Mbeya: Baba atoa ushahidi uliosaidia mwanae ahukumiwe kunyongwa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,569
9,429
Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya kwa kusaidiwa na ushahidi wa Baba mzazi wa Mshitakiwa imemhukumu kunyongwa hadi kufa, Godfrey Sichizya(25) baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumuua Babu yake ili achukue Ng'ombe wake 9.

Akisoma hukumu hiyo katika Mahakama ya Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe, Jaji wa Mahakama Kuu, Atuganile Ngwala alisema baada ya kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili aliridhika pasipo na shaka yoyote kuwa mshitakiwa alimuua Babu yake Labson Sichizya kwa kukusudia.

Alisema ameridhika na ushahidi uliotolewa na Meas Sichizya ambaye ni Baba Mzazi wa mshitakiwa pamoja na Mashaka Sichizya ambaye ni ndugu wa damu, ambao kwa pamoja na wanakijiji walimkamata mshitakiwa na kumpeleka Kituo cha Polisi.

Jaji Ngwala alisema Godfrey kwa maelezo yake kwa mlinzi wa amani alisema alimuua Babu yake ili achukue Ng'ombe tisa waliokuwa wakimilikiwa na Babu huyo.
⁠⁠⁠⁠
 
Umaskini ni mbaya sana.
Njaa mbaya zaidi.
Tamaa ndiyo hatari kuliko hatari yenyewe.
 
Mtoto kaua baba wa baba yake.

Mtoto anasimama upande wa baba yake maana huko ndiko fungu lake lilipo.
 
Back
Top Bottom