Mbeya long time kitambo



NAMBA 13. Ndiyo inathibitisha Mbeya unayozungumzia sio ya ZAMANI!! ,Zamani SOKOINE STADIUM uliitwa MAPINDUZI STADIUM na bado zamani MAPINDUZI haukuwepo pale kulikuwa na miti, pembeni kulikuwa na uwanja mdogo mzuri sisi watoto wa wakati huo tukicheza chandimu. Vichaa alikuwepo PRISON aka UGUMBA HUYO BALAA ! Alikuwepo ALOYCE kazi yake kuimba hana ugomvi na mtu, alikuwepo KANJINGALA anatembea akigonga chuma huku akicheza na kunengua kiuno !!! wengine kina Mwakityaka, Marry nk. lakini Bujibuji usijali inawezekana zamani hiyo unayoizungumzia inalingana na kipindi ulicho kuwepo !! AMANI IWE NASI !
 
Prison alikuwa Na miguu mmoja mfupi kidogo, ana shabaha sana ya mawe.
Uwanja wa mapinduzi ulijengwa na Kila mtu hata wafungwa walishiriki ujenzi.
Kabla hapajawa na uwanja, palikuwa na uwanja wa golf wa Mbeya Club.
Tatizo ni kwamba history was not written, tuendelelee kuandika historia kwa ajili ya kizazi kijacho
 
Mwasimba was nonde ndo alikuwa founder was kuuza bangi na alikuwa mtemi balsa had I mapolisi walikuwa wanachezea vichapo kama kawa!
 
Sahihi Bujibuji tuendelee kukumbushana naamini mungu akijalia tilukijaona onana WOTE tutasema aaah kumbe wewe!!!
 
Kullikuwa na Mama Mmoja Kichaa pale Sokoni wahuni walikuwa wanamdandia Usiku akitoka matembezini...Kuna siku moja Usiku wa kama saa nne hivi nilimkuta Njemba moja limemkunja huyu Mama wa watu pale karibu na Uwanja wa Sokoine nyuma kidogo ya Shule ya sisimba!!!Mama wa watu alukuwa katulia tu...
 
Aiiiiii mamaaaaa nakufaaaaaa, Piere Liquid atapaki kuwa juu
 
Mbeya city mimi nakumbuka ligi ya magari ya kwenda Tunduma kipindi hicho ni hiace ndio zilizotawala. Hiace zilizotamba sana kwa mbio zilikuwa ni Bambucha,Umeme, High Bury, Loita, Mkulu na Mwambambe.

Kuna hiace ilikuwa inaitwa Bambucha kutoka Soko Matola hii ilikuwa inaendeshwa na kaka mkubwa Andrea.

Huyu alikuwa mbabe alipokuwa akifika stend kuuu wahuni wote walikuwa wanakimbia huyu alikuwa mbabe haswa vijana wa Soko matola mpaka Stendi walikuwa wakimuogopa.
 
Daa!! Nonde bwana- machinjioni. Ajira ya vijana wengi. Nyama choma kwa matoki kwa wingiii!! Daaa!!! Mimi kwangu miaka ya 1973 na kuendelea. Nimesoma Mbeya day. Kimpumu original, ubwala bwa misi, Majengo bwana na Ghana!! Acha tu.
 
Nimekaa mbeya 1995 mpaka 1997 Nilikuwa nakaa sokomataloa kalibu na kiwanja mpaka au Olofea,Nilikuwa na Duka langu pale lilikuwa linagonga Reggae sana walikuwa wanapaita kwa Marasta. Ndipo nilipojuana na Ngwisa alikuwa Jamaa Yangu sana.Hata lile sakata la polisi kupiga mabomu Nyumbani kwao nilikuwepo.na kulikuwa na Jamaa mmoja anaitwa BEST au Ipiyana alikuwa anajua sana miziki ya reggea sijui mzima,baadaye nikawa na Duka jingine Rejco kalibu na nonde hapo ndipo nilipojuana na Mwasimba naye alikuwa anakuja kusikiliza reggae,nimeangalia sana Video magorofani
 
Umesahau Mabati kiwanda cha miwa na vitindi , Kilabu cha Mwakyela pale Nonde , Kilabu cha Maendeleo kule Ghana juu , Kwa Mwalalika mashine maarufu ya kukoboa mpunga , Mtemi Mwasimba bangi zikipanda anaenda milima ya Nonde kupandisha Bendera yake alafu ikifika saa sita usiku anaenda kuishusha , Mbeya kuna makaburi maarufu ya Sabasaba na Nonde , Pombe maarufu ni Chimpumu ukinywa leo yakibaki machicha kesha unachemsha maji alafu unamimina mziki unaendelea kwa kutumia mlija unaitwa mkenge , Kilabu Maarufu kutoka kwa mkoloni kilitwa REGCO pembeni kulikua na soko Maarufu liliitwa Soko la Majengo , ukicha shule ya Sisimba na Azimia huku Majengo kulikuwa na shule ya Majengo na ghana kuna shule ya Mbata , matunda ya mbeya masasati , mbulu , numbu , katapela , mang'ang'a, fyulisi , ..... vitongoji maarufu ni Nonde , ghana , majengo , Uhindini , Kwa Mama John, Mwanjelwa a.k.a Njelii , vilio msibani si mchezo .....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…