Mbeya: Boniface Mwabukusi na Mdude Nyagali waachiwa kwa dhamana

hi

yo ni huruma tu ya rais na watulize matako yao hayo, umesahau wakili wao alivyokuwa anampigia magoti rais awaonee huruma maana Mwabukusi ana mishono na Slaa ni mzee. Rais wetu ana huruma na mcha Mungu wa kweli amewasikia sasa kuna lipi la ajabu. Mpongeze rais kwa utu alionao, watulie wawe raia wema. Ukweli tumeusikia wa kauli walizikuwa wanatoa hadharani, naamini hatarudia kutoa kauli za ajabu km zile za kugawa nchi na kuchochea chuki
Hakuna yoyote aliyempigiq magoti Samia, bali kuna chawa walipoona kuwa lazima akina mwabukusi waachiwe maana hakuna kesi yoyote, ikabidi wajitokeze kuhadaa umma, ili wakiachiwa ionekane rais ana huruma. CCM wanapopora chaguzi za nchi hawasababishi chuki na kuligawa taifa?
 
Kama tulivyosema tangu awali , Shetani hajawahi kumshinda Mungu , hatimaye watuhumiwa wote wako huru

Masharti ya Dhamana kwa Mdude na Mwabukusi haya hapa .

View attachment 2720869

====

UPDATES; 1800HRS

=====

Mdude Nyagali na Boniface Mwabukusi waachiwa kwa dhamana.

Watuhumiwa wa kesi ya uhaini wakili Boniface Mwakubukusi na Mdude Nyagali waliokuwa wakishiliwa na jeshi la polisi Mkoa wa Mbeya wameachiwa huru wakibadilishiwa mashtakana na kuwa kesi ya uchochezi.

Wakili Mwambukusi na Mdude wamechiwa majira ya saa 11:30 jioni huku wakiwashukuru watanzania pamoja na mashirika mbalimbali huku wakieleza kuwa watatoa msimamo wao baada ya kukutana na Balozi Dk Wilbroad Slaa.

Wakili Philip Mwakilima anayewatetea Wakili Boniface Mwambukusi na Mdude Nyagali amesema kutoka na dhamana hiyo kosa la uhaini halipo tena hivyo wateja wake wamedhamiwa kwa kosa la uchochezi

Mwabukusi hivi karibuni aliwawakilisha wadai wanne katika kesi iliyofunguliwa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya kupinga mkataba wa ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai (IGA), akiwa kiongozi wa jopo la mawakili.

Kesi hiyo ya kikatiba namba 5 ya mwaka 2023 ilifunguliwa na Alphonce Lusako, Emmanuel Chengula, Raphael Ngonde na Frank Nyalus dhidi ya Serikali.

Agosti 10, mwaka huu Mahakama ilitoa hukumu ya kuitupa kesi hiyo ikisema haina mashiko.

Baada ya kesi kutupiliwa mbali, Jeshi la Polisi lilionya wanaoandaa maandamano ya nchi nzima ili kuiangusha Serikali kabla ya mwaka 2025, likisema waandaaji wanayahusisha na kushawishi jumuiya ya Watanzania kuwaunga mkono katika hoja kuhusu Bandari.

Bila ya kutaja majina au kikundi cha watu, Mkuu wa jeshi hilo (IGP), Camillius Wambura akizungumza na waandishi wa habari alisema kuna taarifa zinasambaa katika mitandao ya kijamii inayohusu maandamano hayo.

Hata hivyo, baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya kutoa hukumu katika kesi ya IGA, wakili Mwabukusi alitangaza uwepo wa maandamano.

Polisi: Tumemkamata Mwabukusi, Mdude kwa mahojiano

Jeshi la Polisi nchini lilithibitisha kuwakamata Wakili Boniface Mwabukusi na Mpaluka Said Nyagali maarufu kama Mdude kwa tuhuma za kutoa maneno ya uchochezi.

Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi, SACP -David Misime ilisema wawili hao wamekatwa kwa mahojiano ambayo yanaendelea.

“Jeshi la Polisi kama lilivyo eleza jana tarehe 11 Agosti 2023 linawafuatilia ili liwakamate watuhumiwa walioandaa na kutoa maneno ya uchochezi, kazi hiyo inaendelea kufanyika kwa mujibu wa sheria.



Mwabukusi alikuwa mmoja wa wanasheria waliofungua kesi ya kupinga mkataba uliofumgwa kati ya serikali na Dubai.


Kukamatwa kwa Mwabukusi kulikuja muda mfupi baada ya Mkuu wa Jeshi la Polisi kuutangazia ulimwengu, kwamba “kuna njama za kumuangusha Rais wa Jamhuri, Dk. Samia Suluhu Hassan.
Ingelikuwa maneno yale aliyosema Slaa ni mtu kutoka Zanzibar asingebadilishiwa mashtaka na kuwa uchochezi na wala kusingekuwa na dhamana
 
Walijichanganya sana kujifanya wanawashtaki kwa uhaini. Ni aibu kubwa sana kwa serikali.
Wamebadilishiwa kwa sababu wanatoka Tanganyika ingekuwa ni kutoka Zanzibar wangekuwa ndani hadi sasa ndio maanza Zanzibar wanataka kuvunja muungano kwa uonevu dhahir kutoka JMT
 
Raisi anajiabisha sana
Samia anakusaidieni sana tanganyika mtu aongea kupindua serikali lakini kwa huruma ya mama anabadilishiwa mashtaka ingekuwa ni kutoka Zanzibar maneno yale wangesekwa ndani kusikojulikana
 
Sipati picha ya Lissu atakachoongea
Lissu hanisi tu, sasa kaufyata karudi kwa daktari wake baada ya kuona wenzake wanatiwa mbaroni, Lissu na Chadema ata haziendi tena kila mtu kivyake yeye mbowe chadema hamna kitu usaliti mtupu
 
Back
Top Bottom