Mbeya Mjini; Kweli Sugu ni Mtetezi Wenu na Watanzania Wengine

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,797
71,217
Niliposikia tamko la Waziri wa Afya kuwa sasa hivi hakuna tena Hospitali za serikali kuzuia maiti za Watanzania ambao wamefariki na kuacha madeni nikamkumbuka mbunge wa Mbeya Mjini.

Hakika mbunge huyu ambaye kuna figisu zinafanyika kumtoa ili kumuingiza mama mmoja kwa njama ni hazina kubwa sana na sidhani kama watu wa Mbeya watakubali hadaa hiyo.

Watapambana kulinda jimbo lao kuwekwa mtu kwa manufaa ya viongozi na sio manufaa yao.

Alilianzisha kwa style yake kama ya hip hop lakini hatimae limekuwa faida kwa wengi wanaofiwa na hawana uwezo. Msikilizeni hapa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
View attachment 1358419

Sent using Jamii Forums mobile app
FB_IMG_1581680945651.jpg
 
Hapa Mbeya tumeshampitisha Tulia Akson awe mbunge wetu, Sugu atafute kazi nyingine, au ajikite kuendesha hoteli yake asijekushindwa kurejesha mkopo wa CRDB

Makamu wa Rais Mama Samia na hata Katibu Mkuu na Makamu Mwenyekiti CCM ( Bara ) wameshaonya sana tabia ya wana CCM kuanza Kampeni mapema kabla ya muda muafaka je, Wewe na wana CCM Wenzako wa hapo Mbeya mlikaa na Kukubaliana hili lini? Na je, lina baraka za Viongozi Waandamizi wa CCM? Kuna Wapuuzi wachache mnafanya wana CCM wote waonekane Wapuuzi wakati kumbe si kweli na wapo wana CCM ambao wanajitambua na wana Maadili yao mazuri tu.
 
Mbeya hata CCM wasipotumia nguvu, mbunge hatatokana na wapinzani. Sugu kachokwa. Hakuna chochote kafanya zaidi ya kuwakimbiza na miradi ya maendeleo.
 
Mbeya hata CCM wasipotumia nguvu, mbunge hatatokana na wapinzani. Sugu kachokwa. Hakuna chochote kafanya zaidi ya kuwakimbiza na miradi ya maendeleo.
Inawezekana kwa muono wako mwanaccm, lakini jee kuhusu hili la serikali kuzuia maiti eti kuna madeni wewe unalionaje? Kapigania jambo la maana hadi serikali imeliona au halina maana?
Hospitali watu wana peleka mgonjwa wao akapone sio kufa sasa inakuwaje afe kisha ing'ang'aniwe maiti?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom