Mbeya: Mwanafunzi mbaroni kwa kutupa kichanga chooni

Ketoka

JF-Expert Member
Sep 23, 2015
1,087
1,913
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia Mwanafunzi wa Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari Isengo, Ines Mtundu (19) kwa kosa la kumtupa chooni mtoto mchanga.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo tarehe 24 Septemba 2018 na Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, SACP Ulrich Matei, inaeleza kuwa, mtuhumiwa alitenda tukio hilo jana wakati akiwa chooni saa chache baada ya kujifungua.

“Tukio hilo limetokea mnamo tarehe 23.09.2018 majira ya saa 09:53 asubuhi huko maeneo ya Isengo – Airport ya zamani, Kata ya Iyela, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya. Inadaiwa kuwa mwanafunzi huyo alikuwa mjamzito na mara baada ya kujifungua chooni ndipo alimtupa mtoto huyo,” inaeleza taarifa ya Kamanda Matei.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa, mara baada ya taarifa kulifikia Jeshi la Polisi, jitihada za haraka zilifanyika kwa kushirikiana na Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji na kufanikiwa kumuokoa mtoto mchanga akiwa hai.

“Mama na mtoto huyo wote wapo Hospitali ya Wazazi – Meta wakipatiwa matibabu. Upelelezi unaendelea na mara baada ya kukamilika mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani,” ianeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Mwanahalisi
 
large.jpg
large.jpg
large.jpg
large.jpg
 
Condoms zinatangazwa kila siku lakini bado watu wanapata mimba...
ila nasikitika pia, huenda alishawishiwa kwa nguvu na njemba, au kiburi chake mwenyewe kujifanya anajua.

ushauri wangu aachiwe huru akalee mtoto wake tu.
 
Huyo katupa ama kazalia chooni?

Natumaini hiyo ilikuwa ni mimba yake ya kwanza.

Wanawake wengi kitendo cha kujifungua huhisi kwenda haja.

Huyo badala ya kumhukumu, ingefaa asaidiwe tu.

Mauzauza ya mimba ya kwanza na ile hali ya uanafunzi ni changsmoto.
 
Condoms zinatangazwa kila siku lakini bado watu wanapata mimba...
ila nasikitika pia, huenda alishawishiwa kwa nguvu na njemba, au kiburi chake mwenyewe kujifanya anajua.

ushauri wangu aachiwe huru akalee mtoto wake tu.
Condom kuziona, kuziongelea na kuzi like ni rahisi.

Lakini kuzitumia ni vigumu sana, sawa na ngamia kupita kwenye tundu la sindano.

Condom zipo, lakini idadi ya mimba zisizotarajiwa pamoja na population density ya raia pamoja na ukimwi vinazidi tu kuongezeka.

Sazingine hata wewe mkuu unayezitajataja condom hapa, huenda haupendi hata matumizi yake, au huzificha ama kuzichomoa katikati ya 'game' ili ku fulfil kiu yako.

Condom huvaliwa kwa jazba kwa kujua kabisa unaenda kujichochea kwa malaya, hivyo usipoteze vyote viwili, pesa na roho yako.
Vinginevyo nyama halisi ya binadamu isiyokinai inaliwa kavukavu.
 
Condoms zinatangazwa kila siku lakini bado watu wanapata mimba...
ila nasikitika pia, huenda alishawishiwa kwa nguvu na njemba, au kiburi chake mwenyewe kujifanya anajua.

ushauri wangu aachiwe huru akalee mtoto wake tu.
Condom si kinga ya ukimwi tu au Na mimba pia? Siku zote nilikua nasema hili lengo la kondom ni mimba wala sio ukimwi shida yao tusizaane tu
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia Mwanafunzi wa Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari Isengo, Ines Mtundu (19) kwa kosa la kumtupa chooni mtoto mchanga.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo tarehe 24 Septemba 2018 na Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, SACP Ulrich Matei, inaeleza kuwa, mtuhumiwa alitenda tukio hilo jana wakati akiwa chooni saa chache baada ya kujifungua.

“Tukio hilo limetokea mnamo tarehe 23.09.2018 majira ya saa 09:53 asubuhi huko maeneo ya Isengo – Airport ya zamani, Kata ya Iyela, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya. Inadaiwa kuwa mwanafunzi huyo alikuwa mjamzito na mara baada ya kujifungua chooni ndipo alimtupa mtoto huyo,” inaeleza taarifa ya Kamanda Matei.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa, mara baada ya taarifa kulifikia Jeshi la Polisi, jitihada za haraka zilifanyika kwa kushirikiana na Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji na kufanikiwa kumuokoa mtoto mchanga akiwa hai.

“Mama na mtoto huyo wote wapo Hospitali ya Wazazi – Meta wakipatiwa matibabu. Upelelezi unaendelea na mara baada ya kukamilika mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani,” ianeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Mwanahalisi
Ana ujasiri, kqjikamua mwenyewe!
 
Back
Top Bottom