Mbeya: Matambiko ya Wazee ya kuzia ajali yanaendelea

Mbeya: Matambiko ya Wazee ya kuzia ajali yanaendelea

Tatizo la Mbeya ni milima na miteremko mikali yaani ukitoka mbeya kwenda Dar pana huo mteremko mkari wa mlima nyoka, Mbeya kwenda chunya/ Tabora ni mlima mkari na inasemwa barabara hiyo ndio iko juu zaidi kutoka usawa wa bahari hapa nchini, Mbeya kwenda Tunduma/Zambia ni miteremko mikali ikiwemo huo wa mbalizi ulioua watu 20 hapa juzi juzi na pia Mbeya kwenda Tukuyu hadi Malawi ni huo mlima igawilo ambapo hivi juzi watu watano walikufa pale. Sasa badala ya kutafuta njia za kisayansi wanaenda kwenye matambiko. Ukifika katikati ya jiji barabara ni finyu na ndio barabara kuu. Cha kushangaza magari yote ikiwemo maroli, daladala, bajaji, mikokoteni vyote vinapita humo. Matambiko bila suluhisho la barabara ni kazi bure.
 
Back
Top Bottom