Mbeya: Mtaa wa Uzunguni ni mzuri sana

Mbeya: Mtaa wa Uzunguni ni mzuri sana

Traxtion

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2021
Posts
5,894
Reaction score
11,782
Mbeya licha ya kuwa na mitaa mingi iliyojengwa hovyo bila mpangilio, lakini mtaa wa Uzunguni ni mzuri sana
Uzunguni kumepangiliwa vizuri, kuna miti mingi, hata hali ya hewa ya utofauti, na majengo yameachiana space, kati ya jengo moja na lingine. Uzunguni ni mtaa ambao upo kimya sana, kiasi kwamba hadi sauti za ndege wakiimba unazisikia. Pako kimya sana na hakuna watu wengi, unaweza kutembea dakika 10 usikutane na mtu njiani

Hakika natamani Tanzania iwe na mitaa mingi ya namna hii

Picha za Uzunguni
PXL_20251214_170314787.jpg
PXL_20251214_170641730.jpg
PXL_20251214_170536851.jpg
PXL_20251214_170800297.jpg
PXL_20251214_170624606.jpg
PXL_20251214_170803623.jpg
PXL_20251214_170947187.jpg
PXL_20251214_171127548.jpg
PXL_20251214_171215759.jpg
PXL_20251214_171323507.jpg
PXL_20251214_171305309.jpg
PXL_20251214_171438936.jpg
PXL_20251214_171419309.jpg
PXL_20251214_171557157.jpg
PXL_20251214_171708945.jpg
PXL_20251214_171745838.jpg
PXL_20251214_171802573.jpg
 
Mbeya ni kuzuri tatizo polisi waleviwalevi wa hapo hawachelewi kukupa kesi na wanakufunga kweli mambuzi zao. Ndio sababu watu tuliotoka Dar hatuwezi kukita mapande kama hayo kwa muda mrefu
 
ramani za Mkoloni hizo, Za kwetu ni zile za mabatini na Kabwe
Pia Iwambi kuna mtaa mpya unaitwa Maziwa. Huku ni ramani zetu Wabongo wenyewe na kumepangiliwa vizuri pia, papo kimya na panajengeka kwa kasi. Nyumba za watu wa Maziwa ni nzuri sana. Siku ikitokea nikiwa free tena nitaenda kupapiga picha.
Japo nakubali mitaa mingi tumeipanga hovyo
 
Mbeya ni kuzuri tatizo polisi waleviwalevi wa hapo hawachelewi kukupa kesi na wanakufunga kweli mambuzi zao. Ndio sababu watu tuliotoka Dar hatuwezi kukita mapande kama hayo kwa muda mrefu
😂😂😂 Yani mapolisi wanakupa kesi bila sababu yoyote au? Kama wanafanya hivyo basi inapaswa wajirekebishe kwa kweli
 
😂😂😂 Yani mapolisi wanakupa kesi bila sababu yoyote au? Kama wanafanya hivyo basi inapaswa wajirekebishe kwa kweli

Bro nilikaa pale mwaka mmoja ikabidi nile kona tu maana niliona manjago wakishapiga mitungi wanajiona wako juu ya sheria na sisi wazawa wa Dar huwa hatutishiwi nyau
 
Bro nilikaa pale mwaka mmoja ikabidi nile kona tu maana niliona manjago wakishapiga mitungi wanajiona wako juu ya sheria na sisi wazawa wa Dar huwa hatutishiwi nyau
Hii nchi police wanapenda kujiona wako juu ya sheria
 
Back
Top Bottom