Mbeya : mama afukua kaburi la mwanae

ipatama

JF-Expert Member
Jun 16, 2016
348
228
Katika hali isiyo ya kawaida mama mmoja mwenyeji wa mkoa huu wa mbeya mji mdogo wa mbalizi, usiku wa kuamkia leo alienda kaburini alikokua kafukiwa mwanae aliyefariki dunia Siku ya jumatatu na kuzikwa jumanne ya wiki Hii na kufukua kaburi hilo na kuitoa maiti

Kwa mujibu wa mama huyo maarufu Kama mama vumi anadai aliambiwa na mchungaji kuwa mwanae hajafa Bali Kuna sehemu anafanya kazi hivo aende akaitoe ile maiti kaburini ili iombewe irudi kuwa binadam wa kawaida,

Jana usiku yule mama ndio akaenda kuifanya kazi aliyotumwa na mchungaji wake ambapo leo asubuhi ndio raia wakagundua ishu na kwenda kukinukisha kwa yule mama, polisi walifika eneo la tukio na kumuokoa yule mama toka kwenye mikono ya wananchi wenye hasira Kali na kuondoka nae pamoja na maiti ya mtoto
 
Duh, nimetoka kwenye ban, japo sijaambiwa ni kwa sababu gani lkn ni comment kuwa sisi wakristo ni wajinga sana. Kuna jamaa alinilalamikia kuwa siheshimu imani za watu.

Sasa imani ya huyu mama na mchungaji wake, naanzanje kuiheshimu?

Im sorry wahusika.
 
Hao raia vipi? walipaswa wakakinukishe kwa huyo mchungaji kwanza na kumtia nakoz za nguvu kabla ya huyo mama....Poleni wafiwa...
 
Mbona mchungaji hajamsindikiza??? Siku hizi kwa kweli makanisani hasa ya kisasa yanashida sana. Kila kukicha wachungaji wanaibuka na mapya na wanajua sana kucheza na akili za waumini wao na hali ya maisha ya kila siku anayokabiliana nayo mwanadamu. "kweli watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa" na kinamama wanajitahidi jmn huko makanisani. Kuna mtumishi mmoja niliwahi kumsikia akisema siku parapanda ikilia km ni asubuhi/mchana itawakuta kina mama wengi sana wako manjiani wanahaha hawajui wakasali dhehebu gani maana kutwa kuzunguka na makanisa sijui ni Mungu yupi wanayemtafuta.
 
Wakristo sio wajinga huyo mama ndo mjinga hv wnaopsema sumbawanga n wachawi inamaana wote n wachawi? la hasha. So think clear
 
Back
Top Bottom