Mbele ni kule unakokwenda au unakotoka??

kauleni

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2009
Posts
356
Reaction score
113
Kulikuwa na msomi mmoja miaka ya sabini huko Mbinga ambaye aliitwa Bambo na kitaaluma alikuwa bwanashamba ila kwa kipindi hicho ninamfahamu alikuwa amechanganyikiwa (mgonjwa wa akili).
Hakuwa mtu wa fujo ila alikuwa muulizaji maswali mazito na yenye mantiki kwenye mikutano ya hadhara hadi ikapelekea kuwekwa ndani pale viongizi wa kitaifa walipotembelea Mbinga kwa hofu ya uongozi wa wilaya kuumbuliwa.
Kwa sisi watu wa kawaida mkikutana njiani anaweza kukuuliza "eti kati ya huko unakokwenda na huko unakotoka mbele ni wapi"??
Kwa mtazamo wake mbele ni kule unakotoka kwa sababu unaweza kuelezea yote uliyoyaona , na kwamba uendako ni nyuma kwa sababu yaliyo mbele yako huyajuwi.
Je alikuwa sahihi??
 
inawezekana nyinyi ndio mlikua wagonjwa wa akili kwa kuwa yeye mwenye akili yupo peke yake mkamtoa akili kwa kigezo cha wingi wenu na sio facts

Ni kawaida kukosolewa unapokua peke yako against all..!!
 
Ukikutana nae muulize. Yeye anakwenda mbele kimbelembele au anakwenda mbele kinyumenyume? Akikujibu hili swali basi utajuwa mbele ni wapi na nyuma ni wapi
 
Kwa hiyo unakubaliana naye
 
Alikuwa anajifanya Socrates eeh? Kulingana na Kezilahabi, wagonjwa wa akili na vichaa ndiyo wana maarifa ya kweli na ndiyo watatuletea mabadiliko ya kweli!
 
Kulikuwa na msomi mmoja miaka ya sabini huko Mbinga ambaye aliitwa Bambo na kitaaluma alikuwa bwanashamba ila kwa kipindi hicho ninamfahamu alikuwa amechanganyikiwa (mgonjwa wa akili).
Hakuwa mtu wa fujo ila alikuwa muulizaji maswali mazito na yenye mantiki kwenye mikutano ya hadhara hadi ikapelekea kuwekwa ndani pale viongizi wa kitaifa walipotembelea Mbinga kwa hofu ya uongozi wa wilaya kuumbuliwa.
Kwa sisi watu wa kawaida mkikutana njiani anaweza kukuuliza "eti kati ya huko unakokwenda na huko unakotoka mbele ni wapi"??
Kwa mtazamo wake mbele ni kule unakotoka kwa sababu unaweza kuelezea yote uliyoyaona , na kwamba uendako ni nyuma kwa sababu yaliyo mbele yako huyajuwi.
Je alikuwa sahihi??

mh complcatd
 
Ukikutana nae muulize. Yeye anakwenda mbele kimbelembele au anakwenda mbele kinyumenyume? Akikujibu hili swali basi utajuwa mbele ni wapi na nyuma ni wapi

Siku zote alikuwa anakwenda mbele kimbelembele. Yeye alisisitiza kuwa kilicho akilini mwake baada ya kukiona ndicho kilicho mbele na kile ambacho hajakiona kipo nyuma. Mfano wa kilicho usoni na kisogoni.
 
Back
Top Bottom