Mbeya imepotea na Mark Mwandosya?

Kweli mkuu
Sera ya kubinafsisha viwanda vya Mwalimu na kuwapa matapeli huu ndio mfano wake mbaya.
Matapeli wanaoendesha kiwanda hicho wanawakamua wananchi mpaka wengine wanajitoa kuendeleza chai.
 
Katika swala la kusuasua kwa maendeleo ya nchi hii na sio Mbeya tu sababu kubwa ni mosi,ccm na sera zake ziliyofeli.Pili ni ubinafsi uliowajaa viongozi wa ccm na siasa zao za maji taka.Viongozi wa ccm hawataki kushirikiana na wapinzani kuleta maendeleo na hili wamekuwa wakilifanya kama mkakati wao wa kisiasa.Serikali kuu imekuwa ikizuia ama kuchelewesha miradi mikubwa katika maeneo yaliyo na upinzani.Sasa cha kujiuliza ni kuwa wanamkomoa nani na sisi wananchi tumulaumu nani? je tumlaumu mbunge anayepigania maendeleo yetu na akakwamishwa kwa wazi kabisa na serikali kuu ya ccm au tuilaumu na kuichukia serikali ya ccm inayokwamisha na kuzuia maendeleo kwa sababu ya siasa za maji taka? Wenye akili tunaelewa nini cha kufanya
 
Hoja yako imepotezwa na ubaguzi wako wa kikanda na kidini. Kwa taarifa yako Mimi naishi na kufanya kazi wilaya ya Magu. Kwa kilichotokea uchaguzi wa 2015 mikoa yenu ya usukumani hakipishani na chuki uijengayo hapa. Bukoba na Mara kwani sio kanda ya Ziwa? Mbona walichagua upinzani kwa kishindo?

Ktk mikoa ambayo wapiga kura ni duni kifikra(hasa elimu ya uraia) ni hiyo mikoa uliyoitaja. Vibiriti, Chumvi ndio vilikua bora kwenu. CCM kwangu sina imani nayo hata kidogo and napigia chapuo Mbeya upinzani uchaguliwe ili serikali yenu itambue.

Tangu enzi za Nyerere serikali imekua ikiitenda mbeya isivyo. Rejea Nyerere kumuweka John Mwakangale(Mungu amrehemu) ambaye shule ilikua tatizo almradi tu afanikishe malengo yake kisiasa. Njoo kwa kwa Kikwete na picha yake na John Mwakipesile utaelewa.

Mbeya watu wake hata wawe duni kiasi gani visasi wanajua kuvifuga na hawasahau. Huyu bwana wa Ss no wonder siku akienda huko labda afanye makubwa yatayowapooza watu dhidi ya kutengwa na serrikali watamuelewa.
 
Mkuu mabadiliko hutokea baada ya mmoja kufanya makosa makosa ya ccm ndo faida kwa chadema nao chadema wakifanya makosa tunaweza kushuhudia chama kingne kikiweka ngome
 
Achia tu hao wapinzani wapindue sugu ataung'arisha kama walivyoona inafaa na kwetu pia inafaa tu!kwani mby nini bana.
Mbeya nini, sumu ishasambaa Njombe, Iringa na Ruvuma, maneno yenu yanazalisha kanda nyingine itakayowasumbua bila kujua muendelee kuropoka tu bila kutumia busara
 
masopakyindi ,

..hivi Mwakyembe na Mwandosya walipewa sumu?

..kwa mtizamo wangu kilichozima ndoto za Prof.Mwandosya ni maradhi yaliyompata.

..lakini hata kama angekuwa imara kiafya na ccm wakampitisha angepata wakati mgumu sana kwasababu siamini kama anaendana na siasa za wakati huu za hapa Tz.

..siasa za Tz na wapiga kura zinahitaji mgombea MACHACHARI kama JPM. Prof.Mwandosya yuko baridi na ni msomi-msomi sidhani kama waTz wangempa kura mgombea wa aina hiyo.
 
Mbeya nini, sumu ishasambaa Njombe, Iringa na Ruvuma, maneno yenu yanazalisha kanda nyingine itakayowasumbua bila kujua muendelee kuropoka tu bila kutumia busara
Mkuu kwani siasa nayo ugomvi?Ina maana wewe hutaki wapinzani nao watawale siku moja?nini basi maana ya vyama vingi! Kubali kataa one day yes!wajipange tu mbona unawaita sumu unataka tuwaue?Mie kwangu boss kubwa anachama chake na mie changu,watoto chao na maisha yanasonga bila shari.
 
