mfuga kuku
JF-Expert Member
- Jul 14, 2014
- 750
- 544
Hii kesi inanifundisha kitu kimoja kikubwa sana kwangu! " Sio kila jambo linatakiwa kuwa wazi kwa wote" Kinachotusumbua nimeona ni uwazi na nia njema ya Serikali yetu ya Awamu ya Sita, huko nyuma mikataba yote ilikua kimya kimya na mambo yalikuwa shwari kabisa!Kama tulivyosema tangu awali , Shetani hajawahi kumshinda Mungu , hatimaye watuhumiwa wote wako huru
Masharti ya Dhamana kwa Mdude na Mwabukusi haya hapa .
View attachment 2720869
====
UPDATES; 1800HRS
=====
Mdude Nyagali na Boniface Mwabukusi waachiwa kwa dhamana.
Watuhumiwa wa kesi ya uhaini wakili Boniface Mwakubukusi na Mdude Nyagali waliokuwa wakishiliwa na jeshi la polisi Mkoa wa Mbeya wameachiwa huru wakibadilishiwa mashtakana na kuwa kesi ya uchochezi.
Wakili Mwambukusi na Mdude wamechiwa majira ya saa 11:30 jioni huku wakiwashukuru watanzania pamoja na mashirika mbalimbali huku wakieleza kuwa watatoa msimamo wao baada ya kukutana na Balozi Dk Wilbroad Slaa.
Wakili Philip Mwakilima anayewatetea Wakili Boniface Mwambukusi na Mdude Nyagali amesema kutoka na dhamana hiyo kosa la uhaini halipo tena hivyo wateja wake wamedhamiwa kwa kosa la uchochezi
Mwabukusi hivi karibuni aliwawakilisha wadai wanne katika kesi iliyofunguliwa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya kupinga mkataba wa ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai (IGA), akiwa kiongozi wa jopo la mawakili.
Kesi hiyo ya kikatiba namba 5 ya mwaka 2023 ilifunguliwa na Alphonce Lusako, Emmanuel Chengula, Raphael Ngonde na Frank Nyalus dhidi ya Serikali.
Agosti 10, mwaka huu Mahakama ilitoa hukumu ya kuitupa kesi hiyo ikisema haina mashiko.
Baada ya kesi kutupiliwa mbali, Jeshi la Polisi lilionya wanaoandaa maandamano ya nchi nzima ili kuiangusha Serikali kabla ya mwaka 2025, likisema waandaaji wanayahusisha na kushawishi jumuiya ya Watanzania kuwaunga mkono katika hoja kuhusu Bandari.
Bila ya kutaja majina au kikundi cha watu, Mkuu wa jeshi hilo (IGP), Camillius Wambura akizungumza na waandishi wa habari alisema kuna taarifa zinasambaa katika mitandao ya kijamii inayohusu maandamano hayo.
Hata hivyo, baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya kutoa hukumu katika kesi ya IGA, wakili Mwabukusi alitangaza uwepo wa maandamano.
Polisi: Tumemkamata Mwabukusi, Mdude kwa mahojiano
Jeshi la Polisi nchini lilithibitisha kuwakamata Wakili Boniface Mwabukusi na Mpaluka Said Nyagali maarufu kama Mdude kwa tuhuma za kutoa maneno ya uchochezi.
Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi, SACP -David Misime ilisema wawili hao wamekatwa kwa mahojiano ambayo yanaendelea.
“Jeshi la Polisi kama lilivyo eleza jana tarehe 11 Agosti 2023 linawafuatilia ili liwakamate watuhumiwa walioandaa na kutoa maneno ya uchochezi, kazi hiyo inaendelea kufanyika kwa mujibu wa sheria.
Mwabukusi alikuwa mmoja wa wanasheria waliofungua kesi ya kupinga mkataba uliofumgwa kati ya serikali na Dubai.
Kukamatwa kwa Mwabukusi kulikuja muda mfupi baada ya Mkuu wa Jeshi la Polisi kuutangazia ulimwengu, kwamba “kuna njama za kumuangusha Rais wa Jamhuri, Dk. Samia Suluhu Hassan.