Mbegu za majani Mchunga zinapatikanaje?

Feb 12, 2017
12
6
Majani haya yaitwayo mchunga hupendwa sana kuliwa na sungura kwani ni machungu,japo baadhi ya watu huyatumia kama mboga.je kuna upatikanaji wa mbegu zake katika maduka ya pembejeo?
 
Nilipokuwa singida yalikuwa yanapatikana kwa wingi,kwa sasa nipo ukerewe yanapatikana kiasi,nilikuwa nauliza upatikanaji wa mbegu kusudi nilime mwenyewe.
 
Mkuu hiyo ni mboga yetu, mbegu zake unangoja yale maua ya njano yakikauka yanakuwa na mbegu nyeusi.
Screenshot_20220514-130128.png

Nimejaribu, imewezekana!
 
Mkuu huu mmea ukikomaa unatoa maua ya njano ndani yake Kuna mbegu, vuna maua kabla ya halijakauka Kisha unalikausha kwa kuweka juani likiwa ndani ya karatasi (mbegu zake Zina asili ya kupeperuka na upepo).

Ukiwa na haraka chimbua mmea ukiwa na mzizi wake kata shina majani yabaki kama manne Kisha panda.
Mbegu yake umepataje
 
Back
Top Bottom