Mbeya long time kitambo

Kulikuwa na kucheza madoyomba, kudaka Magh'ela kuna yanayouma tulikuwa tunayaita polisi(yalikuwa na rangi nyeupe na nyeusi) yale mekundu tulikuwa tunaamini hayaumi lakini sometimes unajichanganya unajikuta unapigwa mishale ya maana
 
Duh, hakika bujibuji unaijua Mbeya! Umenikumbusha mbali sana. Enzi hizo nachezea timu ya Black Town then nikahamia Jogoo basha zote za Br ya 3.Zote ligi Ilikuwa kiwanja ngoma.
Pia namkumbuka Dr. Kasimbazi alikuwa na gonna lake pale Friends Corner bar, hatareee. Mzëe akishalewa anatoka machafu na gari yake Toyota datsun single cabin huyoo anarudi zake rufaa hospital kazini kwake. Mchana kweupee keshalewa.
Wale wavuta petrol Walikuwa ndugu 3,walikuwa balaa wakishavuta. Mjini sokomatola na mtaani kwao karibu na uwanja ngoma hakukaliki. Walikuwa na misauti minene balaa!Duh,mleta post hii umenikumbusha mbali sana.
 
Nonde Machinjioni
Huyo pusher alijulikana kwa jina la Mwasimba aka Shetani. Alimuoa dada mmoja anaitwa Christina Waya. Huyu dada alikuwa classmate wangu Itiji primary school miaka ya 1987-90 alipompatia mimba na kukatisha masomo darasa la 4. Akamchukua Jumla na kuwa Mkewe. Jamaa alikuwa mbabe balaa hadi polisi Walikuwa wanapata wakati mgumu kumkamata kwa biashara yake ya bangi mitaa ya Nonde.
 
Bujibuji ni Dokta Harison Mwakyembe chunguzeni mtaniambia
😀😀😀😀😀😀😀 nouma sana yani kabudi naye ndani huu mtandao never die i love mbeya first time 2013 july
 
Jiwegangi kwa miaka hiyo Itiji bila shaka walimu wafutao utakuwa unawakumbuka vizuri Bwalya, Mwakajila, Ndowa, Kyusa, Kalinga, Manase, Mwanakaya n.k.
 
Na Bob Edgar
Mi si wa mbeya ila nilisoma mbeya, Bujii umewasahau na MTC ? Wale wanachuo wakorofi?
 
Hapo jirani na kwenu, kwa kina Makolija walikuwa na Linolino hapo kwa kina Max Nanyaro walikuwa na Nishio
Makunguru zilikuwepo daladala za mama Monica aliziandika"nashangaa gari" rout ni standkuu to uyole
 
hakika unaifaham mbeya na watu wake....mimi miaka hyo nilikuwa natafutia riziki pale iringa/makambako na kuna muda nilifata mizigo ama kupeleka bidhaa kwenda mbeya kwa kwel ilikuwa mbeya kweli.......
Mtoa uzi nimemkubali sana , nilifika mbeya kwa mara ya kwanza nikiwa kijana miaka ya tisini. Then kuanzia mwaka 2009 nikarudi rasmi kama mwajiriwa kwa kuhamishiwa huku mpaka leo na makazi yangu ni uyole njia panda. Amenipa historia nzuri sana ya Mbeya na mengi nilikuwa siyafahamu. Hongera sana kwa mtoa mada.
 
Bujibuji ukifika Mbeya tuwasiliane, nina miaka saba sasa na nimekukubali sana, ninajua bahadhi ya vitu ila ulivyoongea ni kumbukumbuku tosha kwa bahadi yetu sisi wakuja hapa. Ila wababe na wachakarikaji bado wapo na Jiji linasonga mbele. Fursa bado zipo nyingi kwa upande wa kilimo
 
Kulikuwa na watoto fulani wa Ilolo walikuwa mapacha wanasoma Mbeya Day miaka 1996 to 1999 hakika walikuwa wakali
 
Pale Sangu Sekondari ...kwenye miti kulikuwa na kichaka kinaitwa kaburi la Bob Marley watu wamekula sana ganja pale....lkn leo hii baadhi yao ni watu wakubwa sana hapa chini ya jua......
nimefursiku hizi utakwenda
Disco mount Livingston tulikua tunaita "shimoni" umaarufu ulipungua baada ya kufungua Royal pamodz
Nimeipenda avatar yako na imenikumbusha hiyo picha ya mhusika mkuu wa picha moja ya kinaijera ikiitwa AGUMBA. Karibu sana Mbeya mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…