Mbeya: Housegirl achomwa moto miguu kwa mafuta ya kupikia

mtotomtamuu

JF-Expert Member
Dec 4, 2016
602
1,454
Mbeya. Mtoto Witnes Masondo (14) mkazi wa Kijiji
cha Kaganga Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya
ameunguzwa kwa mafuta ya kupikia katika miguu
yote kwa tuhuma za kuchelewa kupika mboga.
Mtoto huyo alikuwa akifanya kazi za ndani kwa
mkazi wa Uyole aliyetajwa kwa jina la Bupe
Benjamin.
1481453698398.jpg

Kwa mujibu wa maelezo ya Witnes, baada ya
kufanyiwa ukatili huo, bosi wake alimfungia ndani
kwa takriban mwezi mmoja.
Witnes akiwa ameambatana na mama yake mdogo,
Consolata Mgaya alisema alikuwa akifanya kazi za
ndani kwa mama huyo tangu Machi mwaka huu,
bila kulipwa mshahara.
Alisema siku ya tukio mama huyo alirudi jioni na
kuanza kumtuhumu kwa nini amechelewa kupika
mboga, akachukua mafuta ya kupikia yaliyokuwa
motoni kisha akammwagia miguuni.
“Aliponimwagia akaniambia hilo liwe fundisho,”
alisema mtoto huyo.
Alidai kuwa baada ya kitendo hicho alimpiga
marufuku kutoka nje, alikaa ndani takriban mwezi
mmoja akiugulia maumivu ya vidonda bila
kupatiwa matibabu huku akitishiwa kuwa kama
atasema kwa mtu yeyote, atamfanyia kitu kibaya
zaidi.
Witnes alisema kutokana na maumivu makali
aliyokuwa akiyapata, siku moja alitoka nje
kinyemela baada ya mama huyo kwenda kazini,
kisha akaomba msaada kwa mmoja wa majirani
ambaye alimsaidia kumpa nauli ya kurudi
nyumbani kwao Mbarali.
Mama yake mdogo, Consolata alisema binti yake
alifika nyumbani eneo la Ubaruku anakoishi
Desemba 6, mwaka huu akiwa na hali mbaya.
“Siku hiyo jioni, niliona wasamaria wema
wanamleta mtoto akiwa amechoka na kulia
kutokana na maumivu aliyokuwa akiyapata,
nilipomuuliza kulikoni akaanza kunisimulia
yaliyomkuta. Nikaamua kwenda kwa viongozi wa
Serikali ili kupata msaada zaidi,” alisema
Consolata.
Alisema alipokwenda kituo kidogo cha Polisi
kilichopo Ubaruku, aliamriwa aende kituo kikuu
cha polisi makao makuu mjini Rujewa kwa msaada
zaidi.
“Nilipofika niliandikwa PF3 na mtoto akaenda
kutibiwa hospitali ya Wilaya ya Mbarali, lakini
baadaye Polisi walinishauri nirudi Mbeya mjini
lilipotokea tukio nikaandikishe maelezo kwa hatua
zaidi za kisheria,” alisema.
Juzi, mama huyo akiwa ameambatana na mtoto
huyo, walifika Kituo Kikuu cha Polisi cha Mbeya,
kitengo cha dawati la kupinga ukatili wa kijinsia na
kutoa maelezo.
Consolata alisema baada ya kufika Hospitali ya
mkoa, mtoto huyo alilazimika kulazwa na hadi
jana alikuwa akiendelea kupatiwa matibabu
hospitalini hapo, huku polisi nao wakiendelea
kumsaka mtuhumiwa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Dhahiri
Kidavashari alisema hajapokea rasmi taarifa hizo,
lakini askari wake wa dawati la jinsia wanaendelea
kuifanyika kazi.
“Sijaipata taarifa hii rasmi kwa maana ya
maandishi ofisini, lakini za kuambiwa ninazo na
askari wangu wa dawati wanaendelea
kulishughulikia, tukipata taarifa zaidi
tutawajulisha,” alisema kamanda huyo

Source::Mwananchi
 
Unaposikia mtoto mdogo amewekwa kwenye friji au kuona video za watoto 'wakila vipondo' hayo ni matokeo ya vitendo kama hivi.



Wanaume wengi tunashindwa kuwatetea hawa watu 'wasaidizi wa ndani' kwa kuhofia kupoteza ndoa.

Sheria ichukue mkondo wake.
 
Hivi ni sheria gani inaruhusu mtoto wa miaka 14 kupewa majukumu ya nyumbani ya kusimia kila kitu........pumbavu sana hii nchi inamaana sheria haipo wazi kuwa mtoto ni chini ya miaka 18?!
Hawa watoto tunawaweka katika wakati mgumu sana future zao. Hebu sheria iwekwe wazi kuwa hakuna mtoto ambaye yupo chini ya umri wa miaka kumi na nane atapewa majukumu ya nyumbani kama hayo maana wengi wanakuwa ni wahanga wa kubakwa....kufanyiwa vitendo vya ukatili lakini pia hawapati haki ya kimsingi ya kucheza nakusoma kama ilivyo kwa watoto wenzao
 
Hivi kwanini ukatili wa aina hii kwa binadamu mwenzio!!!

Mabinti hawa huvumilia mengi sana, ndio maana huwa wanajifunza ukatili. Twapaswa kuwachukulia kama watoto wetu, tuishi nao kwa upendo.
Tatizo watu huwa wanataka wawe kama malaika, wasikosee.
 
Back
Top Bottom