Kushindwa kwa upinzani ktk uwakilishi bungeni huko kwenu inaeleweka ni nyota ya ukabila wa magufuri dhidi ya vyama vingine, mastermind wa kuchafua images zao ni chama chako cha ccm. Nyamagana mlipiga kampeni Usukuma wa mabula dhidi ya Ujaluo wa Wenje hadharani.

2010 inaeleweka fika uchaguzi ulikua Juma dhidi ya Peter ndio maana kura na viti vingi vilipatikana. Mkoa wa mbeya kuendelea ni juhudi binafsi za wanambeya as serikali ni wazi iliiona mbeya ya muhimu Joyce Banda aliposema ni sehemu ya Malawi.
 

Mkuu acha kufeli,mchizi alipata 5.0GPA undergrad pale FoE akaenda Birmingham,peleka wazungu to the end akapata uprofessor at very young age,he was the youngest electrical professor ever...

Dogo alikua hafai kabisa hata kwa kuchomelea....tumepita FoE tunamjua sana...dogo alikua genius Luhanga anasubiri sana...Luhanga alipita stages one by one,Mark aliruka ujinga wote,na marks zake were perfect scores....
 
Autupie jicho kivipi?uende ccm au?halafu we lijamaa inaonekana utawala huu unakuchefua na mda si mrefu utaitukana ccm waziwazi...ulitoa sana povu enzi za m.kw.ere,au ndio wapiga dili wenyewe?!!!
 
Autupie jicho kivipi?uende ccm au?halafu we lijamaa inaonekana utawala huu unakuchefua na mda si mrefu utaitukana ccm waziwazi...ulitoa sana povu enzi za m.kw.ere,au ndio wapiga dili wenyewe?!!!
Mi mwana CCM damu damu na uzuri wa demokrasia ni kusema kila kinachoenda kombo ili hata JPM apate habari, kwa nyie mnao mdanganya.
JPM rais wa wote.
Sinyi sumu wala sijinyongi, CCM pamoja na mapungufunyake ni.mbere kwa mbere!
 

Attachments

Mi hapo sijaona cha ajabu. Labda ungenitajia patents zake ndo ningeona maajabu. Uprofessor wa science and technology ni products na patents, sio sifa za kusema nilikuwa wa kwanza darasani.

Hiyo ndo tofauti ya MIT na vyuo vingine .
 
Mi mwana CCM damu damu na uzuri wa demokrasia ni kusema kila kinachoenda kombo ili hata JPM apate habari, kwa nyie mnao mdanganya.
JPM rais wa wote.
Sinyi sumu wala sijinyongi, CCM pamoja na mapungufunyake ni.mbere kwa mbere!
Mbona wakati wa jk ulikuwa unatetea kila ujinga!!sio bure dili zako ovu zimeminywa
 
Tutawatumia upinzani hili ndilo chaguo letu, nyinyi huko kwenu watumieni ccm. Huu ni uhuru wetu kama nyinyi mlivyo amua kuchagua ccm na msukuma mwenzenu. Na sie huku tutaendelea na upinzani as nafsi zetu zinakongwa nao.
 
Mbona wakati wa jk ulikuwa unatetea kila ujinga!!sio bure dili zako ovu zimeminywa
Usiwe na wasi mkuu, hivi kwa umri uliofikia umewahi kusikia mfanya biashara aliyekufa kwa kukosa biashara.
Hata sasa tunamtetea JPM katika kila kitu.
Nyie wajinga wajinga ndo msiolielewa hilo kuwa kelele zenu za mlango hazitunyimi usingizi.
 
Usiwe na wasi mkuu, hivi kwa umri uliofikia umewahi kusikia mfanya biashara aliyekufa kwa kukosa biashara.
Hata sasa tunamtetea JPM katika kila kitu.
Nyie wajinga wajinga ndo msiolielewa hilo kuwa kelele zenu za mlango hazitunyimi usingizi.
nafikiri mjinga ni wewe uliyedhani utaendelea kupiga dili kwa vile una kadi ya ccm,sasa hivi unaisoma namba huishi kukosoa lakini kwa watu kama sisi tunaotunza kumbukumbu hutotupata na unafiki wako wa kukosoa utawala huu(haimaanishi naunga mkono baadhi ya matendo ya awamu hii)..usirudie kuleta ujinga wako humu sababu bado tuna kumbukumbu za upuuzi wako wa kutetea kila kitu cha magamba ukiwa unapiga dili..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…