Mbegu ya papai na tikiti | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbegu ya papai na tikiti

Discussion in 'JF Doctor' started by Hajiii, Jun 11, 2012.

 1. H

  Hajiii Member

  #1
  Jun 11, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hi Jf doctors!naomba kujua maajabu ya mbegu za papai na tikiti katika mwili wa binadam vilele maajab ya Mloge maana nimekuwa nikisikia tu kwa muda mrefu sasa kwamba mazao hayo ni tiba kubwa.
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Jun 12, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  mti wa papai.jpg

  Papai
  Papai
  Papai ni tunda la mmea unaofahamika kama "carica papaya" wa jenasi corica, unaasili ya amerika ya kaskazini na unakuwa huko maksiko, karne kadhaa kabala ya kuibuka kwa tamaduni mpya za huko amerika, Ni mti mkubwa wenye shina la urefu wa mita 5 mpaka 10, yenye majani yaliojipanga yaliojizungusha na kujishikiza juu kwenye shina la miti, shina kwa upande wa chini huwa na makovu mengi kuonesha sehemu ambayo majani yalikuwa majani ya mpapai ni makubwa sm 50 – 70 kwa upana, maua yake ni madogo na hutokea sehemu yalipochomoza majani, hutengeneza tunda papai lenye urefu wa sm 15- 45, na upana wa sm10 – 30. Tunda huiva pale linapokuwa laini ( kama vile parachichi au zaidi) na ngozi yake inapokuwa na ngozi yake inapo karibia rangi ya chungwa ladha ya chungwa hukamilana na ile kati ya nanasi na peasi, ingawa huwa ya utulivu bila ya uchungu wowote.
  [hariri]Wingi na matumizi ya papai


  Kutoka asili yake ya Meksiko, Puerto rico amerika ya kati na kusini mwa asia .
  Papai lililoiva huliwa bila ya maganda wala mbegu zake papai bichi huliwa baada ya kuchemshwa na kupimwa pamoja na saladi ya michemsho mingine.
  Papai bichi na mti wake huwa na utovu. Yenye kemikali inayoitwa ‘papari' ambayo hutumika kulainisha nyama kwa kuvunjavunja protini iliyondani yake. Uwezo wake huu wa kulainisha nyama ngumu umetumiwa tangu enzi za zamani na watu wa kale.
  Wanawake huko india, Pakistani, sililanka walitumia sana papai kama njia ya kuzuia mimba na hata kutoa mimba wanawake waliokuwa utumwaniai pia walionekana sana wakitumia sana papai ili kuzuia wasishike mimba na kuwazaa watoto wao utumwani imegundulika hatambegu za papai nazo huweza kusababisha kuondoa uwezo wa kuzaa kwa wanaume.
  Shina na matawi ya mipapai pia yanatumika kutengenezea kamba. mbegu zaidi za mipapai huweza kuliwa na zina radha kali sana. Hu8sagwa na wakati mwingine na kutumiwa kama mbadala wa pilipili. Sehemu Fulani za asia, majani machanga ya mmea wa mpapai huchemshwa kwa mvuke na kuliwa kama spinachi. Sehemu Fulani duniani majani ya mpapai hunyweshwa na chai kama dawaya kutibu malaria, japo hakuna ushahidi wa kutosha juu ya matibabu haya.
  [hariri]Hatari ya matumizi ya papai na mazao yake


  Tunda la papai, mbegu na utomvu wake, pia majani yake yana kiwango kikubwa cha carpaine' kemikali inayoondoa minyoo kwenye mwili lakini matumizi ya kiasi kikubwa huweza kuwa hatari. Inafahamika kuwa mapapai mabichi yanaweza kusababisha kutoka kwa mimba kutokana na kiwango kikubwa cha kemikali ya Latex ambayo husababisha kuta za uterasi kusinyaa japo haijathibitishwa bado. Kula sana mapapai kama ilivyo kwa karoti, huweza kusababisha ugonjwa wa karotinemia ambapo nyayo na viganja huwa vya rangi ya njano japo hakuna madhara yoyote.

  Mbegu za Matikiti maji faida yake ni hii: chukua mbegu za tikiti maji zikaange halafu zitwange ili zitoe unga, chukua juici ya kitunguu thaumu lita moja na asali lita moja changanya pamoja juisi ya kitunguu thaumu na asali weka na vijiko kumi vikubwa vya unga wa tikiti maji koroga vizuri na uwe unakunya dawa hii kikombe kimoja cha kahawa mara tatu kila siku kwa muda wa wiki moja.


  Jamani Mlonge ni dawa na tiba kubwa sana
  Nimesikia mengi kuhusiana na mti wa Mlonge lakini hii ni kali zaidi
  CAPE TOWN, (IPS). Wakati tatizo linalipolikabili Bara la Afrika, watu wanaangalia uwezekano wa kupata misaada kutoka kwenye mashirika ya kimataifa kutoka nje ya bara hilo.


  Lakini hali ya ukame inayoongezeka kwa kasi, miti yenye kuhimili ukame huku ikiwa na majani yenye viini lishe vingi inaweza kuwasaidia watu maskini, pia maeneo ya usalama wa chakula na utapiamlo, wao wenyewe.


  Shamba lenye hekta 15 lilipandwa miti ya Mlonge au wengine huuita mti wa miujiza ambao kwa Kiingereza unaitwa Moringa Oleifera, tayari umeshaanza kuleta mabadiliko katika jimbo moja maskini zaidi la Afrika Kusini la Limpopo.


  Majani ya Mlonge yamepachikwa jina la chakula chenye viwango kwasababu wanasayansi waligundua yana kiasi cha madini ya Kalisium yanayoweza kupatiakana katika glasi nne za maziwa, kiasi cha vitamini c inayopatikana kwenye machungwa saba, Potasium ya kwenye ndizi mbivu tatu. Pia unapata kiasi cha madini ya chuma mara nne zaidi ya kiasi kile kinachopatikana kwenye spinachi. kiasi cha vitamani A mara nne zaidi ya kile kinachopatikana kwenye karoti na kiasi cha protini mara mbili zaidi ya kile kinachopatikana kwenye maziwa. Ukiwa na mti wa Mlonge ni sawa na kuwa na Supermarket kwenye mti.
  Mavis Mathabatha aliyewahi kuwa mwalimu kutoka Tooseng, amekuwa akifanya bidii ya kufungua mashamba ya Mlonge kwa kipindi cha miaka mitatu sasa ambalo litamuwezesha kuzalisha majani ya kutosha ya Mlonge ili kusaidia kuleta mabadiliko katika jamii yake.
  "Nataka kuleta mabadiliko katika jimbo langu na nchi nzima kupitia mradi huu," alisema.
  Mwaka 2009, alianza kuvuna na kuyakausha na kisha kuyasaga majini ya Mlonge kutoka kwenye miti michache aliyokuwa ameipabnda.
  Unga huo wa Mlonge alikuwa ukiwachanganyia watoto 400 kutoka katika familia masikini waliokuwa wakipata chakula kutoka kwenye kituo maalum.
  Kituo hicho kinalisha watoto wanaotoka katika familia zenye kipato kidogo ambacho kiko chini ya dola 250 kwa mwezi.
  Hii inahusuisha watoto wote wa kike na kiume kutoka kwenye jamii hiyo ambayo ina tatizo la ukosefu wa ajira, umasikini na utapiamlo, wengine wana maambukizi ya UKIMWI.


  "Matokeo yake yalikuwa dhahiri kwa muda mfupi sana, Afya za watoto ziliboreka kwa muda mfupi.
  Anasema Elizabeth Serogole, meneja wa kituo hicho cha kulisha watoto ambaye anafanya kazi kwa kushirikiana na Mathabatha.
  Anasema watoto wengi waliokuwa wakionesha kuwa na utapiamlo, kama vile vidonda kwenye ngozi walianza kupona mara baada ya kula mlo huo uliochanganywa na unga wa Mlonge.


  Nyongeza hiyo ya Mlonge kwenye chakula chao iliwasaidia kupambana na magonjwa mengine yaliyojitokeza, pia iliwasaidia kuboresha uwezo wao wa kiakili," anasema Seregole.


  "Wengi sasa wanaweza kusoma vizuri shuleni," anasema. Walichokuwa wanahitaji ni kjiko kimoja cha unga wa molonge katika chakula chao kwa siku. Dk.Samson Tesfay anayseoma Afrika Kusini kwenye chuo kikuu cha Zulu Natal idara inayohusika na masuala ya mbogamboga na matunda,alisema Mlonge ni mmea wenye kutenda maajabu kwenye lishe.


  "Mlonge ni mmea wa kipekeeunaoweza kuutumia kwa faida nyingi, kama vile dawa, chakula, kuponyesha viungo mwilini na kusaidia kupambana na utapiamlo," anasema.


  Source-Gazeti la Nipashe Ijumaa Februari 24, 2012


  Binafsi nimeshasikia kuwa Mlonge unatibu magonjwa 300, bila ya kusahau kansa,maralia,vidonda vya tumbo,kuondoa sumu mwilini na hata kuongeza nguvu za kiume. Maderava wengi wa safari ndefu hutumia Mlonge kuondoa uchovu. Mlonge watu wa kule Tanga wanatumia kama mti wa kujengea fensi, Uzaramoni umepandwa karibu kabisa na vyoo vyao, Dodoma na Morogoro umejaaa tele. Dar mbegu zake zinauzwa kwa Shilingi 1000 kwa pakti.


  Mbegu hizo zina dozi ya 3x3x3 na ukizila kwa wingi huweza kukufanya kuhalisha na kutoa uchafu mwilini. Tafakari ndugu yangu dawa tunazo tunatimia madawa yenye sumu yaliyotayalishwa na wazungu.... Tafakari.

  https://www.jamiiforums.com/jf-doctor/228105-jamani-mlonge-ni-dawa-na-tiba-kubwa-sana.html HAJII
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. B

  Bichau Member

  #3
  Jun 12, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante kwa taarifa njema, mungu akuzidishie yalo mema.
   
 4. E

  Ernest Da Vinci Senior Member

  #4
  Jun 12, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 115
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kwa nyongeza katika hlo la mlonge ni kwamba mbegu zake zikitafunwa na kushushia na maji ni tiba ya kisukari na figo.
   
 5. B

  Bichau Member

  #5
  Jun 12, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hebu naomba maelezo ya kutosha kuhusu dawa ya kisukari maana ni mhanga wa mtihani huo. Je hizo mbegu zatakiwa kunywewa mara ngapi kwa siku na zikiwa mbichi au kavu?:angry:
   
 6. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #6
  Jun 13, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  MZIZIMAKAVU tunashukuru kwa malelzo yako. ila naomaba unisaidie kwenye hili linatibu nini?
  Mbegu za Matikiti maji faida yake ni hii: chukua mbegu za tikiti maji zikaange halafu zitwange ili zitoe unga, chukua juici ya kitunguu thaumu lita moja na asali lita moja changanya pamoja juisi ya kitunguu thaumu na asali weka na vijiko kumi vikubwa vya unga wa tikiti maji koroga vizuri na uwe unakunya dawa hii kikombe kimoja cha kahawa mara tatu kila siku kwa muda wa wiki moja.

   
 7. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #7
  Aug 13, 2014
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,701
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Mlonge mlonge ndio mpango mzima.
  Nalog off
   
 8. First Born

  First Born JF-Expert Member

  #8
  Sep 16, 2014
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 5,315
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #9
  Sep 16, 2014
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Bibie Mwanaweja Ni Dawa ya kila maradhi haswa kwa wanaume nguvu za kiume na maradhi mengine pia inatibu.
   
 10. Bavaria

  Bavaria JF-Expert Member

  #10
  Sep 16, 2014
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 44,102
  Likes Received: 11,254
  Trophy Points: 280

  Mlonge una ladha gan mkuu?? Usikute kama mwarobaini au alovera.
   
 11. mkalee

  mkalee Member

  #11
  May 2, 2016
  Joined: Oct 20, 2015
  Messages: 54
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 15
  Ndio mlonge ndio baba lao.....
   
Loading...