na hatimaye kuchomwa moto na hivyo kuungua vibaya mwilini.

Wakazi wa eneo hilo ambao wamejitokeza kushuhudia tukio hilo wakizungumza na ITV wamesema kuwa kutokana na asili ya eneo hilo kuwa mbali na makazi ya watu matukio kama hayo yamekuwa yakitokea mara kwa mara hususani nyakati za usiku.

Mwenyekiti wa serikali za mitaa wa lumbira akizungumzia tukio hilo ameiomba serikali mkoani Mbeya kushinikiza watu ambao wamegawiwa viwanja katika eneo hilo kujenga haraka kwa sababu eneo hilo sasa hivi sio la mashamba tena na kuongeza kuwa matukio hayo yamekuwa ya kawaida kutokea mtaani kwake.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya Mohamed Mpinga amethibisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba jeshi hilo linafanya uchunguzi ili kuwabaini watu waliofanya tukio hilo la kusikitisha.

Chanzo: ITV
 
Visa vya kuogofya vinaendelea kutamalaki nchini. Eeeh mungu tusadie
 
Aisee inatisha
 
Poleni sana lakini hapo ndio muelewe kuwa huu ni uhalifu kama mwingine wowote sio ikitokea kwa watu flani baasi inakua maneno mingiiiii na ikikua kwa wengine maneno kindogooo
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom